Kwanini Kituo cha mafuta 'Rupeez Oil' kimejengwa kwenye hifadhi ya barabara Kimara Stop Over?

Kwanini Kituo cha mafuta 'Rupeez Oil' kimejengwa kwenye hifadhi ya barabara Kimara Stop Over?

maroon7

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
11,311
Reaction score
15,640
Ukistaajabu ya Musa,

Katika hali ya kushangaza sana kuna kituo kipya cha mafuta kinajengwa kando ya barabara maeneo ya Stop over Kimara. Hii imekuja baada ya vituo vingine vyote kufungwa kwa sababu ileile ya kuwa vipo ndani ya hifadhi ya barabara, ila cha ajabu hiki kituo kipya kinachoitwa Rupeez Oil ndio kipo jirani zaidi ya barabara.

Je, ni nani alieruhusu huu ujenzi? Mbona mbele kidogo tu ya hicho kituo kuna sheli nyingine ilifungwa na hadi leo haijaruhusiwa? Vituo kama vinne hadi kufika pale Mbezi kwa Yusuf mbona vyote vilifungwa imekuaje hawajaruhusiwa na kwanini hiki kituo kipya kinajengwa tena bila aibu?

Au ndio zama za double standards zinarudi kwa kasi?

kituo-pic.jpg

======

UPDATES: 18 Nov 2022

======

UFAFANUZI KUTOKA MAMLAKA YA UDHIBITI WA HUDUMA ZA NISHATI NA MAJI (EWURA)

Kituo kimejengwa kwenye road reserve kwa makubalino ya kisheria na utaratibu baina ya wamiliki na TANROADS

Hivyo, EWURA inapotoa kibali cha ujenzi wa kituo cha mafuta katika eneo fulani, huwa imejiridhirisha kwamba vigezo vyote vimezingatiwa.
 
Kila nikipita pale nashangaa sana inakuwaje kituo kinajengwa karibu kabisa na barabara ili hali kuna watu walivunjiwa nyumba zao wengine wakafa kwa presha, wengine wakawa masikini kabisa n.k.. Na vituo vingine vya mafuta vimezuiwa ili hali vipo mbali na barabara ukilinganisha na hicho kipya kinachojengwa?

Na kuna kingine kinajengwa karibu kabisa na barabara pale roundabout ya Goba njia nne tena chenyewa kipo kati ya barabara mbili ya kutokea Matosa na ile kubwa ya kwenda Mbezi.
 
Nchi hii hicho kitengo kinachoitwa Mipango miji nafikiri ni sehemu ya kutokea tu.
 
Kwani hujui kama jiwe alikua na visasi vya mbwa? unaweza kuvunjuiwa nyumba mita miatano huko kwa kisingizio cha road reserve wakati wenzio wa mita mbili tu hawako kwenye road reserve
 
Kwani hujui kama jiwe alikua na visasi vya mbwa? unaweza kuvunjuiwa nyumba mita miatano huko kwa kisingizio cha road reserve wakati wenzio wa mita mbili tu hawako kwenye road reserve
Sasa hizi zama si waruhusiwe wote warudishe vituo vyao? Na waliovunjiwa nao warudi basi
 
Back
Top Bottom