Kwanini Kikwete hakumshauri Samia amteue Prof. Mwandosya kuwa Makamu wake wa Rais?

-atakuwa na yeye alishauriwa na profesa wa sheria, yeye ndio akaenda kwenye baraza la mawaziri kutoa hoja na sifa akapata yeye,
Hapana, katika kitabu chake aliandika kwamba kulikuwa na tafrija iliyoandaliwa na Misri usiku wa kabla ya asubuhi ya kutia sahihi makubaliano. Mawaziri wengine wakaenda kwenye tafrija yeye akaamua kutoenda na usiku huo kuusoma mkataba kwa makini ndio akagundua mapungufu yake. Kwa hiyo ile tafrija ilipangwa na wa Misri kimkakakati.

Halafu huu mpango wa kutowapa viongozi nafasi ya kusoma mikataba kwa makini ni ujanja unatumiwa na watu wengi sana.

UKienda China, mkiwa mnajadili mkataba wanawaweka kwenye chumba baridi sana, na wanasema hawawezi kupunguza baridi kwa sababu ni mfumo uko automatic. Basi inabidi ukubaliane nao haraka haraka ili utoke kwenye baridi. Pia inasemekana mwili ukiwa na baridi sana uwezo wa kufikiri unapungua kidogo
 
Mkuu...
 
Mzee smart kichwani sana,mwendazake alimuchukulia poa sana, nmesoma research paper zake nyingi Prof Mark Mwandosya. Ameandika kwa uweledi wa hali ya juu. MZEE HUYU NI ELECTRICAL ENGINEER lakini kafanya research nying nje ya fani yake. Kama hamjui uwepo wa Wizara ya mazingira ni ushauri wa kifaa hichi...Kibaya kwa Africa ni kuwa ukiwa Smart utafitinika tu..Nafasi zote za juu pale Huyu Mzee angefiti na Nchi ingeenda sawa.
 
Nadhani sasa umefika wakati muafaka wa Samia kumteua Prof. Mwandosya kama waziri Mkuu, kama sio Makamu wa Raisi. Huenda Kikwete atapinga sana kwa sababu zake binafsi na sio maslahi ya taifa, lakini labda ni vema Samia asimsikilize katika hili
Waziri mkuu ni lazima awe mbunge wa Jimbo na sio wa kuteuliwa
 

Sio siri kuwa yote uliyouliza kuhusu Kikwete na Samia ni Kweli; ndio maana nchi inakwama!! Kikwete believes without him Samia would not have become Presdaa!!!
 
Kikwete ni mshauri wa raisi? Tangu lini?
 
Huyo unayemsifia kafanya nini nyumbani kwake kuhusu utafiti huo? Hebu tumbukiza hapa utafiti wake mmojawapo ambao ndio umetumika kuanzisha mradi wowote ukasimama hadi leo halafu uende nyumbani kwake pamoja na huko anakotokea Rungwe Tukuyu utuletee kitu gani alichokifanya huko kwa kutumia elimu yake hiyo unayoipaisha kwenye jukwaa hili. Kila mtu ana umhimu wake eneo fulani kama kakuzidi wewe usifikiri kamzidi na mwingine!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…