Kwanini kiongozi wetu mkuu hajawahi kukosa USD za kufanya safari za nje ya Nchi ilhali wafanyabiashara wanakosa USD kwenye MABENKI?

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom!!

Kila Kona ya nchi yetu Kwa sasa, dollar imekuwa mtihani, hazipatikani hata Kwa tochi,

Mfanyabiashara mwenye pesa za kitanzania, akienda benki kubadili Tshs Ili apewe USD Kwa ajili ya kuagiza bidhaa nje ya Nchi, anaambiwa dollar hamna. Analazimika kuzitafuta mtaani na kuzipata ni rate kubwa Hadi 3000sh Kwa 1 Usd.

Swali linakuja kuwa,

1. Kiongozi wetu anapofanya safari za nje Huwa anatumia Pesa za kitanzania TSHS akiwa huko Nchi za watu?

2. Na ikiwa Huwa anatumia dollar na walioambatana naye ,wao huwa wanapata wapi hizo USD ambazo wafanyabiashara wakienda benki hawazipati?

3. Tukiwaza Kwa sauti kuwa safari za nje za viongozi wetu ndizo zinakausha hazina ya dollar nchini, tutakuwa tumekosea kuwaza hivyo?

4. Ikiwa hizi Bureau de Change za mtaani wanazo dollar, iweje MABENKI yakose USD, hamnu
si harufu ya kitu kibaya hapo?

USHAURI: Kiongozi wetu mkuu na WA chini yake, wasitishe safari za nje Hadi hapo Nchi itakapokuwa na hazina ya pesa za kigeni za kutosha. Uongozi ni vitendo, ni kuongoza njia, Si maneno matupu.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni🙏
 
Wapi duniani kiongozi mkuu wa nchi amewahi kukosa fedha za kigeni kwa ajili ya shughuli zake?

Hata Cuba,Venezuela, Korea Kaskazini kuna hali ngumu ya kiuchumi na hawana fedha za kigeni lakini huwezi sikia Viongozi wao wakuu wamekosa fedha za kigeni wanaposafiri nje ya Nchi zao
 
Tukisema viongozi wetu ndio wameficha dollar tutakuwa tumekosea?
 
Kwahiyo wao hutengewa pembeni akiba ya dollar tofauti na wananchi wengine?
 
Bro, hata kama tunachangamoto za USD hatujafikia hatua ya kukosa kabisa. Hata hao wafanyabiashara wanapata sema sio kwa mahitaji.

Rais ni mara chache anasafiri na ipo planned. Hivyo ni lazima mabenk yatenge kuisaidia serikali kwa maana ya viongozi wake kukamilisha majukumu.
 
Wewe unaona ni sawa kukosa pesa benki Kisha Kisha uzipate mtaani chache tena Kwa kuzinunua chache chache Kwa rate ya shs Tshs 3000 Kwa 1 Usd?
 
Kwa kifupi hapo inaonyesha
Hutana vipaumbele kwenye matumizi ya uchumi na ya dollar

Hivi inakuwaje Dolla kwa ajili ya wazalishaji au wanaongeza mapato ya serikali zikosekana
Lakini za safari ziwepo

Kuna safari zingine hazina umuhimu wa Rais kwenda atume wawakilishi kupunguza gharama
 
Ni Kweli kabisa,

Balozi atuwakilishe,

Ikiwa wanataka mazungumzo, VIDEO CONFERENCE zitumike,

Safari zimezidi, na hazina TIJA zaidi ya kuturudisha utumwani!!
 
Amen
 
Viongozi wa Africa ni Bata sana ku'mam@kee daah fikiria daily ni mwendo wa Mwewe TU kwa kwenda mbele, hapo jirani Ruto alijetetea Pesa kapewa na Marafiki zake sasa Bibi Zena Mama Abdul hizo dollar anazozipukutisha anazitoa kwenye Mshahara wake au namna gani?
 
Fungu la ofisi ya rais lina kila kitu. Na ana bajeti yake. So si kificho ni utaratibu upo
Sasa ikiwa wafanyabiashara wanakosa dollar kwenye banks,

Kwanini safari za nje zisifutwe Hadi mambo yatakapotengemaa?

Nini maana ya uongozi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…