Kwanini Mabasi makubwa huwekwa silencer kwa muda mrefu sana?

Farolito

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
12,001
Reaction score
27,175
Wakuu,

Ni ipi sababu ya muhimu sana kiasi kwamba mabasi makubwa huwekwa kwenye silencer muda mrefu sana hata masaa mawili,kwa mfano gari inaweza kuwa inaondoka SAA 1.00 kamili asubuhi lakini tangu saa 12.00 asubuhi inakuwa imewashwa.

Je sio matumizi mabaya ya mafuta?au kuna sababu ya kiufundi zaidi?

Kwanini isiwashwe dakika 5 au kumi kabla ya kuanza safari?

Karibuni


Sent using Jamii Forums mobile app
 
ABC Upper Class my favourite bus kwa safari za Dom, Singida kutoka Dar es Salaam.

Wadau tupeni jibu la hili swali.
 
Yale yanakuwa na rotation kubwa kwenye engine na inasaidia oil kupanda kwa wakati kwenye mzunguko wake na kufanya engine kuwa nyepesi na tayari kuanza safari na baada ya mwendo mrefu wa safari sio gaei kubwa tuu hata ndogo unatakiwa gari hata kaa hujamaliza au kufika sshemu husika lakini ukasimama haitakiwa gari ulizime mda huo huo imatakiwa kuliacha kwa muda ili lipoe na oil ipoe kwa wakati
 
Mkuu sio gari kubwa tuu..sio mabasi tuu hata gari ndogo pia wewe umezoea kuendesha town trip huwezi toka na gari dar to dodoma non stop ukafika ukaizima sio sawa kwa afya ya gari.. gari nyingi za disel haswa huwa na turbo huwezi tumia gari kwa mda mrefu ukafika na kuizima tuùuu unaweza ukaua engine mazima..lazima uiache ipoe kwanza taratibu ndio uizime..ndio maana kuna gari nyingine kama nissan patrol na landcruise zinafungwa turbo timer
 
Asante kwa maelezo lakini naona kama muda mrefu sana huo,dakika 20 kweli hazitoshi?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli mkuu kwa upande wa gari ndogo au hata kubwa naelewa ukitoka safari lazima uiache kwa muda Fulani kabla ya kuzima ila hapa nazungumzia mabasi ambayo wakati mwingine yameanzia safari hapo na inawezekana siku ya jana yake ndio yalisafiri
Sent using Jamii Forums mobile app
 
JMC Pia yuko vizuri mbona ngoja this timw nipande hii Gari nionje hiyo Radha wanayoisifu watu.
 
Ha ha mkuu,sina sababu yoyote ya kuitangaza ABC nimeamua kutumia kama mfani tu japo mimi pia ni mteja wa kawaida tu kwakua hua naitumia mara kwa mara kwa safari za Singida.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…