Kwani mfumo ndio nini, na mfano wa mfumo ni upi ambao ni tofauti na uliopo, kwamba Rais anakuwa na wasaidizi toka juu kabisa Hadi ngazi ya kitongoji??
Kuna kipi kinachokosekana hapo, kuna Bunge, Mahakama na Ile Taasisi ya Uraisi, ni mfumo gani huo mwengine
Maana kila mtu, anaongelea Mfumo, mfumoo, bila kuongoza mjadala wa Hilo Neno mfumo,
Mfumo ndio kitu gani Hilo na linafanaje??
Shida siyo mfumo, shida ni wananchi wenyewe,
Kwanza ni wachezea mfumo, lakini pili, Wapo tayari kutetea waharifu wa mfumo,
Nchi yangu hii, iko tofauti Sana pengine na watu wote wa Dunia hii, ni nchi pekee ambayo, watu wake wanaweza kushirikiana na wahamiaji haramu kuwaficha majumbani mwao na kuwasafitisha Kutokea makwao Kwa kutumia magari Yao, ni nchi pekee ambayo watu wake hawajali pindi Mali na utajiri wa nchi Yao unaposombwa na kina Manji, ni nchi pekee inayo walilia wauza dawa za kulevya wake kuwekeza nchini Kwa madai eti walionewa
Ni nchi pekee ambapo watu wake hukaa kimya mafuta ya serikali yanapoibiwa waziwazi huku wananchi wake hawatoi tarifa hata kama nyumba inayofanya uharifu huo imepakana na Watanzania
Ni nchi pekee ambapo mapolisi wanaweza kusindikiza mwizi wa Tanzanite Kwa ulinzi na vingora kumvusha mipakani na bado asikari huyo akapandishwa cheyo
Nchi yangu ya ajabu hii,
Ikipata Raisi wa kukomesha hayo, ataitwa mnyanyasaji na eti hapendi wawekezaji, ni nchi pekee ambapo wakubwa wake, wanauhuru wa kufanya biashara na wasilipe Kodi eti tu wamekuwa viongozi, unajiuliza, ni kivipi Kodi za wananchi zinatumika kuwalipa?
Nenda US, Trampo alichunguzwa Kwa kampuni yake ilipoonekana kuna kipindi ilitaka kukwepa kulipa kodi, tofauti na kwetu ambapo kiongozi anaweza kuwa imma Muuza ngada ama fam...! Yake na bado Watanzania wakaendelea kupiga makofi na kusifia
Mungu wangu..!