Kwanini Kikwete hakumshauri Samia amteue Prof. Mwandosya kuwa Makamu wake wa Rais?

Kwanini Kikwete hakumshauri Samia amteue Prof. Mwandosya kuwa Makamu wake wa Rais?

-atakuwa na yeye alishauriwa na profesa wa sheria, yeye ndio akaenda kwenye baraza la mawaziri kutoa hoja na sifa akapata yeye,
Hapana, katika kitabu chake aliandika kwamba kulikuwa na tafrija iliyoandaliwa na Misri usiku wa kabla ya asubuhi ya kutia sahihi makubaliano. Mawaziri wengine wakaenda kwenye tafrija yeye akaamua kutoenda na usiku huo kuusoma mkataba kwa makini ndio akagundua mapungufu yake. Kwa hiyo ile tafrija ilipangwa na wa Misri kimkakakati.

Halafu huu mpango wa kutowapa viongozi nafasi ya kusoma mikataba kwa makini ni ujanja unatumiwa na watu wengi sana.

UKienda China, mkiwa mnajadili mkataba wanawaweka kwenye chumba baridi sana, na wanasema hawawezi kupunguza baridi kwa sababu ni mfumo uko automatic. Basi inabidi ukubaliane nao haraka haraka ili utoke kwenye baridi. Pia inasemekana mwili ukiwa na baridi sana uwezo wa kufikiri unapungua kidogo
 
Juzi hapa ilitangazwa kwamba Prof. Mwandosya ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa EWURA. Wengi walishangaa kwa nini Prof. Mwandosya kaletwa kutoka hali ambayo wengi wetu tulidhani ni ustaafu na kurudi kuwa Mwenyekiti wa EWURA.

Lakini hatupaswi kushangaa. Uteuzi wa Prof. umetukumbusha pia kwamba wakati Mkapa akikabiliwa na sakata la ununuzi wa rada toka Uingereza, ni Prof. Mwandosya alipewa jukumu la kuliweka sawa jambo hilo, hadi kukawa na joke kwamba Prof. Mwandosya alim-charm yule mwanamke wa Uingereza aliyekuwa akitutuhumu vikali hadi akabadilika na kusema "it wa a very wise decision by Tanzania to buy the radar!"

Na pia kwa mlio na ufahamu, wakati uhusiano kati ya Kiwete na Kagame umeharibika sana hadi Kagame kutishia kumpiga Kikwete ni Prof. Mwandosya alitumwa Rwanda kwenda kuweka mambo sawa.

Na labda niwaambie siri nyingine, wakati Kikwete anaona anashambuliwa kila kona kwa kuwa raisi dhaifu, ni Prof. Mwandosya aliitwa ofisi ya Raisi kama waziri asie na wizara maalum na kuwa mshauri wa karibu wa Kikwete. Matokeo tukayaona, ghafla Kikwete akaanza kuonekana kuwa na busara sana nchini na nje ya nchi. Ilifikia hatua watu wakasema unajua Kikwete aliwahi kugombea uraisi angegombea awamu ijayo maana busara zimekuja mwishini mwa awamu yake, bila kutambua kuwa kulikuwa na busara za Prof. Mwandosya nyuma ya utendaji wa Kikwete katika sehemu kubwa ya awamu ya mwisho ya uraisi wake.

Na hivi, ni Watanzania wangapi wanatambua kuwa dira ya maendeleo aliyotumia Raisi Mkapa kutukwamua kiuchumi (TANZANIA DEVELOPMENT VISION 2025) ni matokeo ya kazi ya Prof. Mwandosya baada ya kuambiwa na Raisi Mkapa asimamie utayarishaji wake? Najua wengi hawakujua hili kwa sababu ilipokamilika iliandikwa imeandaliwa chini ya Planning Commission, bila kueleza iliandaliwa chini ya usimamizi wa Prof. Mwandosya

Na tunaomfahamu Prof. Mwandosya, tunajua kwamba katika nyanja za kimataifa, alikuwa kinara wa majadiliano ya mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi ulioitwa Kyoto Protocol, kiasi kwamba alisifiwa sana juu ya uwezo wake wa kuchambua mambo na Raisi Clinton wa Marekani, pamoja na Al Gore. Wakati huo Prof. Mwandosya alikuwa msemaji wa kundi la G77 & China, lakini hakuwa na madaraka yoyote serikalini Tanzania, jambo ambalo lilimfanya Raisi Clinton wa Marekani amshangae sana Mkapa kutomtumia ipasayo Prof. Mwandosya katika serikali yake - na ndipo Prof Mwandosya "alipoamriwa" na Mkapa akagombee ubunge.

Ndio maana imesemwa kwamba katika mambo ambayo hutakaa umdanganye Prof. Mwandosya ni mambo ya mikataba. Hapo kina Prof. Kabudi na degree za sheria zao weka kando kabisa!

Na wakati fulani Prof. Mwandosya akiwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, kulikuwa na mbinu za nchi ya Misri kubadilisha makubaliano ya matumizi ya mto Nile ili kuinufaisha zaidi Misri. Ilibaki kidogo sana nchi za Mto Nile kutia sahihi mkataba huo mpya pale ambapo Prof. Mwandosya aliibuka tena na kuziamsha nchi nyingine juu ya vipengele kwenye makubaliano hayo mapya ambavyo vingezikandamiza. Kwa sababu ya uchambuzi wake huo, nchi zote za Mto Nile ziliwagomea Misri kuweka sahihi makubaliano hayo mapya. Hadi leo Misri hawataki kabisa kusikia habari za Prof. Mwandosya kwa kuwa wanamuona kuwa mtu aliewanyang'anya tonge mdomoni!

Na labda pia wengi waligundua kwamba mara tu baada ya Prof. Mwandosya kuteuliwa kuwa Mweyekiti wa EWURA, bei ya mafuta ilishuka kiasi tofauti na matarajio ya wengi, na wengi wamekuwa wakijiuliza kama ilikuwa ni utendaji wake kama Mwenyekiti wa EWURA uliosababisha kutoa ahueni kwenye bei za mafuta nchini.

Sasa kuna mengi juu ya Prof. Mwandosya naweza kusema hapa, lakini acha haya yatoshe kwa sasa ili kuweka backdrop ya swali langu. Kwa nini Kikwete hakumshauri Samia amteue Prof. Mwandosya kuwa Makamu wa Raisi?

Swali langu pia linaendana na maoni ndani ya humu JF juu ya uteuzi wa Dr. Mpango kama Makamu wa Raisi. Kwa ujumla wengi wa wana JF hawaridhishwi kabisa na Dr. Mpango kuwa Makamu wa Raisi, hasa ukizingatia matukio ya hivi karibuni yaliyomhusu Dr. Mpango.

Sasa je, Kikwete hakukumbuka kwamba angalau Makamu wa Raisi wa Samia awe mmojawapo wa wagombea wa uraisi wa awamu ya Magufuli? Maana kama Prof. Mwandosya angekuwa Raisi badala ya Magufuli, hadi leo hii angekuwa ni raisi katika awamu yake ya mwisho. Je, inawezekana pia Kikwete hakumpendekeza Prof. Mwandosya kuwa Makamu wa Raisi kutokana na ile issue ya "majina ya mfukoni"?

Kwa tunaomfahamu Prof. Mwandosya, ukiachia mbali porojo za humu JF, kama angekuwa ndio Makamu wa Raisi chini ya Raisi Samia, Tanzania tungeenda mbali sana na uongozi wa Raisi Samia ungeonekana ni bora na ungemfanya maarufu kwa scale ile ya Nyerere - mama wa Taifa! Na naweza kudiriki kusema inawezekana kabisa, Kikwete alitambua wazi kama Prof. Mwandosya angekuwa Makamu wa Raisi wa Samia, basi Kikwete angekuwa na influence kidogo sana kwa Samia, au asingekuwa na influence yeyote!

Kwa hiyo naweza kusema kwamba katika hili ni wazi ubinafsi ulizidi maslahi ya nchi. Raisi Samia alipigwa chenga katika kuteua Makamu wa Raisi. Prof. Mwandosya angemfaa sana na tusingekuwa na habari za kulishwa samaki waliooshwa kwenye maji ya maiti!

Samia anapaswa kuelewa kwamba Watanzania tunakesha tukimwombea uzima na afya tele, na sio tu kwa sababu tunampenda kama Raisi wa Tanzania!
Mkuu...
 
Mzee smart kichwani sana,mwendazake alimuchukulia poa sana, nmesoma research paper zake nyingi Prof Mark Mwandosya. Ameandika kwa uweledi wa hali ya juu. MZEE HUYU NI ELECTRICAL ENGINEER lakini kafanya research nying nje ya fani yake. Kama hamjui uwepo wa Wizara ya mazingira ni ushauri wa kifaa hichi...Kibaya kwa Africa ni kuwa ukiwa Smart utafitinika tu..Nafasi zote za juu pale Huyu Mzee angefiti na Nchi ingeenda sawa.
 
Nadhani sasa umefika wakati muafaka wa Samia kumteua Prof. Mwandosya kama waziri Mkuu, kama sio Makamu wa Raisi. Huenda Kikwete atapinga sana kwa sababu zake binafsi na sio maslahi ya taifa, lakini labda ni vema Samia asimsikilize katika hili
Waziri mkuu ni lazima awe mbunge wa Jimbo na sio wa kuteuliwa
 
Kwa hiyo mleta mada, unataka kutuambia mambo haya ya kufikirika.

1. Kikwete alimshauri Samia kuhusu Philip Mpango awe makamu wake wa Rais. Umejuaje?

2. Kikwete hakumshauri Samia kuhusu Professor Mwandosya kuwa makamu wake wa Rais. Umejuaje?

3. Kikwete huwa yuko busy kumshauri Samia kuhusu nani ashike nyazifa nyeti za serikali yake. Umejuaje?

4. Kitu chochote Kikwete anachomshauri Samia, ni lazima Samia afuate. Umejuaje?

Msingi wa hoja yako uko kwenye dhana ya kusadikika (assumption)

Sio siri kuwa yote uliyouliza kuhusu Kikwete na Samia ni Kweli; ndio maana nchi inakwama!! Kikwete believes without him Samia would not have become Presdaa!!!
 
Mkuu, wewe umesema hayo, sio mimi. Mimi nilichofanya ni kuuliza kwa nini Kikwete hakumshauri,kwa sababu najua Samia huwa kuna wakati anapata ushauri wa Kikwete, toka zamani akiwa na Magufuli. Sasa huko ulikoenda wewe ni kwingine kabisa. Kama Kikwete alitoa ushauri huo Samia akakataa basi sema
Kikwete ni mshauri wa raisi? Tangu lini?
 
Mzee smart kichwani sana,mwendazake alimuchukulia poa sana, nmesoma research paper zake nyingi Prof Mark Mwandosya. Ameandika kwa uweledi wa hali ya juu. MZEE HUYU NI ELECTRICAL ENGINEER lakini kafanya research nying nje ya fani yake. Kama hamjui uwepo wa Wizara ya mazingira ni ushauri wa kifaa hichi...Kibaya kwa Africa ni kuwa ukiwa Smart utafitinika tu..Nafasi zote za juu pale Huyu Mzee angefiti na Nchi ingeenda sawa.
Huyo unayemsifia kafanya nini nyumbani kwake kuhusu utafiti huo? Hebu tumbukiza hapa utafiti wake mmojawapo ambao ndio umetumika kuanzisha mradi wowote ukasimama hadi leo halafu uende nyumbani kwake pamoja na huko anakotokea Rungwe Tukuyu utuletee kitu gani alichokifanya huko kwa kutumia elimu yake hiyo unayoipaisha kwenye jukwaa hili. Kila mtu ana umhimu wake eneo fulani kama kakuzidi wewe usifikiri kamzidi na mwingine!!
 
Back
Top Bottom