realMamy
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 3,925
- 8,853
Nimekuwa nikisoma na kufuatilia baadhi ya visa vya kweli katika vitabu na mitandao ya kijamii vinavyohusu mahusiano na ndoa kuvunjika na moja ya sababu zinazosababisha kutokea hayo ni Mahali pa kazi.
Wake kwa waume wamekuwa wakilalamika kuachwa na mtu wake kwa sababu ya mfanyakazi mwenzie.
Kitu kingine ni ajira za mbali.
Mfano Baba yuko mkoa mwingine na mama yuko mkoa mwingine wakifanya kazi basi utaambiwa Baba alianza kuishi na mfanyakazi mwenzie wa kike na ndoa ikaanza kuyumba.
Lakini pia Boss kuamua kuchukua mke wa mtu kwa kutumia cheo chake au mmoja tamaa za pesa zimemponza.
Vilevile nimegundua kuwa sehemu za kazi watu wanakaa muda mrefu kuliko sehemu nyingine. Na kama mahusiano yameyumba hii inaweza kuwa ni sababu mojawapo.
Sababu nyingine ni zipi?