Kwanini kujenga nyumba imekuwa ni fashion kwa Watanzania?

general assets ina sifa mbili.
1. gharama yake lazima ijulikane
2.utarajie economic benefit kutoka katika hiyo asset
kuna Standard nyingi sana zinaelezea aina za hiyo Assets ila nitaeleza mbili (property, plant and equipment IAS 16 na Inevestment property IAS 40).
PPE IAS 16- inasema Asset inamilikiwa kwa ajili ya uzalishaji mali(bidhaa au Huduma) mfano unajenga ofisi au kiwanda n.k
Investment Property IAS 40- inasema unamiliki Assets kwa dhumuni la kupangisha upate rent au kuuza kwa baadae.
tuitest nyumba ya kuishi kama inafit katika maana ya Asset.
1. Gharama yake inajulikana-JIbu ni ndio
2. mmiliki anatarajia kupata ecenomic benefit- (anaweza kuuza, kupangisha ikafiti katika IAS 40 na IAS 16) kwa hiyo mda wowote anaweza kupata hiyo economic benefit ssa jibu letu litakuwa ni ndio.
katika uendeshaji wa Assets kuna matumizi ya aina mbili
1. matumizi ya kawaida- maintainance cost eg repair na haya matumizi ya kawaida treatment yake ni gharama (normal expenses) unadebit katika PRofit and loss account Auyapeleki katika Upande wa liability
2. matumizi ya kuongeza Thamani Asset-haya mara nyingi ni kuongeza effecieny au capacity ya assets mfano kuweka tiles, kuongeza chumba n.k na haya una debit katika Asset account.
HITIMISHO.
1.nyumba sio liability bali nyumba ni assets bila kuangalia mmiliki anatumia pesa zake kuihudumia (hayo matumizi yataingia katika matumizi ya kawaida au captalized expenses)
2. kama unanafasi jenga Biashara zetu zinaendeshwa na matakwa ya wanasiasa kumbuka mwaka 2015-2021 wafanyabishara wadogowadogo walifurahia dunia ila sasa hivi kiko wapi? (mwanasiasa anaweza kusema lolote na likakukuta la kukuta).
 
Safi kabisa Mhasibu
 
Nyumba ni asset pia na wengi wana ndoto za kuishi kwenye nyumba zao kuepuka usumbufu wa kodi masharti ya wenye nyumba zao
Hamna kitu mnajidanganya tu. Kupenda kujenga jenga ni uoga wa maisha na uharibifu wa mazingira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…