Kwanini kusiwe na mshindani wa NHIF? Kiukweli wanachofanya ni dhuluma

Sikulaumu kwa uelewa wa kujua hali halisi ya namna Mfuko unavyoelemewa na madai ya mahospitali yanayolipwa na NHIF pindi wewe na wachangiaji wengine mnapoenda kutibiwa...

Ninayeweza kumlaumu ni mtunga mitaala ya elimu zetu kutoweka topic za masuala ya bima ili kila aliyehitimu angekuwa na uelewa na mwammko wa kujiunga na mfuko ili kiasi cha kuchangia kishuke.

Kwa sasa kinachochangiwa na wanachama ni kidogo ukilinganisha kinachotumiwa na waliougua.

Watanzania wengi wanakumbuka bima wakiumwa, hawakumbuki wakiwa wazima...hili ndo tatizo kubwa kiongozi...tusaidiane kutoa elimu
 
Unakunja parefu mkuu kama laki ndio makato yako ya bima
 
Sikuombei but siku ikifika zamu yako kuumwa ugonjwa mkubwa ambao gharama zake ni mara kumi au zaidi ya ulichochangia wewe na mwenza wako ndipo utabaini kumbe bima sio wizi

Mungu atuepushie mbali.
Ni hivi hilo wenyewe walieleza sababu ni kuwa baadhi ya wanachama kukosa kuwa Wakweli ktk kutoa taarifa zao.
Lakini kwetu wanachama haina mashiko kabisa!
Wanachotakiwa waimarishe mifumo yao iwawezeshe kupata taarifa sahihi na siyo kuwakata wanachama dabodabo huku na kule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…