Kwanini Kituo cha mafuta 'Rupeez Oil' kimejengwa kwenye hifadhi ya barabara Kimara Stop Over?

Habari za mtaani kwetu hicho kituo ni cha manispaa ya ubungo, wasimamizi wa ujenzi ni Tanroad wenyewe.
 
Yule amepanga eneo la Tanroad kwa muda fulani, anawalipa Tanroad hela, siku wakitaka tumia eneo anapewa notice anaondoka bila kudai chochote
Kama watu walivunjiwa nyumba nayeye anaacha ajenge permanent building haina afya sana, inaweza kuibua hisia kwa raia
 
Ukistaajabu ya Musa,

Katika hali ya kushangaza sana kuna kituo kipya cha mafuta kinajengwa kando ya barabara maeneo ya Stop over Kimara. Hii imekuja baada ya vituo vingine vyote kufungwa kwa sababu ileile ya kuwa vipo ndani ya hifadhi ya barabara, ila cha ajabu hiki kituo kipya kinachoitwa Rupeez Oil ndio kipo jirani zaidi ya barabara.

Je, ni nani alieruhusu huu ujenzi? Mbona mbele kidogo tu ya hicho kituo kuna sheli nyingine ilifungwa na hadi leo haijaruhusiwa? Vituo kama vinne hadi kufika pale Mbezi kwa Yusuf mbona vyote vilifungwa imekuaje hawajaruhusiwa na kwanini hiki kituo kipya kinajengwa tena bila aibu?

Au ndio zama za double standards zinarudi kwa kasi?
atakuwa ester express mbeba mfuko wa taifa
 
Kwani hujui kama jiwe alikua na visasi vya mbwa? unaweza kuvunjuiwa nyumba mita miatano huko kwa kisingizio cha road reserve wakati wenzio wa mita mbili tu hawako kwenye road reserve
ndo maana ccm wanahamasisha kila siku chadema kujenga ofisi,yaan walivyo n roho mbaya hata wakijenga kule buza wangetafuta tu sababu wakalivunje
 
Ukistaajabu ya Musa,

Katika hali ya kushangaza sana kuna kituo kipya cha mafuta kinajengwa kando ya barabara maeneo ya Stop over Kimara. Hii imekuja baada ya vituo vingine vyote kufungwa kwa sababu ileile ya kuwa vipo ndani ya hifadhi ya barabara, ila cha ajabu hiki kituo kipya kinachoitwa Rupeez Oil ndio kipo jirani zaidi ya barabara.

Je, ni nani alieruhusu huu ujenzi? Mbona mbele kidogo tu ya hicho kituo kuna sheli nyingine ilifungwa na hadi leo haijaruhusiwa? Vituo kama vinne hadi kufika pale Mbezi kwa Yusuf mbona vyote vilifungwa imekuaje hawajaruhusiwa na kwanini hiki kituo kipya kinajengwa tena bila aibu?

Au ndio zama za double standards zinarudi kwa kasi?
Serikali ilichukua sampo ya vipimo vya mita toka barabarani na vimepelekwa kwa mkemia mkuu kwa uchunguzi, majibu yakirudi kitaruhusiwa kuendelea na ujenzi wa taifa kupitia usafirishaji, asante ndugu mzalendo kwa kuliona hilo na kutoa taarifa na ukiviona vingine tujulishe.
 
Yule amepanga eneo la Tanroad kwa muda fulani, anawalipa Tanroad hela, siku wakitaka tumia eneo anapewa notice anaondoka bila kudai chochote
Mbona yule wa pale kimara suka wamempiga pin hadi leo?
 
Sidhani kama kutakuwa na comment nyingine ya kipumbavu na kijinga zaidi ya hii ya kwako katika uzi mzima.
Crap.
Acha watu wafanye Kazi Ni Upumbavu unajua Ni mafundi wangapi na Mama ntilie wangapi wanapata Maisha happy?
 
Yule amepanga eneo la Tanroad kwa muda fulani, anawalipa Tanroad hela, siku wakitaka tumia eneo anapewa notice anaondoka bila kudai chochote
Hata hzi sheli za adimiral zinajengwa barabaran sana
 
Ile barabara Unyama uliofanyika we acha tu..yaani barabara imecover 20m..bomoa bomoa ilienda 122m kila upande. Ule ukatili sio wa sayari hii.Sasa leo wenyewe wameanza kula matapishi yao. Kwa haraka haraka hicho kituo, ni cha kupima upepo tu..vingi vitajengwa na wenye mapembe toka kimara mpaka kiluvya. Kwani ninani atawakataza? Zama zilee zilipita...!!
 
Acha watu wafanye Kazi Ni Upumbavu unajua Ni mafundi wangapi na Mama ntilie wangapi wanapata Maisha happy?
unafahamu kwamba hapo kituo kinapojengwa kulikuwa nana nyumba ya mtu ilibomolewa kwamba ipo barabarani? Tena bila kulipwa fidia
 
Tuache kulalamika acheni na sisi mafundi ujenzi tulambe Asali
 
Back
Top Bottom