Kwanini mabosi wengi ikifika muda wa kujaza kifusi kwenye nyumba huwa hamtaki?

Kifusi ni moja ya hidden cost kwenye ujenzi

Huwa hatufikirii sana hilo ila kinagharimu sana ikitegemea ujazo utakaoingia kwenye nyumba yote

​
  • Gharama inaanza utakapokipata je, watakuuzia bei gani?​
  • Utakaowalipa kukipakia kwenye gari ​
  • Wale watakaokijaza site ​
  • Na usafiri​
Hii kitu huwa inawauma sana maboss maana mafundi wengi huwa hawakumbuki kuwaambia mabosi. Inakuwa nje ya bajeti ya mwenye nyumba

Iliwahi kunigharimu sana hii, msingi wa nyumba ulienda juu sana hivyo mashimo kwenye vyumba na korido yakawa marefu kilihitajika kifusi cha maana kmmmk

Ukiacha kifusi kwa ajili ya nyumba yenyewe huwa kuna kifusi cha kufanyia levelling ikitegemea kiwanja kilivyo zote hizi ni gharama zilozojificha wakati wa ujenzi
​
Gharama zimejificha vipi wakati ni kitu kinachoeleweka kabla ya ujenzi? Mimi nadhani ujenzi wetu bado ni kienyeji, na usiofuata mahesabu. Mahesabu madogo tu yanatosha kujua ukubwa wa kifusi kabla hata hujaanza nyumba. NB: Bongo kuna mitego ya kitapeli kwenye mambo mengi hivyo mafundi hutumia huu mwanya kupiga fedha.
 
Juzi tu nimetoka kuumia yaan ile tata moja ni 360000 harafu fundi anasema zinatakiwa tata nne . Kujenga ni gharama sana na mara nyingi kifusi hua hatukiwekei bajeti hapo ndo shida inapoanza maana fundi nae anakua analalamika bila kifusi kujenga kwake kuna kua kwa shida hasa kuseti majukwaa
 
Gharama zimejificha vipi wakati ni kitu kinachoeleweka kabla ya ujenzi? Mimi nadhani ujenzi wetu bado ni kienyeji, na usiofuata mahesabu. Mahesabu madogo tu yanatosha kujua ukubwa wa kifusi kabla hata hujaanza nyumba. NB: Bongo kuna mitego ya kitapeli kwenye mambo mengi hivyo mafundi hutumia huu mwanya kupiga fedha.
Kwa hiyo ukipewa ramani unajua exactly kiasi cha kifusi kitakachohitajika?

Au utajua kiasi cha kifusi kinachohitajika baada ya msingi kujengwa?

Ipo hivi kiwango cha kifusi kitahitajika inategemea:

  • Mwinuko wa eneo (slope)
  • Kina cha msingi
  • Aina ya msingi inayotumika
  • Kiwango cha kukandamiza (compaction) kifusi
Utajuaje haya kama bado haujajenga msingi? Ndio maana huwa tunasema ni hidden cost

Wazo la kujua kifusi kitahitajika lipo kabla hata ya ujenzi, ila kiasi gani hasa cha kifusi utahitaji ni mpaka msingi ujengwe, hapo sasa utaweza kutumia hesabu za Ujazo (M³=urefu×upana×kimo)

Ukipata jumla ya M³ za msingi wote hapo sasa ndio itakusaidia kujua gharama halisi na itakusaidia kujua utumie aina gani ya truck kama ni canter, fuso bajaj, fuso double, mende, Howo m³20 n.k na bei zao
 
Maji na kifusi...
Wengi wao huchukulia poa lakini baadaye hugeuka milio
Sahihi

Pia kuna mbao za majukwaa na za kukodi, usafiri wa materials, kibali cha ujenzi, katika visa vingine kuna kusogeza tofali na mchanga kama viko mbali na msingi unapojengwa, umeme,

Bado kuna kuibiwa unakuta bosi anapigwa analazimika aongeze nondo hata 2 au 1 mara mfuko 1 wa cement fundi amalizie kazi, misumari n.k

Ukisema uandike kila gharama au kitu umenunua utagundua jinsi gani tunazika fedha nyingi kwenye ujenzi
 
Kwa hiyo ukipewa ramani unajua exactly kiasi cha kifusi kitakachohitajika?

Au utajua kiasi cha kifusi kinachohitajika baada ya msingi kujengwa?

Ipo hivi kiwango cha kifusi kitahitajika inategemea:

  • Mwinuko wa eneo (slope)
  • Kina cha msingi
  • Aina ya msingi inayotumika
  • Kiwango cha kukandamiza (compaction) kifusi
Utajuaje haya kama bado haujajenga msingi? Ndio maana huwa tunasema ni hidden cost

Wazo la kujua kifusi kitahitajika lipo kabla hata ya ujenzi, ila kiasi gani hasa cha kifusi utahitaji ni mpaka msingi ujengwe, hapo sasa utaweza kutumia hesabu za Ujazo (M³=urefu×upana×kimo)

Ukipata jumla ya M³ za msingi wote hapo sasa ndio itakusaidia kujua gharama halisi na itakusaidia kujua utumie aina gani ya truck kama ni canter, fuso bajaj, fuso double, mende, Howo m³20 n.k na bei zao
Unaweza kupata makadirio vizuri kabisa, lakini ikiwa unaenda kwa kutumia utamaduni wa kitanzania wa ''mazoea na kuigana'' hutaweza. Huwezi kupata exactly figure lakini makario unaweza kabisa. Watu wanapiga mahesabu ya anga za juu na wanapaa kwenda mwezini, mambo madogo kama hayo yashinikane? You must be kidding dear! NB: labda hujui wataalam wanaoitwa quantity surveyors wana kazi gani.. The real problem ni kuwa nyumba zetu tunajenga kwa kutumia mazoea na siyo utaalam.
 
Kifusi ni moja ya hidden cost kwenye ujenzi

Huwa hatufikirii sana hilo ila kinagharimu sana ikitegemea ujazo utakaoingia kwenye nyumba yote

​
  • Gharama inaanza utakapokipata je, watakuuzia bei gani?​
  • Utakaowalipa kukipakia kwenye gari ​
  • Wale watakaokijaza site ​
  • Na usafiri​
Hii kitu huwa inawauma sana maboss maana mafundi wengi huwa hawakumbuki kuwaambia mabosi. Inakuwa nje ya bajeti ya mwenye nyumba

Iliwahi kunigharimu sana hii, msingi wa nyumba ulienda juu sana hivyo mashimo kwenye vyumba na korido yakawa marefu kilihitajika kifusi cha maana kmmmk

Ukiacha kifusi kwa ajili ya nyumba yenyewe huwa kuna kifusi cha kufanyia levelling ikitegemea kiwanja kilivyo zote hizi ni gharama zilozojificha wakati wa ujenzi
​
Fundi alinipigia hesabu ya trip 8 kujaza kifusi, kulikuwa na kichuguu pembeni nikaamua kukibomoa kwa mikono yangu mwenyewe.
Asubuhi na jioni nikamaliza
 
Unaweza kupata makadirio vizuri kabisa, lakini ikiwa unaenda kwa kutumia utamaduni wa kitanzania wa ''mazoea na kuigana'' hutaweza. Huwezi kupata exactly figure lakini makario unaweza kabisa. Watu wanapiga mahesabu ya anga za juu na wanapaa kwenda mwezini, mambo madogo kama hayo yashinikane? You must be kidding dear! NB: labda hujui wataalam wanaoitwa quantity surveyors wana kazi gani.. The real problem ni kuwa nyumba zetu tunajenga kwa kutumia mazoea na siyo utaalam.
Kumbe makadirio, kwa hiyo tunarudi palepale, msingi ukishajengwa ndio utapata jibu kamili la kifusi kinachohitajika

Hao quantity surveyors wanachofanya ni makadirio si figure halisi ndio maana wakati fulani huongeza viwango
 
Chochote kwenye ujenzi wa nyumba ni makadirio. Huwezi kuwa na exactly figure. Anyway, tumekubaliana kuwa inawezekana kupunguza au kumaliza hayo malalamiko ya vifusi kati ya fundi na mwenye nyumba kama utaalam zaidi utahusika. Hali ya sasa ni kwamba mafundi wanapitia kwenye kichochoro cha kutojua makadirio.
 
Back
Top Bottom