Nimetumiwa meseji na Mfuko wa bima ya afya ya taifa NHIF inasema nanukuu " kadi ya mtoto wako .....itakoma kutumika tarehe .... Mwezi wa kumi namoja baada ya kutimiza umri wa miaka 18. Fika ofis ya NHIF au piga 0800110063" mwisho wa kunukuu.
Ninachangia laki moja na elfu ishirini kila mwezi toka kwenye mshahara wangu kwenye mfuko wa NHIF. Nina watoto wa wili wa kike , mmoja 18 years kasoro, wapili 15 years. Hawa ndo Dependants wanufaika wa mfuko ukiniacha mie. Mke wangu ni mchangiaji pia hivyo naye anatumia bima kutokana na michango yake.
Kwa umri wangu ntaendelea kuchangia for 15 years more nikiwa mwajiriwa.
Sasa hapa wizi ninaouona nikwamba pamoja na kuchangia Sh. Laki moja kila mwezi watoto wangu ati wanaondolewa kama beneficiaries eti ametimiza 18 years. Huyo mtoto bado ni Dependants maana yupo shule bado. Siomwajiriwa au anayejitegemea.
Pili value ya mfuko wa bima ya afya inaonekana pale unaposaidia kutibu close Dependants kama watoto ,baba na mama. Sasa kamna waondoa watoto then value ya hicho ninacho changia haipo ndipo ninapohisi kudhurumiwa.
Nauliza wadau. Hivi hakuna mfuko mbadala zaidi ya NHIF? Na kama ipo, je sheria inaruhusu kujitoa kwenye huu mfuko nyonyaji wa NHIF.
Mkuu pole sana sana. Kwa kweli NHIF ni wababaishaji sana ili jambo lako ni kubwa ila langu mimi naamini ni kubwa kuliko.
Nimeanza kazi kampuni fulani hivi, mpaka sasa nina miezi kama 9, makato ya bima kila mwezi ni Tsh.83,000 ya mshahara wangu na mwajiri na yeye anachangia 83,000 jumla yake kwa mwezi na changia 166,000 kama makato ya NHIF, cha kushangza zaidi mpaka sasa sijapata kadi kwa muda wote wa miezi hiyo 9,natunaambiwa NHIF yeye anaanza kukata pale muajiri anapojiunga na kampuni bila kujali unatumia huduma yao au kinyume chake.
Tunajaribu kufuatilia lakini majamaa hawana mpango kabisa,huu mfuko wa NHIF ni kati ya mifuko hovyo kabisa kwenye hii dunia, mifuko haijali wanachama wake hata kidogo,huduma zao ni mbovu sana sana.
Sheria zao kwanza ni zakibabe sana. Huduma kwa wateja nao ni hovyo kuliko kitu chochote kile duniani, wakipigiwa simu hawapokei, ukienda ofisini kwao hawana cha maana wanachosema, mbaya zaidi ukienda unakutana na bonge la foleni.
Halafu leo wanampango wakufanya mfuko lazima kwa watu wote, kama kwasasa mfuko wa bima haijachukua hata asilimia 5 ya watanzania lakini wanashindwa kutoa huduma ya maana kwa wateja wao,je wakifanya kwa wote wote itakuwaje???
Kati ya Taasisi ambazo Mh.Rais TAL akiambishwa tu inabidi avunjevunje harala iwezekanavyo basi hii taasisi,hii taasisi utendaji wake ni kinyaa hata kuendelea kuandika kuhusu wao.
Kwa kweli tusifanye makosa tena oct 28, hii ccm wamekuwa wanababaisha mpaka kwenye jambo la msingi la afya zetu.