desayi
JF-Expert Member
- Aug 27, 2017
- 3,593
- 5,848
Wahindi wenyewe siku hizi wanajenga labda Hawa wa kuja ila wazaliwa wa huku wanajengaChangamoto yako(siyo tatizo)una mawazo ya Kihindi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wahindi wenyewe siku hizi wanajenga labda Hawa wa kuja ila wazaliwa wa huku wanajengaChangamoto yako(siyo tatizo)una mawazo ya Kihindi.
Tupe mchele kakapumba.
general assets ina sifa mbili.NYUMBA YA KUISHI SIO ASSET
ASSET~ni kitu chochote kinacho kuingizia pesa mfukoni uwepo au usiwepo.
LIABILITY~ni kitu kinachotoa pesa mfukoni kwako.
Ukitaka kuwa tajiri hiki ndio kitu pekee unacho hitaji kukijua na kukifanyia kazi.
Matajiri wote wananunua Assets lakini Masikini na wenye wenye maisha ya saizi ya kati wananunua Liabilities wanazodhani kuwa ni Assets.
Watu wengi ukiwauliza una Asset gan unayomiliki atakutajia vitu kama nyumba, gari, simu, laptop, duka.
Ni sawa kama tu hivyo vitu vinakuingizia pesa, lakini kama havikuingizii chochote hivyo sio Assets bali ni Liabilities.
Hebu tuangalie nyumba
Kama una nyumba yako ya kuishi mwenyewe hiyo ni Liability kubwa sana maana haikuingizii hata mia badala yake inakutolea pesa utalipa umeme, maji, ukarabati na malekebisho ya vitasa, taa, furniture n.k. Hayo yoote yanatoa pesa mfukoni.
Lakini kama nyumba umepangisha hiyo ni Asset. Gari kama unaitumia kwa matumizi yako binafsi ya kila siku hiyo ni Liability kubwa itahitaji mafuta, service na kama umenunua kwa mkopo wa Bank ndio balaa zaidi, ila kama ni la biashara hiyo ni Asset.
Simu ambayo haikuingizii pesa yoyote zaidi ya kukumalizia vocha na kuishia kuchat hiyo ni Liability, Tv na radio hata duka pia, maana siku umelifunga huingizi chochote, matumizi yoote unategemea dukani, badala ya duka kukupa faida, unachukua mshahara unaongeza mtaji.
Wasomi wengi walioajiriwa wanakufa masikini kwasababu mishahara yao na mikopo wanayochukua inaishia kununua liabilities kama furniture, TV, radio, simu kubwa, gari, fridge, nguo, viatu, badala ya Asset ambazo zingewaingizia pesa zingine, mwisho wanaishia kuuza liabilities zao na kubaki masikini kabisa.
Watu wengi wanadhani wakiongezewa mshahara wata tatua matatizo yao, badala yake matatizo yanaongezeka maana mshahara (Income) ukiongezeka, matumizi (Expenses) pia yanaongezeka hivyo kuongeza column ya Liabilities. Na hii yote ni kwasababu hatufundishwi elimu ya pesa darasani.
Matajiri woote wana kuza upande wa kipato (Income) na kupunguza upande wa matumizi (Expenses) kwa kununua Assets nyingi na kupunguza Liabilities, wananunua Luxuries kama gari, tv ,simu kubwa pale tu Assets au vitu walivyowekeza vinapowapatia faida, hivyo faida ndio inanunua magari, nyumba, TV n.k,
Ndio maana wanasema siri ya utajiri ni ubahili, lakini watu wengine kadri kipato kinapoongezeka na matumizi yanaongezeka. Kama unataka kua tajiri lazima ujue pia maana halisi ya neno utajiri(Wealth).
WEALTH~ Is a person's ability to survive so many numbers of days toward, or if you stopped working today, how long could you survive?
Maana yake kama leo utaacha kufanya kazi ambazo zinakuingizia kipato una uwezo wa kuendelea kuishi kwa muda gani?
Ukiona ukiacha kufanya kazi huna uwezo wa kumudu mahitaji ya kila siku kwa muda hata wa mwaka mmoja ujue wewe bado huna Mali(wealth) maana huna Assets zinazoweza kukuingizia kipato cha kuweza kukufanya uendelee kuishi pindi uachapo kazi.
Safi kabisa Mhasibugeneral assets ina sifa mbili.
1. gharama yake lazima ijulikane
2.utarajie economic benefit kutoka katika hiyo asset
kuna Standard nyingi sana zinaelezea aina za hiyo Assets ila nitaeleza mbili (property, plant and equipment IAS 16 na Inevestment property IAS 40).
PPE IAS 16- inasema Asset inamilikiwa kwa ajili ya uzalishaji mali(bidhaa au Huduma) mfano unajenga ofisi au kiwanda n.k
Investment Property IAS 40- inasema unamiliki Assets kwa dhumuni la kupangisha upate rent au kuuza kwa baadae.
tuitest nyumba ya kuishi kama inafit katika maana ya Asset.
1. Gharama yake inajulikana-JIbu ni ndio
2. mmiliki anatarajia kupata ecenomic benefit- (anaweza kuuza, kupangisha ikafiti katika IAS 40 na IAS 16) kwa hiyo mda wowote anaweza kupata hiyo economic benefit ssa jibu letu litakuwa ni ndio.
katika uendeshaji wa Assets kuna matumizi ya aina mbili
1. matumizi ya kawaida- maintainance cost eg repair na haya matumizi ya kawaida treatment yake ni gharama (normal expenses) unadebit katika PRofit and loss account Auyapeleki katika Upande wa liability
2. matumizi ya kuongeza Thamani Asset-haya mara nyingi ni kuongeza effecieny au capacity ya assets mfano kuweka tiles, kuongeza chumba n.k na haya una debit katika Asset account.
HITIMISHO.
1.nyumba sio liability bali nyumba ni assets bila kuangalia mmiliki anatumia pesa zake kuihudumia (hayo matumizi yataingia katika matumizi ya kawaida au captalized expenses)
2. kama unanafasi jenga Biashara zetu zinaendeshwa na matakwa ya wanasiasa kumbuka mwaka 2015-2021 wafanyabishara wadogowadogo walifurahia dunia ila sasa hivi kiko wapi? (mwanasiasa anaweza kusema lolote na likakukuta la kukuta).
Hamna kitu mnajidanganya tu. Kupenda kujenga jenga ni uoga wa maisha na uharibifu wa mazingira.Nyumba ni asset pia na wengi wana ndoto za kuishi kwenye nyumba zao kuepuka usumbufu wa kodi masharti ya wenye nyumba zao
Nakaa kwenye nyumba ya babu yangu hata baba yangu hajajenga
Kuishi kwetu kunakukera?Kumbe tunaongea na mtu anaekaa kwa babu yake[emoji1787]
Dogo siku hizi umekuwa mkorofi. Whats going on?Watakuja kuishi kwako
Hamna kitu bro. Basi tu kuna time watu wanazingua.Dogo siku hizi umekuwa mkorofi. Whats going on?