SoC02 Kwanini mafanikio kupitia elimu yanaonekana kama mvua inyeshayo jangwani?

SoC02 Kwanini mafanikio kupitia elimu yanaonekana kama mvua inyeshayo jangwani?

Stories of Change - 2022 Competition

zephania5

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2022
Posts
232
Reaction score
807
Kwa miaka mingi kabla na hata baada ya uhuru, watanzania wengi na hata watu wengine duniani kote, wamekuwa na imani ya kuwa, elimu ndio ufunguo wa maisha. Lakini katika uhalisia wake elimu na mafanikio katika maisha vimekuwa vitu viwili tofauti kabisa. Ni kama mtu aliyeko kusini akiitafuta kaskazini. Kumekuwa na hoja na mijada mbalimbali hata kule bungeni ya kuwa, Watoro wengi ndio wenye mafanikio, kutokana na maoni na utafiti uliofanyika. Hali hii hufanya wasomi kudharaulika au kujidharau wao wenyewe, vile vile hali kama hii inasababisha ionekane ya kuwa, mafanikio katika elimu, ni kama mvua inyeshayo jangwani, kutokea kwake ni nadra na kwa kubahatisha sana.

Kwa nini wasomi kudharaulika, twende pamoja katika makala hii
'' Kaka Robert amka! ni muda wa shamba, leo umechelewa sana kujiandaa, baba na mama wametangulia tayari. Tangu saa 11 alfajiri, wanasubiri uwapelekee mbolea ya samadi, wakakuelekeze namna ya kupanda viazi na maharage. Nadhani atakuwa amekasirika sana, amechoka kukusubiri, si unamjua baba hana mchezo na kazi za shamba...,''.

Hakika haya yatakuwa ni maneno yenye kukereketa kwa upande wa Robert, mhitimu wa shahada ya uhandisi kwenye chuo kikuu cha Dar es Salaam, tawi la Mbeya (MUST). Ni mwaka wa pili sasa tangu atume maombi ya kazi, katika shirika la umeme Tanzania(TANESCO). Miongoni mwa watu laki mbili waliotuma maombi ya kazi, na wakati huo nafasi mia mbili tu zikiwa zinahitajika.

Matumaini ya Robert yatafikiwa tu, kama endapo maombi yake ya kazi yatakubaliwa, kwa kudra za Mwenyezi Mungu. La sivyo ndoto zitabaki kuwa ndoto tu, siku zote. Kijana wa kitanzania toka familia duni, inayotegemea zizi lenye ng'ombe na mbuzi wachache, waliomalizika kwa kulipa karo na michango ya shule na maisha yenye kutegemea mvua za masika, ndipo chakula kipatikane shambani. Kwa mtazamo wa haraka Robert anaonekana kuwa mzigo badala ya kuwa msaada, elimu na ujuzi wake tangu shule ya awali hadi chuo kikuu, inashindwa kubadilisha hali yake mwenyewe, pamoja na hali ya nyumbani, kwa kipindi chote alichokaa nyumbani.
Nikimaliza kusoma nitafanya nini?
Mwalimu mmoja katika chuo kikuu cha Dodoma, aliwahi kuwauliza wanafunzi waliokuwa wamejiunga na mwaka wa kwanza wa masomo akisema '' Mmekuja kusoma uuguzi kwa lengo gani?''. Wapo waliosema '' Tumekuja kusoma hapa kwa ajili ya kusaidia watu'', wengine wakasema '' Tumekuja kuwa wauguzi kwa sababu ya wito''.

Lakini kwa kweli wengi wao walikuwa wamewaahidi wazazi wao, ndugu zao, jamaa zao na hata wapenzi wao, kuishi maisha yaliyo bora zaidi, mara baada ya kuhitimu elimu ya juu. Kabla ya kumsaidia mwingine hakikisha kwanza usalama wako, na hivyo elimu ya kweli ni ile inayoanza kuleta mabadiliko kiafya, kiakili, kijamii na kiuchumi, kwa yule anayeipata kabla ya kuleta mabadiliko kwa wengine pia. Wasomi wengi wapo mtaani wakiwa hawana matumaini wala dira ya maisha ya leo wala ya baadae.

Viatu vimechakaa na vumbi, kutwa kiguu na njia kugonga milango ya ofisi, popote pale walipotangaza nafasi za kazi, hata kama si ile iliyokuwa ni malengo yake. Wengine wapo sekondari au chuo kikuu, bado wanajiuliza ya kuwa '' Nikimaliza kusoma, nitafanya kazi gani''. Ndipo sasa unakuja ule msemo wa waswahili '' Shule
ilitudai akili, kitaa kinatudai mafanikio''.

Maisha yakikuchagulia ngoma, na wewe chagua namna ya kuyacheza ndugu yangu.
Huu ndio mpango mzima!
Umeshawahi kufikiria kumiliki kampuni au shirika lako mwenyewe, na wewe uisaidie serikali kutoa ajira, kwa wasiokuwa na ajira. Ni jambo gumu kusubiri serikali itoe ajira kwa wananchi wote, hakuna serikali kama hiyo duniani. Wapo wengi waliofeli masomo, na kushindwa kuendelea, lakini leo wanamiliki shule ama vyuo. Unaweza kuona hilo haliwezekani ama jambo gumu, maana kazi rahisi kwako ni kubeti, kuwekekeza kwenye makampuni ya mtandaoni yasiyokuwa na ofisi wala mikataba yeyote, na kuishia kupoteza pesa kila siku. Utakuja kuzinduka, ni wewe peke yako hadi leo unaeendelea kuishi kwenu, huku ukiendelea kusifia mapishi ya mama yako pale jikoni. Heshima haiji bure ndugu, acha matumizi mabaya ya muda na akili.

Maisha ni lazima yaendelee. Muda mwingine si rahisi kutambua kusudi lako hasa la kuishi, ni kweli kuwa elimu ndio ufunguo wa maisha, maana ni vigumu sana jamii yenye watu wajinga kupiga hatua katika maendeleo yakiwa ni ya kiafya, kijamii, kiuchumi au kidiplomasia, lakini si lazima kuweka matumaini yote katika fani uliyoisomea ikiwa ni kwamba uliipenda au ulifuata upepo kama bendera, ili kuleta mabadiliko mazuri na yanayohitajika kwenye maisha yako au kwenye jamii uliyopo.

Mwalimu Nyerere aliacha kazi ya ualimu akajikita kwenye siasa kupitia chama cha TANU, ili kuleta uhuru kwa Tanganyika, ambayo leo ni Tanzania. Leo mimi na wewe, tuna uhuru wa kujieleza kama hivi, tuna uhuru wa kwenda popote duniani, tuna uhuru wa kufanya shughuli zozote kwa ajili ya maendeleo yetu wenyewe. Lakini ajabu kubwa ni kwamba wengi wetu hapa ni watumwa wa kifikra.

Kuna watu huzikalia fursa wao wenyewe, na kisha kuanza kuangaza huku na kule wakitafuta fursa na wala wasizione, huo ni upofu wa akili kweli. Wengine hukosa hamasa au msukumo wa ndani, ili kuzifanyia kazi fursa walizoziona au kupatiwa, uoga na aibu ya kushindwa huwamaliza wengi, wasomi na kwa wasio wasomi. Elimu na ujuzi wako visipotee bure, jaribu kutumia uwezo wako wote, vipawa vyako vyote pamoja na nafasi zote ulizojaliwa na Mwenyezi Mungu, ikiwa ni afya, nguvu na akili. Pia rasilimali au mtaji wowote ulio nao, waweza kukufikisha popote pale unapotaka kufika na kuwa mtu bora zaidi.

Utajiri wanaoukimbia wasomi wengi
Wewe kijana mwenzangu, uliyekimbilia mjini kutafuta maisha baada ya kumaliza masomo yako, huku ukishinda njaa kila siku, rudi kijijini kwenu, maana kupendeza sio kushiba. Utajiri umeuacha kijijini kwenu, umeacha ardhi nzuri kwenye mashamba, pamoja na mabonde yenye maji ya kutosha, kwa ajili ya kilimo cha mazao mbalimbali kama maboga, tikitimaji, machungwa, mchicha, miwa, maparachichi ama ufugaji wa nyuki, samaki,ng'ombe. Ukipata kipato cha kutosha unaweza kumiliki zahanati yako mwenyewe, shule yako, hoteli yako mwenyewe na miradi mingine mingi huko mjini au vijijini.

Maisha yana njia nyingi, na unaweza kutumia njia yeyote kufika kwenye hatima yako. Mfano kabla ya kupiga hatua na mageuzi ya kiviwanda, kiteknolojia, pamoja na ulinzi, nchi kama Marekani na China zilikuwa tayari zimejidhatiti kwenye kilimo, idadi kubwa ya watu katika nchi hizi, ikawa sio kipingamizi kabisa katika maendeleo.
Maisha kupitia ajira
Kama ukipata nafasi ya kuajiriwa, kama ilivyo ndoto za Robert, kama tulivyoona mwanzo wa makala hii. Fanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu, udumu na upande viwango pia, sababu wengi waliitamani lakini wakakosa. Na wengine waliipata nafasi hiyo lakini wakaipoteza, maana hata wewe mwenyewe ni shahidi wa mambo haya, kama ulivyoona na kusikia kwa watumishi walegevu serikalini, walivyotumbuliwa enzi za utawala wa Hayati, John Pombe Magufuli, na wanavyoendelelea kutenguliwa siku kwa siku na raisi wa sasa, Samia Suluhu Hassan.
Inawezekana,usipokata tamaa!
Lakini ndugu yangu nakuambia leo, usikate tamaa kwa kupoteza au kukosa ajira au kazi uliyoipenda au uliyokuwa unaitegemea, jifunze kwa watu waliofanikiwa kutokana na kushindwa mara nyingi kama akina Thomas Edison, Nelson Mandela na MacDonald, ijapo sitawazungumzia habari zao katika makala hii. Maisha ni kitendawili kwa wengi, na hivyo haina budi kujifunza kila siku, kutokana mafunzo unayoyapata kwenye maisha. Hii ndio maana ya elimu ni bahari au elimu haina mwisho na ni zaidi ya kalamu na daftari. Katu katu! Msomi usikibali kudharaulika tena, uwe kichwa na si mkia, uwe msaada na si mzigo tena. Wewe ni mtu mwenye kutumainiwa katika jamii na taifa lako, kama maji kwa msafiri jangwani.
 
Upvote 334
Hiyo ni moja tu ya sababu, lakini kwa kweli hizi shule zetu za ufundi zilikuwa zimesahauliwa kwa muda mrefu, mafunzo mengi ni ya nadharia na si vitendo. Karakana za kufundishia pamoja na vifaa zimekuwa changamoto. Nipende kuishukuru awamu ya tano kwa kuliona hili, kwa namna yake imetoa mchango mkubwa, kwa shule za vipaji na ufundi kwa kuboresha miundimbinu na mazingira rafiki ya kijifunza. Lakini changamoto nyingine ni kuwapata walimu wenye ujuzi pamoja na uzoefu wa haya masomo, kama electrical drafting, technical drawing, plumbing, motor vehicle na mengineyo. Nadharia imekuwa ni nyingi kuliko vitendo, na kusababisha wahitimu kushindwa kujiamini katika fani zao, na kusababisha ndoto kubadilika badilika, katika vipindi tofauti vya maisha.
Reality
 
Hakuna Mtanzania Msomi mwenye akili timamu aliye shindwa kujisaidia, nakataa, nani huyo?? mtaje! .......pengine Tatizo lako unaangalia wasomi waleee;

walevi, wauza madawa ya kulevya. wanywa Gongo, na wale walio rogwa na koo zao ajili ya wivu, Mizimu, waliokimbia uganga wa koo!,vitukuu vya wachawi!

make wale wanaambiwa kabisa ukimaliza kusoma uje ukamate tungulri number 21, kuwanga na kuroga ni jadi yetu! sasa kataa uone moto!....ndo hao unao wasemea!

na kwa mujibu wa Biblia uchawi upo, mfano; Musa mtumishi wa Mungu alirogwa!! sasa kam Musa aliyeongea na Mungu live alirogwa, wewe msomi mtanzania wa kawaida kwa nini usirogwe?

hapo usilinganishe waliorogwa na watu wenye akili timamu, nikupe mfano tu umesomea labda Bee keeping! utashindwaje kulina na kuuza asali yako binafsi wakati ukisubili ajira??

Mwalimu fungua drs la Tuition uani kwenu!! ..ukisubiri ajira!.........Business admin...toa ushauri kwa wafanya bishara kwa malipo kidogo wa draftie hata Business plan zao! wkt unasubiri ajira shida iko wapi?

Umesoma chuo gani ambacho hawakukupa life skills........... Maisha na kazi?? tamka! ..... niwaseme sasa hivi! ukisoma chuo wanakupa na mbinu za kujiajili! wkt ukisubiri ajira never hukwami
Weee dada angu ushawahi ona wapi mtu mwenye mafanikio makubwa duniani akajivunia shule yake au unataka kupisha tuuuh angalia vizuri bana elimu na mafanikio ni vitu viwli tofauti
 
Usipoteze Dira!!! Maarifa na Elimu ni kitu kilekile!! hujui! ....uvivu na ulevi ni Multi secterial na hulka ya Mtu binafsi nI makosa kuuliza walevi, wavivu, wanatoka wapi!!......Kenyataa mdogo ni Rais mlevi kupindukia mpaka sasa!!

Mishahara ya Waalimu wetu! inawatosha sana, umeongopa sijakosea sana tu, acha kukariri!! ...km haiwatoshi mbona hawalalamiki? kazi wanafanya! kuna watu wanasoma ualimu mpaka sasa??

pesa na matumizi ni akili ya Mtu husika tu! baasi!

hata mtu mmoja tu tukikupa Bajeti yote ya Marekani km ni mbumbu hutoki kamwe!!......Hakuna Mwafrica/Mtanzania mpumbavu ivo wa kuangaliwa na ukoo Mzima? ili iweje?..

km weye unafanya ivo basi jua kabisaaa una tatizo la msingi, wategemezi hawana shida bali wewe unae waendekeza wake hapo ndo unafaa kuchapwa hamsa ishirini ili akili ikukae sawa!

Sasa km mshahara una makato, ajili ya Mkopo uliokopeshwa kwa hiari yako!! ulitaka wakopeshaji wakate nini?? Makalio au!! .......bana wee hiyo Elimu yako hiyo inatia ukakasi....uliwahi sikia vyeti fake!
Tatizo kuna kitu kichwani umekieka ndo maana utaki kukubali ukweliii utaki kutoka nje ya kile unakiamini
 
Tatizo kuna kitu kichwani umekieka ndo maana utaki kukubali ukweliii utaki kutoka nje ya kile unakiamini
Imani siyo dhambi!.....acha majibu rahisi rahisi hayo! kijana utafail mbaya na maisha!
 
Si wote wenye elimu wana maarifa, na hiki ndicho kinachosumbua wengi. Elimu au fani yeyote ina ethics,
Niki kusema sana utajisikia vibaya! Mkuu Lkn hujui unacho kiongea! ........Maarifa=na Elimu= Mystical knowledge=Elimu!! ......My people are perishing due to lack of Knowledge! .....

Maarifa ni uwezo wa kujua mambo mengi...na hiyo inakuja kwa kusoma sana maarifa(Elimu)ya Dunia/ ya Mungu. au unatafuta tuition ya bure wewe??
 
Unaongea mengi sana, lakini unarudi pale pale. Moja ya matatizo yanayofanya mafanikio kupitia elimu yaonekane kuwa kama mvua inyeshayo jangwani. Ungesoma vizuri ukaelewa usingekuwa na doubt nyingi
Naongea mengi ili uelewe!/Naelimisha jamii forum.......Ona sasa hujui!!!.......Mvua kunyesha Jangwani ni neema ivune! ......Mfano Negev Desert ni jangwa, tena la Mawe lkn

nchi ile wanaongoza kwa Kilimo cha mboga/majani ya mifugo/Matunda Duniani! wasomi maskini wa kilimo wanaenda kusoma Bureeee!

tena kwa kutumia Drop irrigation systems tu!...lkn weye Mswahili unaona ile ni dhambi!
 
Ni heri kama angekuwa daktari au mwalimu, anayejiongezea kipato kwa sababu gharama za maisha zinapanda kila siku, lakini mshahara wake upo pale pale au hadi ifikapo mwisho wa mwezi. Lakini wapo wengi wanaofanya hivyo bila kupenda, ni kwa sababu ndoto zao zimefeli, na maisha ni lazima yaendelee. Hata ukisema utangaze ajira leo, watakutafuta popote ulipo..
Weye Muongo! au hujui! ajira zilivo! mishahara inapanda kwa madaraja!......km mtu anafanya kazi bila kupenda hana wito, ni mpumbavu! aachie nafasi kwa wanaoijua.....akalime........hakulazimishwa na Mtu kuifanya! nchi huru hii!

huwezi ukafanikisha ndoto zako weeee! kila siku! no! ku fail ni sehemu ya Maisha, ni lazima!...... weye siyo wa kwanza! Matajiri mfano (Bakhresa)/wasomi wote Duniani walifail mara kibao weye nani usi fail?.....tena wengine walikuwa wajingaaaa!
 
Si kweli kama watanzania wote wenye kusoma wapo kwenye kazi za maofisini ama za kutokuonekana kama wachawi ama wanajimu wanaoenda anga za mbali. Nikakuambia mwanzo uishi na jamii ya watu wanaokuzunguka vizuri, upate kujua changamoto zinazoikumba nchi yetu na ulimwengu kwa ujumla.
Labda hujanielewa km mtu yuko kazini mfano ni kondakta wa ma bus mkoani utamuona wapi?? well!! analima shambani mtaonana wapi?..hao unao waona idle mitaani wamerogwa
 
Tukubali kujifunza tatizo we
Imani siyo dhambi!.....acha majibu rahisi rahisi hayo! kijana utafail mbaya na maisha!
H
Naongea mengi ili uelewe!/Naelimisha jamii forum.......Ona sasa hujui!!!.......Mvua kunyesha Jangwani ni neema ivune! ......Mfano Negev Desert ni jangwa, tena la Mawe lkn

nchi ile wanaongoza kwa Kilimo cha mboga/majani ya mifugo/Matunda Duniani! wasomi maskini wa kilimo wanaenda kusoma Bureeee!

tena kwa kutumia Drop irrigation systems tu!...lkn weye Mswahili unaona ile ni dhambi!
Hukuelewa dhamira yangu
Naongea mengi ili uelewe!/Naelimisha jamii forum.......Ona sasa hujui!!!.......Mvua kunyesha Jangwani ni neema ivune! ......Mfano Negev Desert ni jangwa, tena la Mawe lkn

nchi ile wanaongoza kwa Kilimo cha mboga/majani ya mifugo/Matunda Duniani! wasomi maskini wa kilimo wanaenda kusoma Bureeee!

tena kwa kutumia Drop irrigation systems tu!...lkn weye Mswahili unaona ile ni dhambi!
Hujasoma andiko ili uelewe, ungeelewa dhima ya '' Kwanini mafanikio kupitia elimu yanaonekana kama mvua inyeshayo jangwani'' usingeshupaza shingo. Mvua ya jangwani ni nadra, na haiwezi kufanya jangwa lisiwe jangwa tena. Kila bedui atamani ayapate maji yake, lakini changamoto kadha wa wa kadha zinafanya upatikanaji uwe adimu. Kama ungesema nini kifanyike ungeonekana mtu mwenye busara.
 
huwezi ukafanikisha ndoto zako weeee! kila siku! no! ku fail ni sehemu ya Maisha, ni lazima!...... weye siyo wa kwanza! Matajiri mfano (Bakhresa)/wasomi wote Duniani walifail mara kibao weye nani usi fail?.....tena wengine walikuwa wajingaaaa!
Rudi ukasome andiko vizuri
 
Umasikini sio dhambi, haya matabaka yamekuwepo tangu zamani,
Umasikini ni dhambi tena kubwa na mbinguni huendi! kam umeumbwa kwa mfano wa Mungu kwa nini uwe maskini?wkt Mungu ni baba yako Tajiri?...kwa nini usimuombe akumegee tena Bure yaani kuomba tu unashindwa??

Hujalielewa lile andiko la Mfalme suleiman hekima ya maskini hudharauliwa kwa kuwa ina chembe chembe za ushetani ndani yake!
 
Weye Muongo! au hujui! ajira zilivo! mishahara inapanda kwa madaraja!......km mtu anafanya kazi bila kupenda hana wito, ni mpumbavu! aachie nafasi kwa wanaoijua.....akalime........hakulazimishwa na Mtu kuifanya! nchi huru hii!
Sasa unataka kumfanya aliyepandisha mishahara aonekane muongo.
 
Weee dada angu ushawahi ona wapi mtu mwenye mafanikio makubwa duniani akajivunia shule yake au unataka kupisha tuuuh angalia vizuri bana elimu na mafanikio ni vitu viwli tofauti
LOOOL! pole sana Babu! kwanza elewa na ufungue akili yako kabisaaaaa ya .......hiyo!! Shule ni Mafanikio toshaaaa kabisaaa!! tena makubwaaa heeee!...unakula kiubwete huko mbele


hata akijivuna utamuonea wapi?? na wewe ni maskini wa maji matitu hukoooo? mvua zikinyesha kazi?? .... anajivuna akiwa na wa level yake hukoo Dubai,/Honolulu VIP Lounge Baba!...wewe kula vihepe vya bei poa unenepe !
 
Umasikini ni dhambi tena kubwa na mbinguni huendi! kam umeumbwa kwa mfano wa Mungu kwa nini uwe maskini?wkt Mungu ni baba yako Tajiri?...kwa nini usimuombe akumegee tena Bure yaani kuomba tu unashindwa??

Hujalielewa lile andiko la Mfalme suleiman hekima ya maskini hudharauliwa kwa kuwa ina chembe chembe za ushetani ndani yake!
Kuwa masikini si dhambi na kuwa tajiri si utukufu, bali ni mapenzi yake Mungu. Ungesema ulegevu ama uvivu ndio dhambi ungeeleweka. Hata mitume na manabii wengi, hawakuacha wala hawakuwa na utajiri wowote, hata Yesu kristo hakuwa na ghorofa duniani
 
Sasa unataka kumfanya aliyepandisha mishahara aonekane muongo.
kama ni muongo pia ni muongo tu!
bali ni mapenzi yake Mungu. Ungesema ulegevu ama uvivu ndio dhambi ungeeleweka. Hata mitume na manabii wengi, hawakuacha wala hawakuwa na utajiri wowote, hata Yesu kristo hakuwa na ghorofa duniani
tena umesema vizuri sana km ni mapenzi yake ongea nae tu!......Manabii kumtumikia Mungu tu ni utajri tosha! usikariri!
Maghorofa siyo utajiri umekariri ndo maana nasema naongea na mtoto!
Rudi ukasome andiko vizuri
sina sababu ya kufanya ivo!
Kwanini mafanikio kupitia elimu yanaonekana kama mvua inyeshayo jangwani'' usingeshupaza shingo. Mvua ya jangwani ni nadra, na haiwezi kufanya jangwa lisiwe jangwa tena. Kila bedui
Kwako elimu ni ngumu haikufai si uiache tuuu!.......Mungu alisema usimuache Elimu aende zake weye ni nani upinge?? acha uone, danganya wakulima wenzako huko mazinde lkn siyo Born town!

wenzako jangwa ni neema!
 
Kuwa masikini si dhambi na kuwa tajiri si utukufu
Maskini anakufuru nyingi na wengi ndo majambazi!wachawi/wanaroga watu tusifanikiwe! kwanza ibada hafanyi!! atatoa wapi sadaka wkt hela hana??...utajiri ni utukufu kwa wenye asili ya utajiri km sisi!!

lkn huna damu ya kitajiri huujui huwezi jua utukufu wake sikia sasa Ibrahim, isack, Yakobo nk walikuwa matajiri wakubwaa ni kufuru...
 
tena umesema vizuri sana km ni mapenzi yake ongea nae tu!......Manabii kumtumikia Mungu tu ni utajri tosha! usikariri!
Maghorofa siyo utajiri umekariri ndo maana nasema naongea na mtoto!

Kwako elimu ni ngumu haikufai si uiache tuuu!.......Mungu alisema usimuache Elimu aende zake weye ni nani upinge?? acha uone, danganya wakulima wenzako huko mazinde lkn siyo Born town!

wenzako jangwa ni neema!
Elimu haijawahi kuwa ngumu na katu siwezi kuiacha, sababu elimu ni zaidi ya kalamu na daftari. Dini ni elimu, jamii inayotuzunguka ni elimu pia, maisha ya kila siku ni darasa. Lakini iwe formal ama informal education, ni lazima iwe yenye kuleta mabadiliko na si vinginevyo.
 
Hao majambazi na wachawi ni masikini wa mawazo, na si masikini wa mali. Kama ulivyosema hata kufanya ibada ni utajiri, kufanya mambo ya staha ni utajiri pia
Maskini anakufuru nyingi na wengi ndo majambazi!wachawi/wanaroga watu tusifanikiwe! kwanza ibada hafanyi!! atatoa wapi sadaka wkt hela hana??...utajiri ni utukufu kwa wenye asili ya utajiri km sisi!!

lkn huna damu ya kitajiri huujui huwezi jua utukufu wake sikia sasa Ibrahim, isack, Yakobo nk walikuwa matajiri wakubwaa ni kufuru...
 
Hao majambazi na wachawi ni masikini wa mawazo, na si masikini wa mali. Kama ulivyosema hata kufanya ibada ni utajiri, kufanya mambo ya staha ni utajiri pia
Umekosea sihivyo! Mungu hakusema ivo! siyo kila ibada ni utajiri! ....kuna,Mahali, vitu, watu wengi humu Duniani wanafanyiwa ibada!....Mfano; ibada za Wafu, Mizimu, Wanyama na Makaburini ni utajiri wa kwenu huko Mahurunga!

usi generalise!
 
utajiri ni utukufu kwa wenye asili ya utajiri km sisi!!
Usigenarilize vilevile, angalia pia vyanzo vya huo utajiri na vyanzo vya huo umaskini ni vipi. Ndipo sasa, useme ni utukufu ama ni dhambi
 
Back
Top Bottom