Kwanini kitabu cha Enoch kinapingwa vikali na Wanathiolojia?

Duh dini zina vitu vingi tusivo vijua
 
Very useful hizi zipo lakini kumbe ni story ya kweli[emoji111] [emoji111]
 
Nilichojifunza katika kitabu cha Enoch ni juu ya origin ya mtu mweupe (kina eleza Mungu aliumba mtu mweusi ila mtu mweupe alitokana na malaika wenye tamaa i.e fallen angels waliokuwa wakiwaingilia kimwili binadamu).?

Mkuu kama ndivyo ulivyoelewa hivi, basi hukukielewa kitabu cha Enoch! Na pengine ni kwa sababu ya lugha!

Enoch alipozaliwa alikuwa ni mtu mwenye muonekano wa tofauti manaa hata ngozi yake ilikuwa inang'aa sana.

Sasa wakati wa enzi hizo, wana wa Mungu (malaika) waliwatamani wanawake wa kibinadamu. Moja wa malaika wao kiongozi alikuwa anaitwa Azazel na wakashuka wakawachumbia wana wa binadamu, wakaingia kwao wakazaa watoto. Hao watoto walikuwa wanaitwa Wanefil.

Hao kina Azazel wakawafundisha wana wa binadamu juu ya mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na kujipamba, kujipodoa na hata kutengeneza vioo vya kujiangalia. Walifanya machukizo mengi sana mbele za Mungu.

Basi hao wanefil wana wa hawa malaika walikuwa ni madubwana na walikuwa wamekuwa mzigo mkubwa mbele za jamii maaana walikula vyakula vyote vikaisha, wanyama, ng'ombe n.k.

Basi binadamu wakamlilia Mungu juu ya hao wanefil maana walikuwa wameilemea nchi. Sasa kwa matokeo hayo Mungu akaagiza kuwa kina Azazel na malika wengine wafungwe kwenye gereza huko kuzimu mpaka siku za mwisho, pia akawatupa hao wanefil huko kuzimu ndio wakawa majini au pepo wabaya unaowasikia sasa hivi.

Enoch ndiye aliyeitwa na Mungu mpaka mbinguni na wakati anaelekea huko mbinguni kuongea na Mungu nadhani alikuwa amefika kwenye mbingu ya tatu ndipo alipokutana na kina Azazel wakawa wanamsihi awaombee msahmaha kwa Mungu kutokana na matendo yao ili waachiliwe...

Basi kufika huko mbinguni, Enoch alipanda mpaka mbingu ya saba kuongea na Mungu juu ya mambo mbali mbali na ndipo Mungu akampa Enoch kazi ya kwenda kuwahukumu hao malaika wakosefu kina Azazel...

Kwa hiyo sio kweli kuwa Wanefil ndio walikuja kuwa watu weusi... Bali ndio walikuja kuwa majini!

Na hao wanefil ni madubwana makubwa kweli kweli. Yani Mnefil mmoja wanaigina kina Le Mutuz Watano hivi!
 
haya maelezo yananikumbusha muvi fulani ivi nimeisahau jina
 
Iweje aving'oe kwenye Biblia halafu aviache kwenye Google wakati anajua huu ni ulimwengu wa utandawazi? Safari bado ipo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…