Thesis
JF-Expert Member
- Aug 30, 2017
- 1,804
- 3,113
umenena mazito sana. Ni kweli kuna mambo ukizungumza unaweza onekana ni kichaa mbele ya jamii. Ya sirini ni makubwa mno mno mno kuliko yaliyo wazi. Hata siri tu za serikali kuna baadhi zikisemwa kuna watu lazima watesema msemaji ni kichaa maana hawaamini kama serikali inaweza fanya hayo.Mkuu,ndiyo maana nasema kwamba kuna mambo ukisema yana madhara.Sizungumzii madhara ya kimwili lakini kwa watu ambao wanakuwa wanakutazama kwa namna fulani hivi wataanza kuhisi labda una matatizo....
Taratibu tutakuwa tunaelezana tu.Siku moja mwaka 2011 nilimueleza bro wangu mmoja kuhusu uwepo wa mambo yanayofichwa na yanayofanywa na aina fulani ya watu wasiofahamika na wengi.Bro wangu huyu aliniangalia kisha akatikisa kichwa kuonesha amenisikia,lakini sikujua kuwa alikuwa ameanza kuhisi nina shida kichwani hadi alipokuja kupata ushahidi wa niliyomwambia halafu akaja kuniambia ukweli wa namna alivyoniona.....
Tangu siku hiyo nimekuwa makini sana kusema sema mambo hovyo maana unaweza kujikuta unaharibu mahusiano yako na watu bila sababu ya msingi maana mtu ataanza kuhisi labda unavuta bangi au una shida fulani za kufanana na hizo na akaanza kukukwepa.....
Ninakuwa mpole na taratibu tutakuwa tunaambizana yale yalayotustahili mkuu....
Baadhi ya wazazi pia wana siri ambazo watoto wao hawajui na pindi ukiwambia watakuona umechanganyikiwa na utageuka kuwa adui yao mkubwa