Kwanini kusiwe na mshindani wa NHIF? Kiukweli wanachofanya ni dhuluma

NHIF ni wezi na matakataka hilo lipo wazi. Hawana wanalofanya zaidi ya kukaa na kunenepeana kwenye yale maofisi yao. Tena bora wewe umetumiwa msg wengine wamekatwa juu kwa juu.
 
Hudhulumiwi, isipokuwa hiyo fedha inamsaidia mnufaika mwingine wa NHIF ambaye pengine amelazwa muda mrefu au anaumwa ugonjwa sugu wenye gharama kubwa sana ya matibabu kuliko kiasi chake anachochangia kwa mwezi/mwaka.
Unachangia ili wewe na familia yako mpate huduma, hilo ndilo lengo la kwanza na la msingi, siyo kutibia majirani.

Wanapaswa kuiingilia upya, wazazi wawili, wanachangia, watoto waendelee kunufaika!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Hiyo ni sheria, lakini kwa mtoto akiwa shule huwa ni 21yrs. Wa kulaumiwa ni sisi wananchi tunao chagua wabunge wa CCM kwenda bungeni kupiga makofi ya ndiooo na kupitisha Sheria za kijinga za lengo la kuwakamua wananchi. Serikali ya CCM haijali afya ya wananchi, tena wakizeeka ndio janga. Bima kwa wazee ni kubwa sana, japo Wana magonjwa mengi lakini nguvu zao ndio zimelifisha taifa hapa hata kama alikuwa muuza madafu au mkulima wa mihogo.
 
Mhhh hayo mahaba sasa, kumsaidia ndiyo iwepesa yote hiyo? Hiyo mifuko Hata ingefanya sh elfu kumi Kwa mwaka ingetosha kabisa, Kwani wanaumwa ni wachache kuliko wazima
Na CCM hela itapata wapi? Umewahi kusikia mchango wa nhif, ewura, rea, tanesco nk kwenye budget ya mwaka?
 
Sawa, lakini si masharti kama ya nhif Tanzania. Kifupi wanakusanya hela bila kutoa huduma. Wanapanga ni magonjwa yapi mtu augue, mengine hapana. Mkata bima mwanamke anapangiwa muda wa kuzaa tangu akate bima, alimfuata maelekezo ya Magufuli ya kufyatua watoto inakula kwake.
 
Kusema kwamba wanakusanya pesa bila kutoa huduma sio sawa kwa sababu huduma zinatolewa na watoa huduma (Dispensaries, Health Centers, Polyclinics na Hospitals) jukumu la NHIF ni kugharamia huduma,ni vizuri pia ieleweke kuwa jukumu la kuandaa sera na miongozo ya matibabu ni la wizara ya afya, inawezekana kabisa wanufaika wa mfuko hawaridhishwi na huduma wanazopata , hilo linazungumzika na ni jukumu la wabunge
 
Na bahati mbaya, hatuna wabunge! Wangekuwepo sheria kandamizi kama hii ya nhif isingepitishwa. Dispensary, vituo vya afya na hospitali ni mawakala wa nhif, hawana lawama katika mapungufu ya nhif. Mtunga sera ni serikali kupitia wizara ya afya. Ndio inatakiwa
kubeba lawama zote.
 
Hudhulumiwi, isipokuwa hiyo fedha inamsaidia mnufaika mwingine wa NHIF ambaye pengine amelazwa muda mrefu au anaumwa ugonjwa sugu wenye gharama kubwa sana ya matibabu kuliko kiasi chake anachochangia kwa mwezi/mwaka.
No hiyo sio sasa. Lazima mie mchangia michango yangu inufaishe kwanza watoto wangu kabla ya huyo mgonjwa mwingine unaye muongelea. Haiwezekani nichangie lakimoja na elfu ishirini kila mwezi halafu mtoto wangu akiugua bado nikalipie matibabu yake hospital hiyo sio sawa
 
Na isitoshe watanzania wengi huwa hawaendi hospitali mpaka wazidiwe kabisa
Nikweli mkuu pamoja na kuchangia hiyo amount kila mwezi bado nikiumwa nazama duka la dawa kukamata on the counter drugs
 
Pole Sana
NHIF Kwasasa Inatupa Tabu Sana Watumiaji
Ingawa Wanajisifu Mno, Huyo Huyo Mtoto Bado Hana Kazi Wao Wameona Nongwa
 
Nikweli kabisa mkuu. Pale pana nafasi tano za Dependants. Mie nilijaza mbili tu za wanufaika .na mmoja ndo huyo wanataka kumtoa . ati michango yangu ya almost milioni moja na lakitatu kwa mwaka hata watoto wangu wasifaidi hii sio sawa
 
Nafikiri hiyo haijakaa vizuri. Nikwamba kwenye zile nafasi tano mie nimejaza mbili tu. Zote watoto wangu. Ndio hao wanataka kumtoa mmoja eti anatmiza miaka 18 December. Which means hata watoto duration ya kufaidi ni limited
 
Pole sana Kiongozi
Sijasoma michango wa wengine kuona kama umesha shauriwa, Kama bado;
Naomba nikupe muongozo kwani mimi ni moja ya watu walio fuatilia masuala ya Bima ya Afya
Bima ya Taifa NHIF humtambua mtoto kama anaweza kujitegemea pale anapo timiza mika 18 kama hayupo shuleni/chuoni
Kwa watoto wanaosoma Sekondari au Chuo, Bima huendelea hadi watakapo maliza masomo yao, haijalishi miaka.
Cha kufanya; wapelekee uthibitisho unao onesha kuwa mtoto wako yupo shuleni/Chuoni
inaweza kuwa ile formu ya kujiunga shule/chuo au Barua kutoka shuleni/chuoni yenye picha yake inayo onesha anasoma (Mwezi wa kuanza na mwezi tarajiwa wa kumaliza.
Natumaini umesaidika
 
Hudhulumiwi, isipokuwa hiyo fedha inamsaidia mnufaika mwingine wa NHIF ambaye pengine amelazwa muda mrefu au anaumwa ugonjwa sugu wenye gharama kubwa sana ya matibabu kuliko kiasi chake anachochangia kwa mwezi/mwaka.
Ni case ngapi za jibyo. Hawa jamaa inabidi wa-review makadrio yao

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
 
Nashukuru sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…