econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Habari wanajamii.
Tangu Lissu atangaze Nia ya kugombea uenyekiti kumetokea kelele za kila aina. Mara ni kirusi ndani ya CHADEMA, mara anafadhiliwa na Msigwa, mara anampango wa kuhamia CCM nk. Kila mtu anasema la kwake.
Nikawaza, Kwanini kelele zimekuwa nyingi kwa Lissu baada ya tangazo lake la kugombea uenyekiti tofauti na Wenje alipotangaza kugombea umakamu mwenyekiti wa CHADEMA.
Kumbuka ya kwamba Wenje alitangaza kuitaka nafasi aliokuwa nayo Lissu. Lakini hakuna aliyemshukia Wenje kwamba ni msaliti au kirusi ndani ya CHADEMA Kwa kutaka nafasi ya anayoshilia Lissu.
Hii sintofahamu inaonesha labda watu walidharau tangazo la Wenje au walimwona ni dhaifu kupambana na Lissu kwenye umakamu Mwenyekiti. Hivyo wakampuuzia. Ila kwa Lissu wamepiga mayowe labda kwa sababu Lissu ana ushawishi ndani ya CHADEMA na anaweza kushinda nafasi hivyo au Lissu anawanachama wengi wanaomuunga mkono kiasi kwamba akifanyiwa figisu anaweza kuhama na kundi kubwa Kama kipindi kile Cha akina Zitto Kabwe na wenzake akina Prof Mkumbo.
Muda utasema na kutoa majibu.