SoC02 Kwanini mafanikio kupitia elimu yanaonekana kama mvua inyeshayo jangwani?

SoC02 Kwanini mafanikio kupitia elimu yanaonekana kama mvua inyeshayo jangwani?

Stories of Change - 2022 Competition

zephania5

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2022
Posts
232
Reaction score
807
Kwa miaka mingi kabla na hata baada ya uhuru, watanzania wengi na hata watu wengine duniani kote, wamekuwa na imani ya kuwa, elimu ndio ufunguo wa maisha. Lakini katika uhalisia wake elimu na mafanikio katika maisha vimekuwa vitu viwili tofauti kabisa. Ni kama mtu aliyeko kusini akiitafuta kaskazini. Kumekuwa na hoja na mijada mbalimbali hata kule bungeni ya kuwa, Watoro wengi ndio wenye mafanikio, kutokana na maoni na utafiti uliofanyika. Hali hii hufanya wasomi kudharaulika au kujidharau wao wenyewe, vile vile hali kama hii inasababisha ionekane ya kuwa, mafanikio katika elimu, ni kama mvua inyeshayo jangwani, kutokea kwake ni nadra na kwa kubahatisha sana.

Kwa nini wasomi kudharaulika, twende pamoja katika makala hii
'' Kaka Robert amka! ni muda wa shamba, leo umechelewa sana kujiandaa, baba na mama wametangulia tayari. Tangu saa 11 alfajiri, wanasubiri uwapelekee mbolea ya samadi, wakakuelekeze namna ya kupanda viazi na maharage. Nadhani atakuwa amekasirika sana, amechoka kukusubiri, si unamjua baba hana mchezo na kazi za shamba...,''.

Hakika haya yatakuwa ni maneno yenye kukereketa kwa upande wa Robert, mhitimu wa shahada ya uhandisi kwenye chuo kikuu cha Dar es Salaam, tawi la Mbeya (MUST). Ni mwaka wa pili sasa tangu atume maombi ya kazi, katika shirika la umeme Tanzania(TANESCO). Miongoni mwa watu laki mbili waliotuma maombi ya kazi, na wakati huo nafasi mia mbili tu zikiwa zinahitajika.

Matumaini ya Robert yatafikiwa tu, kama endapo maombi yake ya kazi yatakubaliwa, kwa kudra za Mwenyezi Mungu. La sivyo ndoto zitabaki kuwa ndoto tu, siku zote. Kijana wa kitanzania toka familia duni, inayotegemea zizi lenye ng'ombe na mbuzi wachache, waliomalizika kwa kulipa karo na michango ya shule na maisha yenye kutegemea mvua za masika, ndipo chakula kipatikane shambani. Kwa mtazamo wa haraka Robert anaonekana kuwa mzigo badala ya kuwa msaada, elimu na ujuzi wake tangu shule ya awali hadi chuo kikuu, inashindwa kubadilisha hali yake mwenyewe, pamoja na hali ya nyumbani, kwa kipindi chote alichokaa nyumbani.
Nikimaliza kusoma nitafanya nini?
Mwalimu mmoja katika chuo kikuu cha Dodoma, aliwahi kuwauliza wanafunzi waliokuwa wamejiunga na mwaka wa kwanza wa masomo akisema '' Mmekuja kusoma uuguzi kwa lengo gani?''. Wapo waliosema '' Tumekuja kusoma hapa kwa ajili ya kusaidia watu'', wengine wakasema '' Tumekuja kuwa wauguzi kwa sababu ya wito''.

Lakini kwa kweli wengi wao walikuwa wamewaahidi wazazi wao, ndugu zao, jamaa zao na hata wapenzi wao, kuishi maisha yaliyo bora zaidi, mara baada ya kuhitimu elimu ya juu. Kabla ya kumsaidia mwingine hakikisha kwanza usalama wako, na hivyo elimu ya kweli ni ile inayoanza kuleta mabadiliko kiafya, kiakili, kijamii na kiuchumi, kwa yule anayeipata kabla ya kuleta mabadiliko kwa wengine pia. Wasomi wengi wapo mtaani wakiwa hawana matumaini wala dira ya maisha ya leo wala ya baadae.

Viatu vimechakaa na vumbi, kutwa kiguu na njia kugonga milango ya ofisi, popote pale walipotangaza nafasi za kazi, hata kama si ile iliyokuwa ni malengo yake. Wengine wapo sekondari au chuo kikuu, bado wanajiuliza ya kuwa '' Nikimaliza kusoma, nitafanya kazi gani''. Ndipo sasa unakuja ule msemo wa waswahili '' Shule
ilitudai akili, kitaa kinatudai mafanikio''.

Maisha yakikuchagulia ngoma, na wewe chagua namna ya kuyacheza ndugu yangu.
Huu ndio mpango mzima!
Umeshawahi kufikiria kumiliki kampuni au shirika lako mwenyewe, na wewe uisaidie serikali kutoa ajira, kwa wasiokuwa na ajira. Ni jambo gumu kusubiri serikali itoe ajira kwa wananchi wote, hakuna serikali kama hiyo duniani. Wapo wengi waliofeli masomo, na kushindwa kuendelea, lakini leo wanamiliki shule ama vyuo. Unaweza kuona hilo haliwezekani ama jambo gumu, maana kazi rahisi kwako ni kubeti, kuwekekeza kwenye makampuni ya mtandaoni yasiyokuwa na ofisi wala mikataba yeyote, na kuishia kupoteza pesa kila siku. Utakuja kuzinduka, ni wewe peke yako hadi leo unaeendelea kuishi kwenu, huku ukiendelea kusifia mapishi ya mama yako pale jikoni. Heshima haiji bure ndugu, acha matumizi mabaya ya muda na akili.

Maisha ni lazima yaendelee. Muda mwingine si rahisi kutambua kusudi lako hasa la kuishi, ni kweli kuwa elimu ndio ufunguo wa maisha, maana ni vigumu sana jamii yenye watu wajinga kupiga hatua katika maendeleo yakiwa ni ya kiafya, kijamii, kiuchumi au kidiplomasia, lakini si lazima kuweka matumaini yote katika fani uliyoisomea ikiwa ni kwamba uliipenda au ulifuata upepo kama bendera, ili kuleta mabadiliko mazuri na yanayohitajika kwenye maisha yako au kwenye jamii uliyopo.

Mwalimu Nyerere aliacha kazi ya ualimu akajikita kwenye siasa kupitia chama cha TANU, ili kuleta uhuru kwa Tanganyika, ambayo leo ni Tanzania. Leo mimi na wewe, tuna uhuru wa kujieleza kama hivi, tuna uhuru wa kwenda popote duniani, tuna uhuru wa kufanya shughuli zozote kwa ajili ya maendeleo yetu wenyewe. Lakini ajabu kubwa ni kwamba wengi wetu hapa ni watumwa wa kifikra.

Kuna watu huzikalia fursa wao wenyewe, na kisha kuanza kuangaza huku na kule wakitafuta fursa na wala wasizione, huo ni upofu wa akili kweli. Wengine hukosa hamasa au msukumo wa ndani, ili kuzifanyia kazi fursa walizoziona au kupatiwa, uoga na aibu ya kushindwa huwamaliza wengi, wasomi na kwa wasio wasomi. Elimu na ujuzi wako visipotee bure, jaribu kutumia uwezo wako wote, vipawa vyako vyote pamoja na nafasi zote ulizojaliwa na Mwenyezi Mungu, ikiwa ni afya, nguvu na akili. Pia rasilimali au mtaji wowote ulio nao, waweza kukufikisha popote pale unapotaka kufika na kuwa mtu bora zaidi.

Utajiri wanaoukimbia wasomi wengi
Wewe kijana mwenzangu, uliyekimbilia mjini kutafuta maisha baada ya kumaliza masomo yako, huku ukishinda njaa kila siku, rudi kijijini kwenu, maana kupendeza sio kushiba. Utajiri umeuacha kijijini kwenu, umeacha ardhi nzuri kwenye mashamba, pamoja na mabonde yenye maji ya kutosha, kwa ajili ya kilimo cha mazao mbalimbali kama maboga, tikitimaji, machungwa, mchicha, miwa, maparachichi ama ufugaji wa nyuki, samaki,ng'ombe. Ukipata kipato cha kutosha unaweza kumiliki zahanati yako mwenyewe, shule yako, hoteli yako mwenyewe na miradi mingine mingi huko mjini au vijijini.

Maisha yana njia nyingi, na unaweza kutumia njia yeyote kufika kwenye hatima yako. Mfano kabla ya kupiga hatua na mageuzi ya kiviwanda, kiteknolojia, pamoja na ulinzi, nchi kama Marekani na China zilikuwa tayari zimejidhatiti kwenye kilimo, idadi kubwa ya watu katika nchi hizi, ikawa sio kipingamizi kabisa katika maendeleo.
Maisha kupitia ajira
Kama ukipata nafasi ya kuajiriwa, kama ilivyo ndoto za Robert, kama tulivyoona mwanzo wa makala hii. Fanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu, udumu na upande viwango pia, sababu wengi waliitamani lakini wakakosa. Na wengine waliipata nafasi hiyo lakini wakaipoteza, maana hata wewe mwenyewe ni shahidi wa mambo haya, kama ulivyoona na kusikia kwa watumishi walegevu serikalini, walivyotumbuliwa enzi za utawala wa Hayati, John Pombe Magufuli, na wanavyoendelelea kutenguliwa siku kwa siku na raisi wa sasa, Samia Suluhu Hassan.
Inawezekana,usipokata tamaa!
Lakini ndugu yangu nakuambia leo, usikate tamaa kwa kupoteza au kukosa ajira au kazi uliyoipenda au uliyokuwa unaitegemea, jifunze kwa watu waliofanikiwa kutokana na kushindwa mara nyingi kama akina Thomas Edison, Nelson Mandela na MacDonald, ijapo sitawazungumzia habari zao katika makala hii. Maisha ni kitendawili kwa wengi, na hivyo haina budi kujifunza kila siku, kutokana mafunzo unayoyapata kwenye maisha. Hii ndio maana ya elimu ni bahari au elimu haina mwisho na ni zaidi ya kalamu na daftari. Katu katu! Msomi usikibali kudharaulika tena, uwe kichwa na si mkia, uwe msaada na si mzigo tena. Wewe ni mtu mwenye kutumainiwa katika jamii na taifa lako, kama maji kwa msafiri jangwani.
 
Upvote 334
zephania5 kaka umeandika asee had nimesoma marambili mbili asante sana kwa makala yako hii daah asante sana nmepata kitu aseee
 
zephania5 kaka umeandika asee had nimesoma marambili mbili asante sana kwa makala yako hii daah asante sana nmepata kitu aseee
Shukrani sana tuko pamoja, nakutakia kila la heri unapoenda kuyazingatia pia kwa pale ulipojifunza
 
Chapisho ni zuri changamoto sisi tunaotumia mobile apps tunashindwa wapigia kura. Sijawai penda jf ya browse.

Je washiriki hamuoni kama jf inawanyima haki yenu ya kupata kura.

Je kutakua na usawa katika ushindi.

Kila la kheri mkuu

Point
 
Shukrani sana, hili limekuwa changamoto kubwa. Watu wanashindwa kutoa maoni au kupiga kura kupitia jamii forum app. Suala hili liangaliwe upya pia. Shukrani kwa kuliona hili na maoni yako pia
 
Kwanza umewahi kujiuliza kuwa! unaenda lima matikiti maji kwenye mabonde ya mito! ili umuuzie nani?? wakati wasomi hawana ajira/hela??............wafanyakazi na wakulima mnategemeana sana!!

Mkulima! utamuuzia mfanya kazi gani wkt hana pesa? .....km siyo kuvutana kwa vihela vichache vilivyopo vya wafanya kazi wenye mishahara mikubwa! hawa si wengi! .....ni wazi utakesha!

Ukiona kazi hakuna maofisini humo, na hela hakuna mitaani, kapange matikiti yako barabarani km hayataoza yoote! hata wapangaji wa nyumba yako hupati! si hawana ajira?

hata kama ukipata basi maatizo kila siku!.....manake ni nini? Tz km nchi hatuuzi vizuri Duniani, au tulikopwa! kipimo kizuri cha wewe kuamua ukalime/fuga ilii uuze nyma na maziwa ni trend ya wafanyakazi nchini!

Hukuandika kwa mapana na marefu, utalima sana, matikiti lkn hakuna wanunuzi(sababu hawana ajira)!... TZ km ilivo ni wewe binafsi na mkulima mmoja mmoja!!

Nchi yeyote inapata hela kwa kuangalia wao km nchi wanauza nini huko soko la Dunia!! pia wanahitaji nini km nchi ili waweze kuishi na kusustain kilimo chao! mfano!

Madawa ya Binadamu/Mifugo na Mazao km pamba.korosho, Mbolea, Pembejeo, Maghala ya kuhifadhia Mazao ya chakula na Biashara, nk! ......haya yoote nayotaja yanahitaji wafanya kazi wasomi,

Na ili Mkulima alime kwa tija, kwakutumia mbolea bora ya kiwandani, iliyotayarishwa na Msomi bora!, na kiwanda cha mbolea kinahitaji wasomi ma- engineer, walinzi, wafanya usafi,

na walinda afya za wafanya kazi, Mafundi mitambo, Mameneja, watafuta masoko nk je watatoka wapi wkt wako shambani..... Yaweza kuwa pia Mkulima huko shambani ataumwa na Nyoka, au akazimia

Lazima akatibiwe na Nurse bora Hospitalini BOra ! na kwa usafiri bora na faster! ili awaishwe hatimaye akazalishe! mazao faster! lkn eti dr yuko shamba! mwee!

kupitia wananchi wao, km weye unaelima matikiti, pamba, chai,korosho, kahawa nk!...jua kuwa hao wasio kuwa na kazi maofisini ndo wangekununulia hayo matikikiti...eti nao sasa wanalima!

yaani wasomi wooote tuwe wakulima duuuuu! hayo ni mawazo Mgando Sana, ndo maana uko ivo!...wapo waliopenda na kusomea kilimo, Jeshini pia na vyuo vyetu vikuu wengine mpaka nje israel hukooo wako Uraiani mfano;

Uvuvi, Ufugaji, umwagiliaji, ardhi, mazingira, misitu, Nyuki, mbolea nk! wapo waliosomea hayo unayoyataka tuyafanye kutokea vyuo vikuu vya kilimo!! vya ndani na nje ya nchi,

Endapo woote au nusu ya watanzania mtakuwa wakulima/wafugaji, bado tatizo litakuwa palepale kwa sababu wewe uliye kimbia taaluma yako, utashindwa kusonga uzuri, walio somea kilimo watafanya vizuri zaidi kimauzo,

kuliko nyie mliokimbia ajira zenu na kufanya kilimo ambacho hamkukisomea!.... hao waache waende huko kunako sekta ya kilimo! sasa weye unataka na Nurse nae kakosa ajira akalime? kweli? wagonjwa wakifa mnalia tena??

ukijikata na jembe shambani atakutibu nani wkt na yeye Nesi yuko shambani kwake analima??...Mawazo km haya hayatufai km watanzania sijui kwa nini wamekuruhusu!

some times hata Nurse akifungua kiduka chake cha dawa ajiajili ... dawa hizo atamuuzia nani? wkt hakuna wafanya kazi??waviwandani na maofisini?? Mkulima nae huku hajauza ujue??

Kifupi hujanishawishi bana weee! naona umepuliza cha A town tu!
 
Kwa nini wasomi kudharaulika, twende pamoja katika makala hii
Wasomi hawadharauliki sema jamii yako ukiwamo wewe mnawaroga sana ajili ya wivu! wadhalilike ....lkn pia km mnawadharau nyie sie hatufanyi hivo usigeneralise!! sema kuna baadhi ya watu mna dharauliana.

Mfano sisi kijijini kwetu, mabwana shamba, waandisi, waalimu Drs wanao kuja hawana ajira, kijiji kimetoa jengo bureee! watibie wanavoweza waajil wanavo jisikia! wajilipe wao..

kama msomi anadharauliwa!! kwani mjinga asiyesoma anaheshimiwa??......unaona raha gani kumiliki kiwanda chenye maelezo na spares za Mzungu bila kusoma shule??,

spare unapataje, mikataba inakuwaje Dunia ya kitapeli hii ..mikutano ya wajasilia mali Duniani ukienda unaongea nini?? wkt hujui kiingereza??

Well! Mabasi 1000 huna Elimu kichwani yatadumu kweli hayo? au unayatengeneza mwenyewe?? hilo haliwezekani! leo hata miaka ijayo!! hata ndagu zimekufa!.....hata uwe la saba ''B'' hutamiliki!

labda useme wana Elimu lkn ya chini kidogo!
 
Elimu ni nzuri sana, na kama nilivyokwisha kusema ni vigumu kwa jamii ya watu wajinga kupiga hatua kimaendeleo ya kiuchumi, kijamii na kiafya. Lakini kwa uhalisia wake wasomi wengi wamekata tamaa, wasomi wengi wana msongo wa mawazo.. hasa ndoto zao zinapoelekea kushindwa. Nikaja na mada hii kuona, ni kwa namna gani msomi anaweza kuleta heshima na mabadiliko yanayotarajiwa kwenye jamii mbalimbali. Hekima ya masikini hudharaulika tu siku zote, na hivyo ni lazima elimu iwe ni yenye tija na si vinginevyo.
Wasomi hawadharauliki sema jamii yako ukiwamo wewe mnawaroga sana ajili ya wivu! wadhalilike ....lkn pia km mnawadharau nyie sie hatufanyi hivo usigeneralise!! sema kuna baadhi ya watu mna dharauliana.

Mfano sisi kijijini kwetu, mabwana shamba, waandisi, waalimu Drs wanao kuja hawana ajira, kijiji kimetoa jengo bureee! watibie wanavoweza waajil wanavo jisikia! wajilipe wao..

kama msomi anadharauliwa!! kwani mjinga asiyesoma anaheshimiwa??......unaona raha gani kumiliki kiwanda chenye maelezo na spares za Mzungu bila kusoma shule??,

spare unapataje, mikataba inakuwaje Dunia ya kitapeli hii ..mikutano ya wajasilia mali Duniani ukienda unaongea nini?? wkt hujui kiingereza??

Well! Mabasi 1000 huna Elimu kichwani yatadumu kweli hayo? au unayatengeneza mwenyewe?? hilo haliwezekani! leo hata miaka ijayo!! hata ndagu zimekufa!.....hata uwe la saba ''B'' hutamiliki!

labda useme wana Elimu lkn ya chini kidogo!
 
Lakini kwa uhalisia wake wasomi wengi wamekata tamaa, wasomi wengi wana msongo wa mawazo.. hasa ndoto zao zinapoelekea kushindwa
WASOMI NIKIWAMO mimi hatuja kata tamaa unalazimisha unavojua weye!! hilo ni tatizo lako binafsi! ...hatuna msongo wa mawazo wewe ndo unao!.......... kuwa msomi haina maana kuwa sipati changa moto ndo ujinga mkubwa wa watu msio soma!

hata millionea ana changa moto nyingi sana kuliko maskini unao wajua,haina maana kuwa amekata tamaa huo ni ujinga wa kuto kujua saikolojia ya maisha!
wengi wana msongo wa mawazo.. hasa ndoto zao zinapoelekea kushindwa
Msemo wa kiswahili una sema nanukuu ''wasi wasi ndo akili'' alipokuwa akisoma shule lazima pia alikuwa na msongo wa mawazo ili afaulu kwa hiyo mawazo ni uhai, mawazo ni maisha/mafanikio!

Usione dege linaelea juu unafurahia lkn kuna watu waliopita walikuwa na Msongo wa mawazo wa kulipaisha hilo dege unalopanda kwa kukenua mimeno hiyo!

Wewe hukufaulu ni kwakuwa hukuwa na msongo wa mawazo kuhusu ufaulu! muache msomi awe nayo! ndo alivyo!....ndo tunataka hayo sisi.....si lazima ndoto yako itimie hata kuikaribia tu inatosha!!..

.Kamwe Binadamu yeyote mwenye akili hataishiwa ndoto kuhusu maisha never! labda uwe kilaza km weye! leo tuko hivi tulivo sababu ya ndoto za watu ambazo hazikuwahi kwisha...ukishindwa weye engine wanakuja!

Tunaishi Duniani humu ni ndoto za watu usitudanganye!! nachelea kusema kweli weye hukusoma! Bakhresa mpaka sasa bado ana ndoto zake japo ni tajiri!

ukinunua basi moja una ndoto ya kusheheni mabasi stand yoote ndo wenzako walivyo!....bado utataka na dege la mizigo zaidi ya moja!
anaweza kuleta heshima na mabadiliko yanayotarajiwa kwenye jamii mbalimbali
Heshima ya nchi siyo mpaka iletwe na msomi aliye soma madarasani tuu! Bali wenye moyo na uelewa wa kile nchi/Dunia yetu inahitaji kwa wakati maalumu!..Elimu siyo drsani tu! au nimalize chuo kikuu tu!

Hapo ndo msiosoma mnasumbua tutawaelimisha mpaka lini?? Elimu ya kujitegemea/siasa ni kilimo/sansi kim/Geograph nk ni kisomo cha Elimu ya Msingi! ni Elimu.ikusaidie hiyo!

Tatizo la watu msiosoma mnaangalia ya chuo kikuu tuuu basi ndo ujinga mlionao! lkn ya Msingi/sec. siyo Elimu! then mnajidharau eti mnadharaulika yaani nyie ni mizigo hasaaa!
Hekima ya masikini hudharaulika tu siku zote, na hivyo ni lazima elimu iwe ni yenye tija na si vinginevyo.
Hakuna mtu anaye dharau maskini mtu asiye mjua, huo ni uongo umeamua kutudanganya! bali huyo anaye jiona maskini alisha jidharau mwenyewe! kutokana na matendo yake ya giza na dhambi zake!

sasa km mtu amejidharau mwenyewe tokana na matendo yake...... unataka sisi tumfanyeje humu JF??..... aende akatubu kwa Mola wake huko msikitini inatuhusu nini sisi???
 
WASOMI NIKIWAMO mimi hatuja kata tamaa unalazimisha unavojua weye!! hilo ni tatizo lako binafsi! ...hatuna msongo wa mawazo wewe ndo unao!.......... kuwa msomi haina maana kuwa sipati changa moto ndo ujinga mkubwa wa watu msio soma!

hata millionea ana changa moto nyingi sana kuliko maskini unao wajua,haina maana kuwa amekata tamaa huo ni ujinga wa kuto kujua saikolojia ya maisha!

Msemo wa kiswahili una sema nanukuu ''wasi wasi ndo akili'' alipokuwa akisoma shule lazima pia alikuwa na msongo wa mawazo ili afaulu kwa hiyo mawazo ni uhai, mawazo ni maisha/mafanikio!

Usione dege linaelea juu unafurahia lkn kuna watu waliopita walikuwa na Msongo wa mawazo wa kulipaisha hilo dege unalopanda kwa kukenua mimeno hiyo!

Wewe hukufaulu ni kwakuwa hukuwa na msongo wa mawazo kuhusu ufaulu! muache msomi awe nayo! ndo alivyo!....ndo tunataka hayo sisi.....si lazima ndoto yako itimie hata kuikaribia tu inatosha!!..

.Kamwe Binadamu yeyote mwenye akili hataishiwa ndoto kuhusu maisha never! labda uwe kilaza km weye! leo tuko hivi tulivo sababu ya ndoto za watu ambazo hazikuwahi kwisha...ukishindwa weye engine wanakuja!

Tunaishi Duniani humu ni ndoto za watu usitudanganye!! nachelea kusema kweli weye hukusoma! Bakhresa mpaka sasa bado ana ndoto zake japo ni tajiri!

ukinunua basi moja una ndoto ya kusheheni mabasi stand yoote ndo wenzako walivyo!....bado utataka na dege la mizigo zaidi ya moja!

Heshima ya nchi siyo mpaka iletwe na msomi aliye soma madarasani tuu! Bali wenye moyo na uelewa wa kile nchi/Dunia yetu inahitaji kwa wakati maalumu!..Elimu siyo drsani tu! au nimalize chuo kikuu tu!

Hapo ndo msiosoma mnasumbua tutawaelimisha mpaka lini?? Elimu ya kujitegemea/siasa ni kilimo/sansi kim/Geograph nk ni kisomo cha Elimu ya Msingi! ni Elimu.ikusaidie hiyo!

Tatizo la watu msiosoma mnaangalia ya chuo kikuu tuuu basi ndo ujinga mlionao! lkn ya Msingi/sec. siyo Elimu! then mnajidharau eti mnadharaulika yaani nyie ni mizigo hasaaa!

Hakuna mtu anaye dharau maskini mtu asiye mjua, huo ni uongo umeamua kutudanganya! bali huyo anaye jiona maskini alisha jidharau mwenyewe! kutokana na matendo yake ya giza na dhambi zake!

sasa km mtu amejidharau mwenyewe tokana na matendo yake...... unataka sisi tumfanyeje humu JF??..... aende akatubu kwa Mola wake huko msikitini inatuhusu nini sisi???
Hata mimi ni mwanachuo ndugu yangu, usije fikiria sikusoma. Mwenye nyumba siku zote ndiye anayejua inapovuja, elimu ina mambo mengi mazuri, lakini penye mapungufu ni lazima pafanyiwe kazi. Ukitaka kufanikiwa ni lazima uangalie changamoto zilizopo katika eneo ulilopo ukizitatua utafanikiwa. Hatuwezi kuenenda kama vipofu, ni lazima tusome tukiwa na tahadhari. Na mtu siku zote huonywa anapoenda na si anaporudi, hutakuwa umemsaidia kwa lolote.
 
Unayosema ni sahihi, kwa sababu umeangalia upande mmoja tu wa sarafu. Ni lazima pia tuangalie katika upande mwingine juu ya elimu yetu. Kama imekusaidia wewe na watu wa jamii yako, ni jambo la heri, na hongera pia. Lakini pa toka uangalie maisha ya watanzania wengi waliosoma, wanavyoshindwa kuisaidia jamii yao na hata wao wenyewe. Hapa suluhisho likipatikana, tutakuwa tumetua mzigo huu.
 
Hata mimi ni mwanachuo ndugu yangu, usije fikiria sikusoma. Mwenye nyumba siku zote ndiye anayejua inapovuja, elimu ina mambo mengi mazuri, lakini penye mapungufu ni lazima pafanyiwe kazi. Ukitaka kufanikiwa ni lazima uangalie changamoto zilizopo katika eneo ulilopo ukizitatua utafanikiwa. Hatuwezi kuenenda kama vipofu, ni lazima tusome tukiwa na tahadhari. Na mtu siku zote huonywa anapoenda na si anaporudi, hutakuwa umemsaidia kwa lolote.
Ndugu yangu wee!! km mwanachuo na unawaza hivi?? kuna shida mahali? afadhali kabisa usingeenda kumalizia watu wenye hari za kusoma nafasi zao! ....asa ulienda ili u fail maisha ukachanga nyikiwe??

Mapungufu,upofu, na changamoto zako unavo chukulia si kwa wengine ili wafanikiwe!........ni makosa kudhania ivo!.. kamwe usimuonye mpambanaji Muache aende afe au apone ndo maana ya vita....

Hata akirudi kuanza moja!3,4,5,6,78,..... bado ni mafanikio makubwa sana,........ narudia tena sijakosea yule anaye rudi kuanza moja amefanikiwa zaidi kuliko yule ambaye hakuthubutu kabisa nirudie tena??......... na si dhambi!........
 
Back
Top Bottom