Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na huo ndio mwanzo wa ubabe, fitina, kuhasimiana, ugomvi, na mwishowe talaka tatu. Kuna mmoja alirusha dongo zito eti bundi ametua kwa majirani.
Mama alisema huyu ni simba na unajua kitisho cha simba! Kila mdudu katishiwa maslahi yake yani so attack lazima! Ila simba alisema internet warriors hawamnyimi chembe ya ucngz alishindwa jiwe itakuwa hawa fomfoo?
Inakuhusu nini, wewe umeshindwa mangapi? Acheni kuleta ujinga kwenye taasisi zinazoendeshwa na katiba, watu mnashupaza shingo wakati hamjawahi ongonza ata Nyumba kumi ,pumbavu
Sisi ccm mbona tushakaa mingi tu ?Angalau Zitto alionesha ukomavu akastaafu. Hovyo ana ka uhalali la kusema hivyo. Mbowe ajifunze kitu kutoka kwa Zitto.
Nilichogundua chadema ina tabia zile zile za unafiki wa CCM. Yaani madhaifu ya wazi wanaogopa kusema ili kulinda vyeo vyao ndani ya chama. Ila siku Mbowe aking'atuka utasikia wakimsema na kumlaumu..... tabia zile zile za CCM.
Kwa staili hii tunadaije demokrasia kama sisi wenyewe hatuiheshimu. Usishangae wakaibuka watu wakasema fomu iwe moja tu au Lissu avuliwe uanachama.
Mbowe bado ana ushawishi hata asipokua mwenyekiti na licha ya kwamba namsupport Lissu ila I'm sure Mbowe ana wajumbe wengi zaidi sababu hakuna mwanasiasa yupo chadema bila influence ya Mbowe.
Kwahiyo angeacha tu demokrasia ichukue mkondo wake I believe anaweza kushinda ingawa kunaweza tokea suprise akaangushwa na inaweza leta damage kwa reputation yake na hata akishinda itaonekana ametumia incumbency kubakia madarakani so either way its a lose-lose situation.
Busara ni kwamba apishe ili awaachie Lissu, Heche, Mnyika etc wagombee uenyekiti kwa open primaries kabisa na hatimaye apatikane mwenyekiti mmoja wa kutuvusha 2025.
In a worst case scenario, Mbowe akigombea na kushinda basi Lissu ateuliwe ukatibu mkuu maana Mnyika amepwaya sana bora arudi kwenye kurugenzi ya Mawasiliano aliyokua anaimudu vizuri zaidi na ambayo Mrema ameprove kuwa failure.
Kelele lazima ziwepo ,Lissu ni msomi na Mzee Mbowe alifeki elimu ya sekondari ndio maana hakuweza kuendelea na masomo ya elimu ya juu .Habari wanajamii.
Tangu Lissu atangaze Nia ya kugombea uenyekiti kumetokea kelele za kila aina. Mara ni kirusi ndani ya CHADEMA, mara anafadhiliwa na Msigwa, mara anampango wa kuhamia CCM nk. Kila mtu anasema la kwake.
Nikawaza, Kwanini kelele zimekuwa nyingi kwa Lissu baada ya tangazo lake la kugombea uenyekiti tofauti na Wenje alipotangaza kugombea umakamu mwenyekiti wa CHADEMA.
Kumbuka ya kwamba Wenje alitangaza kuitaka nafasi aliokuwa nayo Lissu. Lakini hakuna aliyemshukia Wenje kwamba ni msaliti au kirusi ndani ya CHADEMA Kwa kutaka nafasi ya anayoshilia Lissu.
Hii sintofahamu inaonesha labda watu walidharau tangazo la Wenje au walimwona ni dhaifu kupambana na Lissu kwenye umakamu Mwenyekiti. Hivyo wakampuuzia. Ila kwa Lissu wamepiga mayowe labda kwa sababu Lissu ana ushawishi ndani ya CHADEMA na anaweza kushinda nafasi hivyo au Lissu anawanachama wengi wanaomuunga mkono kiasi kwamba akifanyiwa figisu anaweza kuhama na kundi kubwa Kama kipindi kile Cha akina Zitto Kabwe na wenzake akina Prof Mkumbo.
Muda utasema na kutoa majibu.
Mbowe dikteta kama Putin, kajimilikisha chama kama chake binafsi, kisa baba mkwe. Mbowe hata angekuwa raisi angeng'ang'ania madaraka. CHADEMA wakimrudisha Mbowe hawana haki ya kudai Katiba Mpya ya nchi.
Mbowe aachie kiti, udikteta ni pamoja na kuzuia viongozi wengine wasi emerge. Fear of unknown inawasumbua, kwamba kisa Mbowe ana influence sasa hivi na amekiongoza chama kwa muda mrefu then hakutaweza kutokea kiongozi mwingine atakaye lead chama vizuri zaidi ya yeye, this is fear of unknown....
Gentleman,Habari wanajamii.
Tangu Lissu atangaze Nia ya kugombea uenyekiti kumetokea kelele za kila aina. Mara ni kirusi ndani ya CHADEMA, mara anafadhiliwa na Msigwa, mara anampango wa kuhamia CCM nk. Kila mtu anasema la kwake.
Nikawaza, Kwanini kelele zimekuwa nyingi kwa Lissu baada ya tangazo lake la kugombea uenyekiti tofauti na Wenje alipotangaza kugombea umakamu mwenyekiti wa CHADEMA.
Kumbuka ya kwamba Wenje alitangaza kuitaka nafasi aliokuwa nayo Lissu. Lakini hakuna aliyemshukia Wenje kwamba ni msaliti au kirusi ndani ya CHADEMA Kwa kutaka nafasi ya anayoshilia Lissu.
Hii sintofahamu inaonesha labda watu walidharau tangazo la Wenje au walimwona ni dhaifu kupambana na Lissu kwenye umakamu Mwenyekiti. Hivyo wakampuuzia. Ila kwa Lissu wamepiga mayowe labda kwa sababu Lissu ana ushawishi ndani ya CHADEMA na anaweza kushinda nafasi hivyo au Lissu anawanachama wengi wanaomuunga mkono kiasi kwamba akifanyiwa figisu anaweza kuhama na kundi kubwa Kama kipindi kile Cha akina Zitto Kabwe na wenzake akina Prof Mkumbo.
Muda utasema na kutoa majibu.
Mi sidhani kama hiyo ndiyo tatizo, na sidhani kama Mbowe kamzuia mtu kugombea hiyo nafasi, mi naona wengi wanamtaka Lisu, na wanataka awe mwenyekiti wa chadema, lakini hao hao hawataki demokrasia.
Ile nafasi inagombewa, na mgombea siyo Lisu pekee, wapo wengine wanania ya kugombea pia. Na mwenyekiti aliyepo, asiporwe haki yake ya kugombea eti tu kwa sababu amekuwa mwenyekiti kwa muda mrefu.
Kila siku tunapinga utaratibu wa kupita bila kupingwa, tunataka uchaguzi na kura ndiyo iamue mshindi, lakini kuna watu tayari wanamuaona Lisu ndiye mshindi hata kabla ya uchaguzi, demokrasia mmeiacha wapi?
Kumpigia kampeni mgombea siyo tatizo, lakini kuna wanaoenda mbali na kusema eti Mbowe akigombea huko ni kung'ang'ania madaraka!?
Yani nafasi ya demokrasia haitakiwi anapokuwa ni Lisu, na ni lazima ashinde Lisu, kwanini?
Mbowe haachii kiti, Mbowe ashindanishwe na Lisu ili kuleta usawa na haki ndani ya CHADEMA. Kama mnataka aachie, kwanini tunawapinga CCM wanaosema WATANZANIA WALIISHA AMUA S.S.HASSAN MITANO TENA?
Je tukubali Tanzania ni ya CCM peke yao, kaiiba kura ni sawa, wakijitangaza washindi hata waliposhindwa ni sawa?
Tunataka demokrasia lakini hatuitaki inapokuja kwa mgombea wetu wenyewe?
Yani tunapotaka vyetu ,tuko tayari kuminya haki za wengine, ni sawa?
Lisu is known, sijui fear of unknown inatoka wapi?
Lisu ni makamu mwenyekiti chadema, anayoyalalamikia anashindwaje kuya address ndani ya chama?
Watu tunataka sympathy kwa mgombea wetu, huo ni udhaifu ninao uona mimi kitaifa, utahurumiwa ndani ya CHADEMA, Ok Mbowe hata gombea utashinda, ikifika general election tutaomba SS.Hassan amwachie T.Lisu kwa sababu CCM imekuwa madarakani muda mrefu?
Au tutawaambia wananchi CCM wanaogopa T.Lisu asitawale kwasababu they have fear of unknown?
Agombee, aache kuomba huruma ya wananchi na wanachama wa chadema.
Sawa agombee ila na nyie wafuasi wake msipite na huo upepo wa kwa vile amekiongoza chama kwa muda.mrefu hawezi tena kupata mpinzani ndani ya chama kama mnavyofanya, wengine mmeenda mbali kumfansnisha mbowe na Nyerere ili tu kumpa green tick Jesus! Ndio maana na sisi tunakuja na fear of unknown....wagombee wote ila msitu influence ujinga ujinga
Zitto hakuondoka wakati mmoja na akina Prof Mkumbo. Zitto alifukuzwa mapema kabisa. Akina Mkumbo waliondoka majuzi baada ya chadema kukodishwa kwa Lowassa ili agombelee urais. Hapo ndipo kundi kubwa tuliondoka.