SoC02 Kwanini mafanikio kupitia elimu yanaonekana kama mvua inyeshayo jangwani?

Stories of Change - 2022 Competition

zephania5

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2022
Posts
232
Reaction score
807
Kwa miaka mingi kabla na hata baada ya uhuru, watanzania wengi na hata watu wengine duniani kote, wamekuwa na imani ya kuwa, elimu ndio ufunguo wa maisha. Lakini katika uhalisia wake elimu na mafanikio katika maisha vimekuwa vitu viwili tofauti kabisa. Ni kama mtu aliyeko kusini akiitafuta kaskazini. Kumekuwa na hoja na mijada mbalimbali hata kule bungeni ya kuwa, Watoro wengi ndio wenye mafanikio, kutokana na maoni na utafiti uliofanyika. Hali hii hufanya wasomi kudharaulika au kujidharau wao wenyewe, vile vile hali kama hii inasababisha ionekane ya kuwa, mafanikio katika elimu, ni kama mvua inyeshayo jangwani, kutokea kwake ni nadra na kwa kubahatisha sana.

Kwa nini wasomi kudharaulika, twende pamoja katika makala hii
'' Kaka Robert amka! ni muda wa shamba, leo umechelewa sana kujiandaa, baba na mama wametangulia tayari. Tangu saa 11 alfajiri, wanasubiri uwapelekee mbolea ya samadi, wakakuelekeze namna ya kupanda viazi na maharage. Nadhani atakuwa amekasirika sana, amechoka kukusubiri, si unamjua baba hana mchezo na kazi za shamba...,''.

Hakika haya yatakuwa ni maneno yenye kukereketa kwa upande wa Robert, mhitimu wa shahada ya uhandisi kwenye chuo kikuu cha Dar es Salaam, tawi la Mbeya (MUST). Ni mwaka wa pili sasa tangu atume maombi ya kazi, katika shirika la umeme Tanzania(TANESCO). Miongoni mwa watu laki mbili waliotuma maombi ya kazi, na wakati huo nafasi mia mbili tu zikiwa zinahitajika.

Matumaini ya Robert yatafikiwa tu, kama endapo maombi yake ya kazi yatakubaliwa, kwa kudra za Mwenyezi Mungu. La sivyo ndoto zitabaki kuwa ndoto tu, siku zote. Kijana wa kitanzania toka familia duni, inayotegemea zizi lenye ng'ombe na mbuzi wachache, waliomalizika kwa kulipa karo na michango ya shule na maisha yenye kutegemea mvua za masika, ndipo chakula kipatikane shambani. Kwa mtazamo wa haraka Robert anaonekana kuwa mzigo badala ya kuwa msaada, elimu na ujuzi wake tangu shule ya awali hadi chuo kikuu, inashindwa kubadilisha hali yake mwenyewe, pamoja na hali ya nyumbani, kwa kipindi chote alichokaa nyumbani.
Nikimaliza kusoma nitafanya nini?
Mwalimu mmoja katika chuo kikuu cha Dodoma, aliwahi kuwauliza wanafunzi waliokuwa wamejiunga na mwaka wa kwanza wa masomo akisema '' Mmekuja kusoma uuguzi kwa lengo gani?''. Wapo waliosema '' Tumekuja kusoma hapa kwa ajili ya kusaidia watu'', wengine wakasema '' Tumekuja kuwa wauguzi kwa sababu ya wito''.

Lakini kwa kweli wengi wao walikuwa wamewaahidi wazazi wao, ndugu zao, jamaa zao na hata wapenzi wao, kuishi maisha yaliyo bora zaidi, mara baada ya kuhitimu elimu ya juu. Kabla ya kumsaidia mwingine hakikisha kwanza usalama wako, na hivyo elimu ya kweli ni ile inayoanza kuleta mabadiliko kiafya, kiakili, kijamii na kiuchumi, kwa yule anayeipata kabla ya kuleta mabadiliko kwa wengine pia. Wasomi wengi wapo mtaani wakiwa hawana matumaini wala dira ya maisha ya leo wala ya baadae.

Viatu vimechakaa na vumbi, kutwa kiguu na njia kugonga milango ya ofisi, popote pale walipotangaza nafasi za kazi, hata kama si ile iliyokuwa ni malengo yake. Wengine wapo sekondari au chuo kikuu, bado wanajiuliza ya kuwa '' Nikimaliza kusoma, nitafanya kazi gani''. Ndipo sasa unakuja ule msemo wa waswahili '' Shule
ilitudai akili, kitaa kinatudai mafanikio''.

Maisha yakikuchagulia ngoma, na wewe chagua namna ya kuyacheza ndugu yangu.
Huu ndio mpango mzima!
Umeshawahi kufikiria kumiliki kampuni au shirika lako mwenyewe, na wewe uisaidie serikali kutoa ajira, kwa wasiokuwa na ajira. Ni jambo gumu kusubiri serikali itoe ajira kwa wananchi wote, hakuna serikali kama hiyo duniani. Wapo wengi waliofeli masomo, na kushindwa kuendelea, lakini leo wanamiliki shule ama vyuo. Unaweza kuona hilo haliwezekani ama jambo gumu, maana kazi rahisi kwako ni kubeti, kuwekekeza kwenye makampuni ya mtandaoni yasiyokuwa na ofisi wala mikataba yeyote, na kuishia kupoteza pesa kila siku. Utakuja kuzinduka, ni wewe peke yako hadi leo unaeendelea kuishi kwenu, huku ukiendelea kusifia mapishi ya mama yako pale jikoni. Heshima haiji bure ndugu, acha matumizi mabaya ya muda na akili.

Maisha ni lazima yaendelee. Muda mwingine si rahisi kutambua kusudi lako hasa la kuishi, ni kweli kuwa elimu ndio ufunguo wa maisha, maana ni vigumu sana jamii yenye watu wajinga kupiga hatua katika maendeleo yakiwa ni ya kiafya, kijamii, kiuchumi au kidiplomasia, lakini si lazima kuweka matumaini yote katika fani uliyoisomea ikiwa ni kwamba uliipenda au ulifuata upepo kama bendera, ili kuleta mabadiliko mazuri na yanayohitajika kwenye maisha yako au kwenye jamii uliyopo.

Mwalimu Nyerere aliacha kazi ya ualimu akajikita kwenye siasa kupitia chama cha TANU, ili kuleta uhuru kwa Tanganyika, ambayo leo ni Tanzania. Leo mimi na wewe, tuna uhuru wa kujieleza kama hivi, tuna uhuru wa kwenda popote duniani, tuna uhuru wa kufanya shughuli zozote kwa ajili ya maendeleo yetu wenyewe. Lakini ajabu kubwa ni kwamba wengi wetu hapa ni watumwa wa kifikra.

Kuna watu huzikalia fursa wao wenyewe, na kisha kuanza kuangaza huku na kule wakitafuta fursa na wala wasizione, huo ni upofu wa akili kweli. Wengine hukosa hamasa au msukumo wa ndani, ili kuzifanyia kazi fursa walizoziona au kupatiwa, uoga na aibu ya kushindwa huwamaliza wengi, wasomi na kwa wasio wasomi. Elimu na ujuzi wako visipotee bure, jaribu kutumia uwezo wako wote, vipawa vyako vyote pamoja na nafasi zote ulizojaliwa na Mwenyezi Mungu, ikiwa ni afya, nguvu na akili. Pia rasilimali au mtaji wowote ulio nao, waweza kukufikisha popote pale unapotaka kufika na kuwa mtu bora zaidi.

Utajiri wanaoukimbia wasomi wengi
Wewe kijana mwenzangu, uliyekimbilia mjini kutafuta maisha baada ya kumaliza masomo yako, huku ukishinda njaa kila siku, rudi kijijini kwenu, maana kupendeza sio kushiba. Utajiri umeuacha kijijini kwenu, umeacha ardhi nzuri kwenye mashamba, pamoja na mabonde yenye maji ya kutosha, kwa ajili ya kilimo cha mazao mbalimbali kama maboga, tikitimaji, machungwa, mchicha, miwa, maparachichi ama ufugaji wa nyuki, samaki,ng'ombe. Ukipata kipato cha kutosha unaweza kumiliki zahanati yako mwenyewe, shule yako, hoteli yako mwenyewe na miradi mingine mingi huko mjini au vijijini.

Maisha yana njia nyingi, na unaweza kutumia njia yeyote kufika kwenye hatima yako. Mfano kabla ya kupiga hatua na mageuzi ya kiviwanda, kiteknolojia, pamoja na ulinzi, nchi kama Marekani na China zilikuwa tayari zimejidhatiti kwenye kilimo, idadi kubwa ya watu katika nchi hizi, ikawa sio kipingamizi kabisa katika maendeleo.
Maisha kupitia ajira
Kama ukipata nafasi ya kuajiriwa, kama ilivyo ndoto za Robert, kama tulivyoona mwanzo wa makala hii. Fanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu, udumu na upande viwango pia, sababu wengi waliitamani lakini wakakosa. Na wengine waliipata nafasi hiyo lakini wakaipoteza, maana hata wewe mwenyewe ni shahidi wa mambo haya, kama ulivyoona na kusikia kwa watumishi walegevu serikalini, walivyotumbuliwa enzi za utawala wa Hayati, John Pombe Magufuli, na wanavyoendelelea kutenguliwa siku kwa siku na raisi wa sasa, Samia Suluhu Hassan.
Inawezekana,usipokata tamaa!
Lakini ndugu yangu nakuambia leo, usikate tamaa kwa kupoteza au kukosa ajira au kazi uliyoipenda au uliyokuwa unaitegemea, jifunze kwa watu waliofanikiwa kutokana na kushindwa mara nyingi kama akina Thomas Edison, Nelson Mandela na MacDonald, ijapo sitawazungumzia habari zao katika makala hii. Maisha ni kitendawili kwa wengi, na hivyo haina budi kujifunza kila siku, kutokana mafunzo unayoyapata kwenye maisha. Hii ndio maana ya elimu ni bahari au elimu haina mwisho na ni zaidi ya kalamu na daftari. Katu katu! Msomi usikibali kudharaulika tena, uwe kichwa na si mkia, uwe msaada na si mzigo tena. Wewe ni mtu mwenye kutumainiwa katika jamii na taifa lako, kama maji kwa msafiri jangwani.
 
Upvote 334
Lakini pa toka uangalie maisha ya watanzania wengi waliosoma, wanavyoshindwa kuisaidia jamii yao na hata wao wenyewe. Hapa suluhisho likipatikana, tutakuwa tumetua mzigo huu.
Hakuna Mtanzania Msomi mwenye akili timamu aliye shindwa kujisaidia, nakataa, nani huyo?? mtaje! .......pengine Tatizo lako unaangalia wasomi waleee;

walevi, wauza madawa ya kulevya. wanywa Gongo, na wale walio rogwa na koo zao ajili ya wivu, Mizimu, waliokimbia uganga wa koo!,vitukuu vya wachawi!

make wale wanaambiwa kabisa ukimaliza kusoma uje ukamate tungulri number 21, kuwanga na kuroga ni jadi yetu! sasa kataa uone moto!....ndo hao unao wasemea!

na kwa mujibu wa Biblia uchawi upo, mfano; Musa mtumishi wa Mungu alirogwa!! sasa kam Musa aliyeongea na Mungu live alirogwa, wewe msomi mtanzania wa kawaida kwa nini usirogwe?

hapo usilinganishe waliorogwa na watu wenye akili timamu, nikupe mfano tu umesomea labda Bee keeping! utashindwaje kulina na kuuza asali yako binafsi wakati ukisubili ajira??

Mwalimu fungua drs la Tuition uani kwenu!! ..ukisubiri ajira!.........Business admin...toa ushauri kwa wafanya bishara kwa malipo kidogo wa draftie hata Business plan zao! wkt unasubiri ajira shida iko wapi?

Umesoma chuo gani ambacho hawakukupa life skills........... Maisha na kazi?? tamka! ..... niwaseme sasa hivi! ukisoma chuo wanakupa na mbinu za kujiajili! wkt ukisubiri ajira never hukwami!
 
maisha ya watanzania wengi waliosoma, wanavyoshindwa kuisaidia jamii yao na hata wao wenyewe.
Nakupa mfano: shule ya Msingi na Ufundi Kibumaye S.L.P 172, Tarime Mara Tanzania, Hii shule mnafundishwa ufundi wa aina mbali mbali! na kilimo

yaani wana mashamba mazuri ya mazao mbali mbali pia Bustani za mboga na Maua, ukisoma hii shule hutashindwa kuchonga kisturi kizuri ukauza na ukapata hela! nzuri mnoo!

kuna watu mpaka dakika hii wanatafuta fenicha kwa nini usiwachongee uwapelekee!.....well!! kwa nini uslime mchicha, tena Mama ntilie wakaja wao wenyewe kununua??.....

Mfano palee chuo cha Madaktari wasaidizi Mtwara COTC wale wana chuo wana vibustani vidogo vidogo vya michicha sasa wafanya biahsra wanakuja wenyewee kununua mboga za jumla kutoka sokoni mjini!

nani aliwafundisha hao wana chuo hicho kilimo?? .......ni wazi walitoka na akili hizo shuleni zao za misingi km hiyo hapo juu!.......ukiona unakosa ajira umerogwa tu! au laana ya kutukana watu wazima!

kwa sababu kwa nini wewe Msomi usilime Bustani rahisi tu! kisomi na ukaishi vizuri mnoo! unazo elimu lukuki kichwani humo tena nzuri zaidi wanalima hata kwenye makopo! makrate ya Bia /soda!

sasa weye unatuletea habari za watu wenye laana/walevi/wavivu,nk! Manake ni wazi hawa ndiyo unao onana nao kwenye Mazingira yanayo kuzunguka mkuu na wewe unaonja kidogo ile kitu! sema tu!!??

Km mie muongo uli waona wapi? make ni ngumu kumjua mtu aliyesoma na asiye soma kwa kumuangalia tu usoni! au weye ndo unawaroga sababu unawajua fika walivo soma!

wasomi hawajapigwa mihuri! usoni wal mgongoni nyie ndo wachawi wenyewe make unajua kila aliye soma na ambaye hakusoma hiyo kazi ya sensa unaifanya saa ngapi na kwamalipo yapi wakt uko busy?

Dr umesomea let say Muhimbili, ukaenda kuishi Kamunyonge bila kazi, sawa sasa nani atakujua kuwa weye ni DR huna kaziiii??...jibu ni mchawi tu! ndo atajua!
 
Usije kuwa kipofu wa akili pia, kushindwa kuona wimbi la watu, wakifanya vitu nje ya malengo yao. Hata biblia ikasema '' watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, na si elimu''. Kama ni elimu watu wanapata, hao walevi na wavivu wanatoka wapi, ni kukosa maarifa ya kumudu maisha. Maisha yana mambo mengi ya kukufunza ambayo pengine, hautakaa ufundishwe popote. Hata walimu wenyewe mishahara haiwatoshi, kuendesha maisha yao, hasa ukiangalia familia zetu za kiafrika, ukoo unamuangalia mtu mmoja, mwenye uelekeo wa maisha. Mshahara unatoka ukiwa na makato ya mikopo uliyokopeshwa na serikali. Elimu ya ujamaa na kujitegemea imesahauliwa kwa namna fulani..
 
Kila mwaka watu huhitimu elimu ya sekondari, huhitimu elimu ya chuo kikuu. Na wengine hujiunga kila mwaka, unafikiri hawa wote huenda wapi? Ni jambo la kawaida leo mtu amesoma udaktari ama ualimu, akiendesha bodaboda, kuuza mitumba, na kazi nyingine kama hizo. Ishi na watu vizuri utajua mengi kama haya, na wala si uchawi ama uganga. Elimu ya ufundi inatolewa, lakini si kwa kiwango kinachomfanya mtu awe proffesional, bali afaulu tu mitihani. Mfano kuna hizi shule zetu za ufundi kama, moshi technical, tanga tech au iyunga, wahitimu wengi wanamaliza akiwa hawana ujuzi kamili wa kutengeneza hata redio, televisheni, kujenga nyumba, kutengeneza magari nakadhalika. Ni lazima tujiandae vizuri kwa maisha kamili, umetoa mawazo mazuri, watu kutumia fursa walizo nazo. Jitahidi pia kukaa na watu wa matabaka mbalimbali katika jamii mbalimbali pia, ili ujue changamoto wanazokutana nazo.
 
Kwa miaka mingi kabla na hata baada ya uhuru, watanzania wengi na hata watu wengine duniani kote, wamekuwa na imani ya kuwa, elimu ndio ufunguo wa maisha. Lakini katika uhalisia wake elimu na mafanikio katika maisha vimekuwa vitu viwili tofauti kabisa. Ni kama mtu aliyeko kusini akiitafuta kaskazini. Kumekuwa na hoja na mijada mbalimbali hata kule bungeni ya kuwa, Watoro wengi ndio wenye mafanikio, kutokana na maoni na utafiti uliofanyika. Hali hii hufanya wasomi kudharaulika au kujidharau wao wenyewe, vile vile hali kama hii inasababisha ionekane ya kuwa, mafanikio katika elimu, ni kama mvua inyeshayo jangwani, kutokea kwake ni nadra na kwa kubahatisha sana.

Kwa nini wasomi kudharaulika, twende pamoja katika makala hii
'' Kaka Robert amka! ni muda wa shamba, leo umechelewa sana kujiandaa, baba na mama wametangulia tayari. Tangu saa 11 alfajiri, wanasubiri uwapelekee mbolea ya samadi, wakakuelekeze namna ya kupanda viazi na maharage. Nadhani atakuwa amekasirika sana, amechoka kukusubiri, si unamjua baba hana mchezo na kazi za shamba...,''.

Hakika haya yatakuwa ni maneno yenye kukereketa kwa upande wa Robert, mhitimu wa shahada ya uhandisi kwenye chuo kikuu cha Dar es Salaam, tawi la Mbeya (MUST). Ni mwaka wa pili sasa tangu atume maombi ya kazi, katika shirika la umeme Tanzania(TANESCO). Miongoni mwa watu laki mbili waliotuma maombi ya kazi, na wakati huo nafasi mia mbili tu zikiwa zinahitajika.

Matumaini ya Robert yatafikiwa tu, kama endapo maombi yake ya kazi yatakubaliwa, kwa kudra za Mwenyezi Mungu. La sivyo ndoto zitabaki kuwa ndoto tu, siku zote. Kijana wa kitanzania toka familia duni, inayotegemea zizi lenye ng'ombe na mbuzi wachache, waliomalizika kwa kulipa karo na michango ya shule na maisha yenye kutegemea mvua za masika, ndipo chakula kipatikane shambani. Kwa mtazamo wa haraka Robert anaonekana kuwa mzigo badala ya kuwa msaada, elimu na ujuzi wake tangu shule ya awali hadi chuo kikuu, inashindwa kubadilisha hali yake mwenyewe, pamoja na hali ya nyumbani, kwa kipindi chote alichokaa nyumbani.
Nikimaliza kusoma nitafanya nini?
Mwalimu mmoja katika chuo kikuu cha Dodoma, aliwahi kuwauliza wanafunzi waliokuwa wamejiunga na mwaka wa kwanza wa masomo akisema '' Mmekuja kusoma uuguzi kwa lengo gani?''. Wapo waliosema '' Tumekuja kusoma hapa kwa ajili ya kusaidia watu'', wengine wakasema '' Tumekuja kuwa wauguzi kwa sababu ya wito''.

Lakini kwa kweli wengi wao walikuwa wamewaahidi wazazi wao, ndugu zao, jamaa zao na hata wapenzi wao, kuishi maisha yaliyo bora zaidi, mara baada ya kuhitimu elimu ya juu. Kabla ya kumsaidia mwingine hakikisha kwanza usalama wako, na hivyo elimu ya kweli ni ile inayoanza kuleta mabadiliko kiafya, kiakili, kijamii na kiuchumi, kwa yule anayeipata kabla ya kuleta mabadiliko kwa wengine pia. Wasomi wengi wapo mtaani wakiwa hawana matumaini wala dira ya maisha ya leo wala ya baadae.

Viatu vimechakaa na vumbi, kutwa kiguu na njia kugonga milango ya ofisi, popote pale walipotangaza nafasi za kazi, hata kama si ile iliyokuwa ni malengo yake. Wengine wapo sekondari au chuo kikuu, bado wanajiuliza ya kuwa '' Nikimaliza kusoma, nitafanya kazi gani''. Ndipo sasa unakuja ule msemo wa waswahili '' Shule
ilitudai akili, kitaa kinatudai mafanikio''.

Maisha yakikuchagulia ngoma, na wewe chagua namna ya kuyacheza ndugu yangu.
Huu ndio mpango mzima!
Umeshawahi kufikiria kumiliki kampuni au shirika lako mwenyewe, na wewe uisaidie serikali kutoa ajira, kwa wasiokuwa na ajira. Ni jambo gumu kusubiri serikali itoe ajira kwa wananchi wote, hakuna serikali kama hiyo duniani. Wapo wengi waliofeli masomo, na kushindwa kuendelea, lakini leo wanamiliki shule ama vyuo. Unaweza kuona hilo haliwezekani ama jambo gumu, maana kazi rahisi kwako ni kubeti, kuwekekeza kwenye makampuni ya mtandaoni yasiyokuwa na ofisi wala mikataba yeyote, na kuishia kupoteza pesa kila siku. Utakuja kuzinduka, ni wewe peke yako hadi leo unaeendelea kuishi kwenu, huku ukiendelea kusifia mapishi ya mama yako pale jikoni. Heshima haiji bure ndugu, acha matumizi mabaya ya muda na akili.

Maisha ni lazima yaendelee. Muda mwingine si rahisi kutambua kusudi lako hasa la kuishi, ni kweli kuwa elimu ndio ufunguo wa maisha, maana ni vigumu sana jamii yenye watu wajinga kupiga hatua katika maendeleo yakiwa ni ya kiafya, kijamii, kiuchumi au kidiplomasia, lakini si lazima kuweka matumaini yote katika fani uliyoisomea ikiwa ni kwamba uliipenda au ulifuata upepo kama bendera, ili kuleta mabadiliko mazuri na yanayohitajika kwenye maisha yako au kwenye jamii uliyopo.

Mwalimu Nyerere aliacha kazi ya ualimu akajikita kwenye siasa kupitia chama cha TANU, ili kuleta uhuru kwa Tanganyika, ambayo leo ni Tanzania. Leo mimi na wewe, tuna uhuru wa kujieleza kama hivi, tuna uhuru wa kwenda popote duniani, tuna uhuru wa kufanya shughuli zozote kwa ajili ya maendeleo yetu wenyewe. Lakini ajabu kubwa ni kwamba wengi wetu hapa ni watumwa wa kifikra.

Kuna watu huzikalia fursa wao wenyewe, na kisha kuanza kuangaza huku na kule wakitafuta fursa na wala wasizione, huo ni upofu wa akili kweli. Wengine hukosa hamasa au msukumo wa ndani, ili kuzifanyia kazi fursa walizoziona au kupatiwa, uoga na aibu ya kushindwa huwamaliza wengi, wasomi na kwa wasio wasomi. Elimu na ujuzi wako visipotee bure, jaribu kutumia uwezo wako wote, vipawa vyako vyote pamoja na nafasi zote ulizojaliwa na Mwenyezi Mungu, ikiwa ni afya, nguvu na akili. Pia rasilimali au mtaji wowote ulio nao, waweza kukufikisha popote pale unapotaka kufika na kuwa mtu bora zaidi.

Utajiri wanaoukimbia wasomi wengi
Wewe kijana mwenzangu, uliyekimbilia mjini kutafuta maisha baada ya kumaliza masomo yako, huku ukishinda njaa kila siku, rudi kijijini kwenu, maana kupendeza sio kushiba. Utajiri umeuacha kijijini kwenu, umeacha ardhi nzuri kwenye mashamba, pamoja na mabonde yenye maji ya kutosha, kwa ajili ya kilimo cha mazao mbalimbali kama maboga, tikitimaji, machungwa, mchicha, miwa, maparachichi ama ufugaji wa nyuki, samaki,ng'ombe. Ukipata kipato cha kutosha unaweza kumiliki zahanati yako mwenyewe, shule yako, hoteli yako mwenyewe na miradi mingine mingi huko mjini au vijijini.

Maisha yana njia nyingi, na unaweza kutumia njia yeyote kufika kwenye hatima yako. Mfano kabla ya kupiga hatua na mageuzi ya kiviwanda, kiteknolojia, pamoja na ulinzi, nchi kama Marekani na China zilikuwa tayari zimejidhatiti kwenye kilimo, idadi kubwa ya watu katika nchi hizi, ikawa sio kipingamizi kabisa katika maendeleo.
Maisha kupitia ajira
Kama ukipata nafasi ya kuajiriwa, kama ilivyo ndoto za Robert, kama tulivyoona mwanzo wa makala hii. Fanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu, udumu na upande viwango pia, sababu wengi waliitamani lakini wakakosa. Na wengine waliipata nafasi hiyo lakini wakaipoteza, maana hata wewe mwenyewe ni shahidi wa mambo haya, kama ulivyoona na kusikia kwa watumishi walegevu serikalini, walivyotumbuliwa enzi za utawala wa Hayati, John Pombe Magufuli, na wanavyoendelelea kutenguliwa siku kwa siku na raisi wa sasa, Samia Suluhu Hassan.
Inawezekana,usipokata tamaa!
Lakini ndugu yangu nakuambia leo, usikate tamaa kwa kupoteza au kukosa ajira au kazi uliyoipenda au uliyokuwa unaitegemea, jifunze kwa watu waliofanikiwa kutokana na kushindwa mara nyingi kama akina Thomas Edison, Nelson Mandela na MacDonald, ijapo sitawazungumzia habari zao katika makala hii. Maisha ni kitendawili kwa wengi, na hivyo haina budi kujifunza kila siku, kutokana mafunzo unayoyapata kwenye maisha. Hii ndio maana ya elimu ni bahari au elimu haina mwisho na ni zaidi ya kalamu na daftari. Katu katu! Msomi usikibali kudharaulika tena, uwe kichwa na si mkia, uwe msaada na si mzigo tena. Wewe ni mtu mwenye kutumainiwa katika jamii na taifa lako, kama maji kwa msafiri jangwani.
kabisa kila kitu duniani kinawezekana kinawezekana kama utaeka juhudi na nia
 
Usije kuwa kipofu wa akili pia, kushindwa kuona wimbi la watu, wakifanya vitu nje ya malengo yao. Hata biblia ikasema '' watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, na si elimu''. Kama ni elimu watu wanapata, hao walevi na wavivu wanatoka wapi, ni kukosa maarifa ya kumudu maisha. Maisha yana mambo mengi ya kukufunza ambayo pengine, hautakaa ufundishwe popote. Hata walimu wenyewe mishahara haiwatoshi, kuendesha maisha yao, hasa ukiangalia familia zetu za kiafrika, ukoo unamuangalia mtu mmoja, mwenye uelekeo wa maisha. Mshahara unatoka ukiwa na makato ya mikopo uliyokopeshwa na serikali. Elimu ya ujamaa na kujitegemea imesahauliwa kwa namna fulani..
Usipoteze Dira!!! Maarifa na Elimu ni kitu kilekile!! hujui! ....uvivu na ulevi ni Multi secterial na hulka ya Mtu binafsi nI makosa kuuliza walevi, wavivu, wanatoka wapi!!......Kenyataa mdogo ni Rais mlevi kupindukia mpaka sasa!!

Mishahara ya Waalimu wetu! inawatosha sana, umeongopa sijakosea sana tu, acha kukariri!! ...km haiwatoshi mbona hawalalamiki? kazi wanafanya! kuna watu wanasoma ualimu mpaka sasa??

pesa na matumizi ni akili ya Mtu husika tu! baasi!

hata mtu mmoja tu tukikupa Bajeti yote ya Marekani km ni mbumbu hutoki kamwe!!......Hakuna Mwafrica/Mtanzania mpumbavu ivo wa kuangaliwa na ukoo Mzima? ili iweje?..

km weye unafanya ivo basi jua kabisaaa una tatizo la msingi, wategemezi hawana shida bali wewe unae waendekeza wake hapo ndo unafaa kuchapwa hamsa ishirini ili akili ikukae sawa!

Sasa km mshahara una makato, ajili ya Mkopo uliokopeshwa kwa hiari yako!! ulitaka wakopeshaji wakate nini?? Makalio au!! .......bana wee hiyo Elimu yako hiyo inatia ukakasi....uliwahi sikia vyeti fake!
 
Nakupa mfano: shule ya Msingi na Ufundi Kibumaye S.L.P 172, Tarime Mara Tanzania, Hii shule mnafundishwa ufundi wa aina mbali mbali! na kilimo

yaani wana mashamba mazuri ya mazao mbali mbali pia Bustani za mboga na Maua, ukisoma hii shule hutashindwa kuchonga kisturi kizuri ukauza na ukapata hela! nzuri mnoo!

kuna watu mpaka dakika hii wanatafuta fenicha kwa nini usiwachongee uwapelekee!.....well!! kwa nini uslime mchicha, tena Mama ntilie wakaja wao wenyewe kununua??.....

Mfano palee chuo cha Madaktari wasaidizi Mtwara COTC wale wana chuo wana vibustani vidogo vidogo vya michicha sasa wafanya biahsra wanakuja wenyewee kununua mboga za jumla kutoka sokoni mjini!

nani aliwafundisha hao wana chuo hicho kilimo?? .......ni wazi walitoka na akili hizo shuleni zao za misingi km hiyo hapo juu!.......ukiona unakosa ajira umerogwa tu! au laana ya kutukana watu wazima!

kwa sababu kwa nini wewe Msomi usilime Bustani rahisi tu! kisomi na ukaishi vizuri mnoo! unazo elimu lukuki kichwani humo tena nzuri zaidi wanalima hata kwenye makopo! makrate ya Bia /soda!

sasa weye unatuletea habari za watu wenye laana/walevi/wavivu,nk! Manake ni wazi hawa ndiyo unao onana nao kwenye Mazingira yanayo kuzunguka mkuu na wewe unaonja kidogo ile kitu! sema tu!!??

Km mie muongo uli waona wapi? make ni ngumu kumjua mtu aliyesoma na asiye soma kwa kumuangalia tu usoni! au weye ndo unawaroga sababu unawajua fika walivo soma!

wasomi hawajapigwa mihuri! usoni wal mgongoni nyie ndo wachawi wenyewe make unajua kila aliye soma na ambaye hakusoma hiyo kazi ya sensa unaifanya saa ngapi na kwamalipo yapi wakt uko busy?

Dr umesomea let say Muhimbili, ukaenda kuishi Kamunyonge bila kazi, sawa sasa nani atakujua kuwa weye ni DR huna kaziiii??...jibu ni mchawi tu! ndo atajua!
Unaakili nyingi.. nipunguzie basi [emoji23]

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Kila mwaka watu huhitimu elimu ya sekondari, huhitimu elimu ya chuo kikuu. Na wengine hujiunga kila mwaka, unafikiri hawa wote huenda wapi?
Makakazini kwao ndo maana huwaoni mitaani!
Elimu ya ufundi inatolewa, lakini si kwa kiwango kinachomfanya mtu awe proffesional, bali afaulu tu mitihani. Mfano kuna hizi shule zetu za ufundi kama, moshi technical, tanga tech au iyunga, wahitimu wengi wanamaliza akiwa hawana ujuzi kamili wa kutengeneza hata redio, televisheni, kujenga nyumba, kutengeneza magari nakadhalika.
Sasa km mtu alikuwa mtoro!mvivu unategemea nini?? mie nimesoma shule ya msingi na ufundi, lkn mambo madogo madogo/makubwa kwenye gari yangu/nyumbani kwangu, nafanya mwenyewe,

mfano painting, ujenzi wa nyumba jamani kuna ugumu hapo kweli kwa msomi? labda uwe mvivu tu, nina uwezo wakujua gari hii nzuri au kimeo kwa muungurumo tuu!

ukiona mtu ameshindwa kutumia aliyo somea na kasomea ufundi,, alirukia fani kwa kufuata mkumbo tu! aliharibu nafasi za watu kuumbe alifaa kuwa dereva wa malori!

Ni jambo la kawaida leo mtu amesoma udaktari ama ualimu, akiendesha bodaboda, kuuza mitumba, na kazi nyingine kama hizo.
Kwani daktari,Mwalimu, akiwa na Boda boda, ili kujiongezea kipato kuna shida gani?? akitoka kazini anaruka na abiria kuelekea kwake kwanza ana faida pikipiki yake haiendi bure anapata hela ya mafuta kesho yake,

akifuga kuku/, nguruwe / akilima Bustani ya mboga nyumbani kwake, fuga nyuki akala na kuuza , ni dhambi kwani?? tena huyu ndo mzuri atapata sana soko kwa sababu.

anapeleka kwa wafanya kazi wenzake/college mate wake watamuungisha kuwauzia!..pia kwa kuwa wanamjua watakuwa hawana hofu ya kuibiwa, wala kuporwa,

hao hao ulio soma nao wanakuamini wanaweza hata kumtuma Mboga sokoni upeleke home, cement, fenicha bila wao kuwepo kumsimamia! kusoma na watu tu ni soko kubwa sana!

hayo ya ufugaji/kilimo amesoma tangia s/msingi! na sec. (unajua topic ya Agromechanics weye? Horticulture je, na Floriculture!! nielezee make naweza kuwa naongea na kilaza flani ivi)

endapo ukizijua hizo kwanini usifanye na ukapata hela ya ziada? una ujuzi nayo!.....kwanza yana faida kubwa wewe unaona boda boda ni kosa??...wewe? hizi gari/pikipiki tunapanda ni za wafanyakazi wewe? wa wapi?

kwani unataka aandike hii pikipiki mie mwalimu? ndo maana nina shaka na Elimu yako!
 
Usipoteze Dira!!! Maarifa na Elimu ni kitu kilekile!! hujui! ....uvivu na ulevi ni Multi secterial na hulka ya Mtu binafsi nI makosa kuuliza walevi, wavivu, wanatoka wapi!!......Kenyataa mdogo ni Rais mlevi kupindukia mpaka sasa!!

Mishahara ya Waalimu wetu! inawatosha sana, umeongopa sijakosea sana tu, acha kukariri!! ...km haiwatoshi mbona hawalalamiki? kazi wanafanya! kuna watu wanasoma ualimu mpaka sasa??

pesa na matumizi ni akili ya Mtu husika tu! baasi!

hata mtu mmoja tu tukikupa Bajeti yote ya Marekani km ni mbumbu hutoki kamwe!!......Hakuna Mwafrica/Mtanzania mpumbavu ivo wa kuangaliwa na ukoo Mzima? ili iweje?..

km weye unafanya ivo basi jua kabisaaa una tatizo la msingi, wategemezi hawana shida bali wewe unae waendekeza wake hapo ndo unafaa kuchapwa hamsa ishirini ili akili ikukae sawa!

Sasa km mshahara una makato, ajili ya Mkopo uliokopeshwa kwa hiari yako!! ulitaka wakopeshaji wakate nini?? Makalio au!! .......bana wee hiyo Elimu yako hiyo inatia ukakasi....uliwahi sikia vyeti fake!

Sasa km mtu alikuwa mtoro!mvivu unategemea nini?? mie nimesoma shule ya msingi na ufundi, lkn mambo madogo madogo/makubwa kwenye gari yangu/nyumbani kwangu, nafanya mwenyewe,

mfano painting, ujenzi wa nyumba jamani kuna ugumu hapo kweli kwa msomi? labda uwe mvivu tu, nina uwezo wakujua gari hii nzuri au kimeo kwa muungurumo tuu!

Usipoteze Dira!!! Maarifa na Elimu ni kitu kilekile!! hujui! ....uvivu na ulevi ni Multi secterial na hulka ya Mtu binafsi nI makosa kuuliza walevi, wavivu, wanatoka wapi!!......Kenyataa mdogo ni Rais mlevi kupindukia mpaka sasa!!
Si wote wenye elimu wana maarifa, na hiki ndicho kinachosumbua wengi. Elimu au fani yeyote ina ethics, ukiwa muuguzi, daktari, mwanasheria ni lazima uwe na maadili na kufuata miongozo yote inayotakiwa, bila kujali hulka au tabia yako uliyo nayo au uliyozaliwa nayo. Hapo unataka kuniambia kuwa kuna ukiukwaji ama elimu imeshindwa kumsaidia!?
 
Mishahara mingi, ni kwa ajili ya kujikimu na kuendesha maisha ya kila siku. Nilitolea mfano kwa walimu, lakini ni wafanyakazi wengi tu. Namshukuru raisi Samia Suluhu kwa kuliona hili na kuamua kuwaongeza wafanyakazi, nimeshuhudia waajiriwa wengi wakijenga umri ukiwa umeenda sana, kwenye kiinua mgongo. Ni mambo yanayoonekana, hapa hapa kwetu Tanzania na wala si ya kusimuliwa ama kuota.
 
ukiona mtu ameshindwa kutumia aliyo somea na kasomea ufundi,, alirukia fani kwa kufuata mkumbo tu! aliharibu nafasi za watu kuumbe alifaa kuwa dereva wa malori!
Unaongea mengi sana, lakini unarudi pale pale. Moja ya matatizo yanayofanya mafanikio kupitia elimu yaonekane kuwa kama mvua inyeshayo jangwani. Ungesoma vizuri ukaelewa usingekuwa na doubt nyingi
 
Mishahara mingi, ni kwa ajili ya kujikimu na kuendesha maisha ya kila siku. Nilitolea mfano kwa walimu, lakini ni wafanyakazi wengi tu. Namshukuru raisi Samia Suluhu kwa kuliona hili na kuamua kuwaongeza wafanyakazi, nimeshuhudia waajiriwa wengi wakijenga umri ukiwa umeenda sana, kwenye kiinua mgongo. Ni mambo yanayoonekana, hapa hapa kwetu Tanzania na wala si ya kusimuliwa ama kuota.
Kuwaongezea wafanyakazi mishahara
 
Kwani daktari,Mwalimu, akiwa na Boda boda, ili kujiongezea kipato kuna shida gani?? akitoka kazini anaruka na abiria kuelekea kwake kwanza ana faida pikipiki yake haiendi bure anapata hela ya mafuta kesho yake,
Ni heri kama angekuwa daktari au mwalimu, anayejiongezea kipato kwa sababu gharama za maisha zinapanda kila siku, lakini mshahara wake upo pale pale au hadi ifikapo mwisho wa mwezi. Lakini wapo wengi wanaofanya hivyo bila kupenda, ni kwa sababu ndoto zao zimefeli, na maisha ni lazima yaendelee. Hata ukisema utangaze ajira leo, watakutafuta popote ulipo..
 
Sasa km mtu alikuwa mtoro!mvivu unategemea nini?? mie nimesoma shule ya msingi na ufundi, lkn mambo madogo madogo/makubwa kwenye gari yangu/nyumbani kwangu, nafanya mwenyewe,

mfano painting, ujenzi wa nyumba jamani kuna ugumu hapo kweli kwa msomi? labda uwe mvivu tu, nina uwezo wakujua gari hii
Hiyo ni moja tu ya sababu, lakini kwa kweli hizi shule zetu za ufundi zilikuwa zimesahauliwa kwa muda mrefu, mafunzo mengi ni ya nadharia na si vitendo. Karakana za kufundishia pamoja na vifaa zimekuwa changamoto. Nipende kuishukuru awamu ya tano kwa kuliona hili, kwa namna yake imetoa mchango mkubwa, kwa shule za vipaji na ufundi kwa kuboresha miundimbinu na mazingira rafiki ya kijifunza. Lakini changamoto nyingine ni kuwapata walimu wenye ujuzi pamoja na uzoefu wa haya masomo, kama electrical drafting, technical drawing, plumbing, motor vehicle na mengineyo. Nadharia imekuwa ni nyingi kuliko vitendo, na kusababisha wahitimu kushindwa kujiamini katika fani zao, na kusababisha ndoto kubadilika badilika, katika vipindi tofauti vya maisha.
 
Mishahara ya Waalimu wetu! inawatosha sana, umeongopa sijakosea sana tu, acha kukariri!! ...km haiwatoshi mbona hawalalamiki? kazi wanafanya! kuna watu wanasoma ualimu mpaka sasa??
Kwa kuliona hili raisi akapandisha mishahara kwa wafanyakazi serikalini.
 
Makakazini kwao ndo maana huwaoni mitaani!
Si kweli kama watanzania wote wenye kusoma wapo kwenye kazi za maofisini ama za kutokuonekana kama wachawi ama wanajimu wanaoenda anga za mbali. Nikakuambia mwanzo uishi na jamii ya watu wanaokuzunguka vizuri, upate kujua changamoto zinazoikumba nchi yetu na ulimwengu kwa ujumla.
 
Shukrani kwa kuendelea kuelewana vizuri., katika suala hili
 
Ndugu yangu wee!! km mwanachuo na unawaza hivi?? kuna shida mahali? afadhali kabisa usingeenda kumalizia watu wenye hari za kusoma nafasi zao! ....asa ulienda ili u fail maisha ukachanga nyikiwe??

Mapungufu,upofu, na changamoto zako unavo chukulia si kwa wengine ili wafanikiwe!........ni makosa kudhania ivo!.. kamwe usimuonye mpambanaji Muache aende afe au apone ndo maana ya vita....
Elimu isiyoweza kuleta mabadiliko kwenye jamii si elimu. Hauwezi kuwa na taa ukaificha chini ya uvungu, isiweze kumulika. Taifa na jamii linahitaji watu wenye upeo. Tumejifunza mengi kutoka kwa watu wenye mtazamo chanya, wenye hamu ya kuona mabadiliko kwenye jamii za watu kama akina Maslow, lennin, Aristotloe, Plato, Mwalimu Nyerere na wengine wengi kwenye jamii mbalimbali. Hata nyakati za zamani, walikuwepo manabii, wafalme, wenye hekima, wagunduzi mbalimbali. Kwa mawazo yao ndio maana dunia ipo hivi leo. La sivyo tungebaki namna ile ile
 
Hakuna mtu anaye dharau maskini mtu asiye mjua, huo ni uongo umeamua kutudanganya! bali huyo anaye jiona maskini alisha jidharau mwenyewe! kutokana na matendo yake ya giza na dhambi zake!

sasa km mtu amejidharau mwenyewe tokana na matendo yake...... unataka sisi tumfanyeje humu JF??..... aende akatubu kwa Mola wake huko msikitini inatuhusu nini sisi???
Umasikini sio dhambi, haya matabaka yamekuwepo tangu zamani, na yataendelea kuwepo. Kama ukipata muda soma pia theories of development. Hata Sulemani alikuwa ni mwenye hekima lakini akazidishiwa na utajiri pia.. ndio maana yeye mwenyewe akasema hekima ya masikini hudharauliwa.
 
Back
Top Bottom