Kwanini Mabasi makubwa huwekwa silencer kwa muda mrefu sana?

Kwanini Mabasi makubwa huwekwa silencer kwa muda mrefu sana?

Hakuna kitu kinaitwa warm up kwa engine za miaka hii, labda uzungumzie za miaka hiyo, siku hizi engine nyingi ni low rev philosophy, yaan maxmum torque at 1300 rpm ,

Ukiniambia mfumo wa upepo nitakuelewa , napo pia kwa basi ya abiria ambayo haivutii trela inatakiwa ndani ya dk 10 iwe full pressured

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwahiyo oil sikuhizi inapata moto ghafla tu bin vu chap ishalainika na ishasambaa katika engine nzima?
 
Kwahiyo oil sikuhizi inapata moto ghafla tu bin vu chap ishalainika na ishasambaa katika engine nzima?
Japo umeuliza kwa kejeli!!!

Haichukui hata sekunde 30 kabla ya oil haijasambaa engine nzima , by the time taa ya oil imezima , oil inakuwa ilishafika kila sehemu ya engine
Scenario ya oil kupata moto , haikubaliki na engine manufacure yeyote , maana ndipo majanga yanapoanzia , engine nyingi zina oil cooler , lengo likiwa ni kuifanya oil iwe katika temperature sawa na coolant (maji)



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Angalau wewe ndiyo umejibu kitu kunachoeleweka. ..vizuri sana.
Muda wa kufanya warm up hautakiwi kuzidi dk 10 kama air presure iko sawa ,
Wanachofanya hao wenye basi kungurumisha engine zaidi ya masaa mawili ni uharibifu tu wa engine
Diesel engine hasa hizi kubwa huwa piston inakuwa lubricated kupitia oil nozzle iliyopo chini ya crankcase , to the best of my knowlede , kunakua na very litlle au nil piston lubrication , wakati engine ikiwa silencer( idling). Kwa maana hiyo manufacure wengi hawashauri sana long time idling , sababu ya premature wearing of piston due to insufficient lubricants

Muda pekee unaoshauriwa ku idle diesel engine , (turbocharged only) ni pale unaposimama baada ya kufanya kazi ngumu, mathalan ukipanda milima mkali halafu ukalazimika kusimama , basi inashauriwa kusubiri dk 5 ili kuruhusu turbo ambayo ilikuwa ina mizunguko karibia 200000 per min, ipunguze mizunguko yake kuwa kawaida huku iki enjoy lubrication kutoka kwenye oil pump, unapozima engine wakati turbo ipo red hot jumlisha mizunguko mikali, utasababisha turbo izunguke baadhi ya rotation ikiwa kavu maana unapozima engine na oil pump inasimama muda huo huo.

Kwa gari ndogo za petrol, non turbocharged diesel engine hakuna sababu ya ku idle , hata kama umetoka safari ya mbali , mana katika hali ya kawaida , engine huwa inakuwa inaoperate at a certain temperature ambayo mara nyingi inakuwa constant.






Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwifwa my super doctor, madereva wetu hawako professional and well trained, wanamaliza mafuta bure tuuu
Sio kweli mkuu..huwezi washa gari na kuanza safari hapo hapo..hata sheria mafunzo ya udereva hayafunzi hivyo..utaambiwa pima oil cheki maji kwenye rejeta then washa gari wakati inaunguruma unafanya ukaguzi wa vitu vingine vidogo vidogo kama upepo kwenye tyre,taa n.k.

Kwanza lazima uwasha gari na kuiacha ikiunguluma kabla ya kuanza safari ili kwanza ipandishe oil then ndio uanze safari ndio taratibu zilivyo..sio gari unawasha na kuweka gia nakuondoka hapana sio kweli utaua engine.
 
Wakuu,

Ni ipi sababu ya muhimu sana kiasi kwamba mabasi makubwa huwekwa kwenye silencer muda mrefu sana hata masaa mawili,kwa mfano gari inaweza kuwa inaondoka SAA 1.00 kamili asubuhi lakini tangu saa 12.00 asubuhi inakuwa imewashwa.

Je sio matumizi mabaya ya mafuta?au kuna sababu ya kiufundi zaidi?

Kwanini isiwashwe dakika 5 au kumi kabla ya kuanza safari?

Karibuni


Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbuka gari hiyo inakwenda kufanya safari ndefu ya masaa mengi sana na ikitoka hapo ni mpele mpela vurugu mechi bila kuzimwa non stop zaidi ya masaa 12..inatakiwa ikitoka hapo iwe isha pashwa vya kutosha coz inaingia kwenye shuluba na mchuano wa non stop panda shuka milima kama jua na mvua vyake..

Swali lako dogo sana ungekuwa dereva au fundi usingeliuliza.huwezi washa gari nakuanza kuitumia hapo hapo maspeed n.k utaua engine siku mbili tuu..

Hujawahi jiuliza kwanini wachezaji kabla hawajaingia uwanjani hasa mchezaji wa sab unakuta anaanza kupasha misuli moto na mwili akiwa nje ya uwanja??.
 
Duniani huko wameshaanza kutumia magari ya umeme. Sisi ndio kwanza tuna "convert" yatumie gas! Khaaa!
Mbona hata hapa zipo za kutosha sana..sema changamoto kwenye vipuli hasa hasa HV BATTERY na hata wenye navyo bado changamoto kwenye bei bado nimzozo pia wanatandika sana bei juu..na changamoto nyingine mafundi ndio wanaziharibu na watumiaji pia ndio wauwaji namba moja..

Sijisifu lkn kwabahati nzuri zote nilizokutana nazo nafurahi nilifanikiwa kuzitibu na kama hazikutengamaa bali nilifanikiwa kujua tatizo ni nn na solution yake ni nn?? Ingawa wenye nazo hawakuweza kugaramikia spea..
 
Yale yanakuwa na rotation kubwa kwenye engine na inasaidia oil kupanda kwa wakati kwenye mzunguko wake na kufanya engine kuwa nyepesi na tayari kuanza safari na baada ya mwendo mrefu wa safari sio gaei kubwa tuu hata ndogo unatakiwa gari hata kaa hujamaliza au kufika sshemu husika lakini ukasimama haitakiwa gari ulizime mda huo huo imatakiwa kuliacha kwa muda ili lipoe na oil ipoe kwa wakati
Uzi ufungwe.
 
Kwa waliopanda mabasi ya NEW FORCE na GOLDEN DEER haina ubishi kwamba hotelini Aljazeera zinazimwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli
New force na golden deer hawakai na bus muda mrefu , wanaziuza

Location ya aljazeera hotel ukitokea pande zote ,ni flat , engine temp huwa normal turbo kwa mazingira yale inakuwa haipo katika full boost , thus mizunguko kidogo ya ku relax hata ukizima engine damage inakua ni kidogo,
Lakini kama hao new force wangekua wanakula let's say bismilahi pale juu, ili wawe wanazima gari mara baada ya kupandisha kitonga,majibu wangeyapata mapema sana,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli gari inaenda safari ndefu lakini nilichouliza ni huko kupashwa muda mrefu,halafu kama umepitia post za baadhi ya wachangiaji utaona kuna wengine hawakubaliani na hilo suala labda kwa muda mfupi
Kumbuka gari hiyo inakwenda kufanya safari ndefu ya masaa mengi sana na ikitoka hapo ni mpele mpela vurugu mechi bila kuzimwa non stop zaidi ya masaa 12..inatakiwa ikitoka hapo iwe isha pashwa vya kutosha coz inaingia kwenye shuluba na mchuano wa non stop panda shuka milima kama jua na mvua vyake..

Swali lako dogo sana ungekuwa dereva au fundi usingeliuliza.huwezi washa gari nakuanza kuitumia hapo hapo maspeed n.k utaua engine siku mbili tuu..

Hujawahi jiuliza kwanini wachezaji kabla hawajaingia uwanjani hasa mchezaji wa sab unakuta anaanza kupasha misuli moto na mwili akiwa nje ya uwanja??.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom