econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
- Thread starter
- #41
Hahaha hakuna asiyetaka agombee, wafuasi wa Lisu ndio wanataka penalt ya bure na hawataki golikipa golini.
Tunajisahau kama chama cha demokrasia, halafu tunataka kukiuka kanuni zetu wenyewe. Hakuna anayemfananisha na Nyerere. Nyerere yupi maana siku hizi wako wengi, kama yule anayeitwa baba wa taifa hana mfano wa kuigwa.
Alipewa nchi na wingereza, hakugombea, na alijipa uwenyekiti wa chama na urais hakuchaguliwa mpaka anaondoka.
Mbowe anachaguliwa kila uchaguzi unapofika, akiwa ni mgombea naye anastahili kuwa na base yake na anatakiwa afanye kampeni.
Lakini wafuasi wa Lisu hawataki mtu mwingine yeyote agombee na Lisu. Wanataka Lisu ashindanishwe na Lisu tu, nasiyo mtu mwingine yeyote, hapo mnakuwa hama tofauti na CCM, ambaye Mwenyekiti wake anapitishwa tu akiisha kuwa Rais.
Sisi tunaolilia haki kila siku tutataka Lisu wetu apitishwe bila kupingwa. Huyo Lisu ndiye mwenye haki pekee ndani ya Chadema, demokrasia mnaitupa wapi na kwanini?
Mnamlemaza mgombea wenu, na mnasahau misingi mnayoipigania kila siku.
Hivi wanaolalamika ni wafuasi wa Lissu au Mbowe. Maana tangu Lissu achakue fomu kelele zimekuwa nyingi dhidi yake. Si ulimsikia yule mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya.