Kwanini kusiwe na mshindani wa NHIF? Kiukweli wanachofanya ni dhuluma

Kwanini kusiwe na mshindani wa NHIF? Kiukweli wanachofanya ni dhuluma

Bima ya Afya ya NHIF ni Majanga na Mateso makubwa. Sasa wewe bora uko na monthly contributions. Vile Vifurushi binafsi ndiyo majanga makubwa. Aliyevipitisha ninafikiri si Mtanzania maana kwa hali zetu asingepanga hivyo. Nina waziwazi wafanye maamuzi huko NHIF watakuwa ni either Warundi au Wanyarwanda. Bima hii kwa huduma mbovu nimeamua kwa moyo mmoja nikiwa mwana CCM lakini nitampigia kura Tindu Lissu maana kipaumbele chake ni kuondoa kero za Bima ya afya.
Sikulaumu kwa uelewa wa kujua hali halisi ya namna Mfuko unavyoelemewa na madai ya mahospitali yanayolipwa na NHIF pindi wewe na wachangiaji wengine mnapoenda kutibiwa...

Ninayeweza kumlaumu ni mtunga mitaala ya elimu zetu kutoweka topic za masuala ya bima ili kila aliyehitimu angekuwa na uelewa na mwammko wa kujiunga na mfuko ili kiasi cha kuchangia kishuke.

Kwa sasa kinachochangiwa na wanachama ni kidogo ukilinganisha kinachotumiwa na waliougua.

Watanzania wengi wanakumbuka bima wakiumwa, hawakumbuki wakiwa wazima...hili ndo tatizo kubwa kiongozi...tusaidiane kutoa elimu
 
Nimetumiwa meseji na Mfuko wa bima ya afya ya taifa NHIF inasema nanukuu " kadi ya mtoto wako .....itakoma kutumika tarehe .... Mwezi wa kumi namoja baada ya kutimiza umri wa miaka 18. Fika ofis ya NHIF au piga 0800110063" mwisho wa kunukuu.

Ninachangia laki moja na elfu ishirini kila mwezi toka kwenye mshahara wangu kwenye mfuko wa NHIF. Nina watoto wa wili wa kike , mmoja 18 years kasoro, wapili 15 years. Hawa ndo Dependants wanufaika wa mfuko ukiniacha mie. Mke wangu ni mchangiaji pia hivyo naye anatumia bima kutokana na michango yake.

Kwa umri wangu ntaendelea kuchangia for 15 years more nikiwa mwajiriwa.

Sasa hapa wizi ninaouona nikwamba pamoja na kuchangia Sh. Laki moja kila mwezi watoto wangu ati wanaondolewa kama beneficiaries eti ametimiza 18 years. Huyo mtoto bado ni Dependants maana yupo shule bado. Siomwajiriwa au anayejitegemea.

Pili value ya mfuko wa bima ya afya inaonekana pale unaposaidia kutibu close Dependants kama watoto ,baba na mama. Sasa kamna waondoa watoto then value ya hicho ninacho changia haipo ndipo ninapohisi kudhurumiwa.

Nauliza wadau. Hivi hakuna mfuko mbadala zaidi ya NHIF? Na kama ipo, je sheria inaruhusu kujitoa kwenye huu mfuko nyonyaji wa NHIF.
Unakunja parefu mkuu kama laki ndio makato yako ya bima
 
Sikuombei but siku ikifika zamu yako kuumwa ugonjwa mkubwa ambao gharama zake ni mara kumi au zaidi ya ulichochangia wewe na mwenza wako ndipo utabaini kumbe bima sio wizi

Mungu atuepushie mbali.
Ni hivi hilo wenyewe walieleza sababu ni kuwa baadhi ya wanachama kukosa kuwa Wakweli ktk kutoa taarifa zao.
Lakini kwetu wanachama haina mashiko kabisa!
Wanachotakiwa waimarishe mifumo yao iwawezeshe kupata taarifa sahihi na siyo kuwakata wanachama dabodabo huku na kule.
 
Back
Top Bottom