Kwanini mabosi wengi ikifika muda wa kujaza kifusi kwenye nyumba huwa hamtaki?

Kifusi ni moja ya hidden cost kwenye ujenzi

Huwa hatufikirii sana hilo ila kinagharimu sana ikitegemea ujazo utakaoingia kwenye nyumba yote

​
  • Gharama inaanza utakapokipata je, watakuuzia bei gani?​
  • Utakaowalipa kukipakia kwenye gari ​
  • Wale watakaokijaza site ​
  • Na usafiri​
Hii kitu huwa inawauma sana maboss maana mafundi wengi huwa hawakumbuki kuwaambia mabosi. Inakuwa nje ya bajeti ya mwenye nyumba

Iliwahi kunigharimu sana hii, msingi wa nyumba ulienda juu sana hivyo mashimo kwenye vyumba na korido yakawa marefu kilihitajika kifusi cha maana kmmmk

Ukiacha kifusi kwa ajili ya nyumba yenyewe huwa kuna kifusi cha kufanyia levelling ikitegemea kiwanja kilivyo zote hizi ni gharama zilozojificha wakati wa ujenzi
​
 
Eti
uelewa mbovu au ni nini?
Ha ha ha ni ngumu sana kutoa hela kufanya kitu 'kisichoonekana' impact yake. Unaambiwa eti hapa tujaze mende 8 yaani kama 2m wakati hio 2m tukijenga tofali tunafika mbali sana. Kwa kweli hata mimi kujaza kifusi ni mwisho kabisa kwanza lazima mashimo ya choo yachimbwe yasaidie kupunguza maumuvu.
 
Hii hatua inakula hela kifala sana.
 
Mi nilibahatika uwanja ulikuwa na gema kidogo,nikatumia hilo kujaza udongo ,walinipiga tu gharama ya kujazia
 
Yeah ni bora ufanye mambo mengine kwenye ujenzi ili usiharibu bajeti yako kwanza

Uzuri wa kifusi hata ukishaezeka kinajazwa tu ili mradi kwa ndani uwe na majukwaa ya kusaidia kazi za juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…