Ukistaajabu ya Musa,
Katika hali ya kushangaza sana kuna kituo kipya cha mafuta kinajengwa kando ya barabara maeneo ya stop over Kimara. Hii imekuja baada ya vituo vingine vyote kufungwa kwa sababu ileile ya kuwa vipo ndani ya hifadhi ya barabara, ila cha ajabu hiki kituo kipya kinachoitwa Rupeez Oil ndio kipo jirani zaidi ya barabara.
Je, ni nani alieruhusu huu ujenzi? Mbona mbele kidogo tu ya hicho kituo kuna sheli nyingine ilifungwa na hadi leo haijaruhusiwa? Vituo kama vinne hadi kufika pale Mbezi kwa Yusuf mbona vyote vilifungwa imekuaje hawajaruhusiwa na kwanini hiki kituo kipya kinajengwa tena bila aibu?
Au ndio zama za double standards zinarudi kwa kasi?