Kwanini Kituo cha mafuta 'Rupeez Oil' kimejengwa kwenye hifadhi ya barabara Kimara Stop Over?

Kwanini Kituo cha mafuta 'Rupeez Oil' kimejengwa kwenye hifadhi ya barabara Kimara Stop Over?

Ukistaajabu ya Musa,

Katika hali ya kushangaza sana kuna kituo kipya cha mafuta kinajengwa kando ya barabara maeneo ya Stop over Kimara. Hii imekuja baada ya vituo vingine vyote kufungwa kwa sababu ileile ya kuwa vipo ndani ya hifadhi ya barabara, ila cha ajabu hiki kituo kipya kinachoitwa Rupeez Oil ndio kipo jirani zaidi ya barabara.

Je, ni nani alieruhusu huu ujenzi? Mbona mbele kidogo tu ya hicho kituo kuna sheli nyingine ilifungwa na hadi leo haijaruhusiwa? Vituo kama vinne hadi kufika pale Mbezi kwa Yusuf mbona vyote vilifungwa imekuaje hawajaruhusiwa na kwanini hiki kituo kipya kinajengwa tena bila aibu?

Au ndio zama za double standards zinarudi kwa kasi?
giphy.gif
 
Ile barabara Unyama uliofanyika we acha tu..yaani barabara imecover 20m..bomoa bomoa ilienda 122m kila upande. Ule ukatili sio wa sayari hii.Sasa leo wenyewe wameanza kula matapishi yao. Kwa haraka haraka hicho kituo, ni cha kupima upepo tu..vingi vitajengwa na wenye mapembe toka kimara mpaka kiluvya. Kwani ninani atawakataza? Zama zilee zilipita...!!
Wapige na highway mall kabisa maana kwa tunakoelekea hata mi naweza kwenda kukodi reserve ya road nikajenga highway pub
 
Hii ishu ya Tanroad kuweza kuwapangisha wengine na wengine kuwapa masharti magumu kwenye hii biashara ya ushindani pana kitu hakipo sawa hapo ila wacha tuendelee na utaratibu wao...
 
Ukistaajabu ya Musa,

Katika hali ya kushangaza sana kuna kituo kipya cha mafuta kinajengwa kando ya barabara maeneo ya Stop over Kimara. Hii imekuja baada ya vituo vingine vyote kufungwa kwa sababu ileile ya kuwa vipo ndani ya hifadhi ya barabara, ila cha ajabu hiki kituo kipya kinachoitwa Rupeez Oil ndio kipo jirani zaidi ya barabara.

Je, ni nani alieruhusu huu ujenzi? Mbona mbele kidogo tu ya hicho kituo kuna sheli nyingine ilifungwa na hadi leo haijaruhusiwa? Vituo kama vinne hadi kufika pale Mbezi kwa Yusuf mbona vyote vilifungwa imekuaje hawajaruhusiwa na kwanini hiki kituo kipya kinajengwa tena bila aibu?

Au ndio zama za double standards zinarudi kwa kasi?

======

UPDATES: 18 Nov 2022

======

UFAFANUZI KUTOKA MAMLAKA YA UDHIBITI WA HUDUMA ZA NISHATI NA MAJI (EWURA)

Kituo kimejengwa kwenye road reserve kwa makubalino ya kisheria na utaratibu baina ya wamiliki na TANROADS

Hivyo,EWURA inapotoa kibali cha ujenzi wa kituo cha mafuta katika eneo fulani,huwa imejiridhirisha kwamba vigezo vyote vimezingatiwa.
Januari makamba hicho chawa wa mama
 
Pale pale kinapojengwa kile kituo palikua na nyumba ya mtu, ILIBOMOLEWA na serikali hii hii sikifu ya CCM. Leo hii serikali hii hii inampa mtu wake wa ndani kabisa leseni pale pale afanye biashara.
Malipo Ni hapa hapa.
 
Kinachosikitisha pale kulikuwa na nyumba moja kati ya zile zilizobomolewa islsikuwa ni ya Mzee mmoja hivi . Yule mzee mwenye nyumba alikuwa mzee wa umri mkubwa. Magu alizibomoa akapalalaizi then akafa. Nilikuwa napita na kukaa sana yale maeneo.
 
Back
Top Bottom