Kwanini mafunzo ya mgambo yasiwe "compulsory" kwa wanafunzi wote waliohitimu kidato cha sita ambao hawakubahatika kuchaguliwa kujiunga na mafunzo JKT?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Kwanini mafunzo ya mgambo yasiwe "compulsory" kwa wanafunzi wote waliohitimu kidato cha sita ambao hawakuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya J.K.T?




Nimeamua kuuliza hivi kwa maana kwamba, inafahamika vema na watanzania wengi ya kuwa lengo la kuwapeleka hawa wadogo wetu JKT ni kuwajengea uzalendo, ukakamavu pamoja na mentality ya kujitegemea.

Ninafahamu fika ya kuwa serikali haiwezi kupeleka graduates wote wa kidato cha sita kwenda mafunzo ya JKT kutokana na ufinyu wa budget, lakini inapaswa kukumbuka pia kwa kutokufanya hivyo inakuwa imetengeneza kundi lingine kuwa la vijana waliokosa fursa adhimu ya kupata mafunzo ya ukakamavu na uzalendo huko vyuoni na mtaani.



Kuna mtoto mmoja wa mama yangu mdogo yeye hakubahatika kupata nafasi ya kuchaguliwa kwenda huko sasa kwa namna anavyogombana na baba yake kila siku ilikuwa mpaka kero.

Kijana mdogo wa kiume yeye akilala usiku kuja kuamka kesho yake basi ni saa nne au tano asubuhi. Mtoto hajui kufagia uwanja wala kufuta madirisha ya nyumbani kwao mpaka huwa ninajiuliza sasa watoto kama hao ambao ndio tunategemea watakuja kuwa taifa la kesho ndio wanakuwa lelemama kiasi hiki sijui Tanzania ya mwaka 2050 itakuwa na watu wazima wa aina gani?

ANGALIZO: Mimi Infantry Soldier sio askari jeshi wala mtumishi wa ofisi yoyote ya serikali bali ni raia mwema ninayeipenda sana Tanzania. Hili jina nilijpa tu kutokana na changamoto kadhaa nzito nilizowahi kuzipitia katika maisha yangu. Hakika umasikini ni m-baya.



USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Maoni ya mdau
=====

 
Mkuu wazo lako zuri ila Kwa dunia ya sasa tunaitaji vijana wenye technical skills ili waweze kujiajiri na kuzalisha sio ukakamavu tena dunia unaenda mbio saizi hakuna kulima na jembe la ng'ombe au kusukuma mizigo kuna Conveyor belt .

Ilo Jambo la ukakamavu lirudishwe shule za msingi na sekondari Kwa kuweka program za michezo walau mara 2 Kwa wiki na mazoezi ya viungo kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma kulikuwa na mbio za mchakamchaka,Umiseta na Umitashunta.

Sasa tupo kwenye zama za science na technology serikali inabidi ikubali vijana wanaohitimu au walio mitaani wapate technical skills ili waweze kukitegemea na kujiajiri. Mfano huo muda wa kukimbia mgambo kisha urudi kitaa ni bora watu wakusanywe wilayani kisha waitwe wauzaji wa Maroli ya kichina ya Faw,Howo,Beiben,Dayun,Foton na Shacman Kwa muda wa mwezi watoe training kwa watu wanaojifunza ufundi upepo,brake system, umeme, mechanical na rangi hapo kila kijana akitoka anatoka na skills ambayo itamsaidia vivyo hivyo kwenye simu,pikipiki na boti.
 
Kwa dunia ya sasa tunaitaji vijana wenye technical skills ili waweze kujiajiri na kuzalisha sio ukakamavu tena dunia unaenda mbio saizi hakuna kulima na jembe la ng'ombe au kusukuma mizigo kuna Conveyor belt .
Ndio maana baada ya kutoka mafunzo ya ukakamavu sasa wanaenda chuoni kupata mafunzo hayo ambayo wewe unayaita kuwa ni "technical skills"

Hata nchi zilizoendelea kama Israel bado wanathamini sana mafunzo ya ukakamavu wa mwili na akili kwa vijana wao...
 
Naunga mkono hoja.

Dunia ya sasa haiendeshwi kwa njia primitive kama zamani.

Achilia mbali mitaani hata hao maaskari wa nchi za wenzetu vitani hawapigani kwa kutumia miguvu kama zamani ni akili tu na teknolojia.
Mtu yupo Korea analipua marekani
 
Je haya mafunzo yana tija yoyote kwa vijana wetu?
Mimi nadhani hawa form six kwanza mda wanaokaa mtaani ni mdogo sababu wanamaliza mwezi wa 5 na wa 10 wanaenda chuo.

Naona kama form four ndo wangechukuliwa na kuundiwa kozi fupi fupi za ujuzi hasa kompyuta au ufundi au ujenzi (veta) maana wanazagaa sana mtaani na itasaidia vijana kupata ujuzi tu.

Kiuhalisia huku kwenye mafunzo ya mgambo na jkt ni sehemu ambayo hawa mabinti wanachakazwa kwelikweli kama umewahi pitia nadhani unaelewa hilo.
 
Mkuu tusijilinganishe na hao Israel au Korea Sisi mahitaji yetu na yao ni tofauti.

Vijana wanaenda chuo kikuu kupata elimu ambayo haitomuwezesha kujiajiri na sio rafiki Kwa mazingira yetu kujiajiri.Ninachomaanisha ni vijana wowote wale ambao wataenda chuo na wasioenda wapate technical skills za kujitegemea.

Chuo unaenda kusoma uchumi,it,utalii ila ukirudi mtaani utakutana na hali tofauti. Sisi shughuli zetu kubwa ni kilimo,uvuvi,utalii na madini.

Unadhani vijana wakipewa elimu ya kurekebisha mitambo ya kilimo na madini ,uvuvi kama mashine za boti, kusuka nyavu na kutengeneza zana za uvuvi athari chanya kubwa itayotokea itaonekana na tutakuwa tumesogea sana mbele.Chuo kuna mfumo wa mzungu na sisi ni waafrika tuna matatizo yetu unadhani nani atatatua kama sio sisi wenyewe.
 
Mimi binafsi natamani kama VETA wangeanzisha program ya kufundisha kozi fupi za namna ya kutengeneza out board injini za boti,marekebisho ya fiber boat, usukaji wa zana za uvuvi hii program ikifanyika mikoa yenye maziwa,mabwawa,mito mikubwa na bahari ingesaidia sana kuwapa skills vijana wengi na wangejiajiri.

Mpaka sasa Tanzania hakuna chuo au taasisi yoyote inayofundisha ufundi wa injini ndogo za petrol za boti. Mafundi wengi wanatumia uzoefu na wengine wamiliki wanarekebisha wenyewe.
 
Ilo Jambo la ukakamavu lirudishwe shule za msingi na sekondari Kwa kuweka program za michezo walau mara 2 Kwa wiki na mazoezi ya viungo kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma kulikuwa na mbio za mchakamchaka,Umiseta na Umitashunta.
Kwa hapa upo sahihi na ninakuunga mkono kwamba ukakamavu na uzalendo uanze kufundishwa kuanzia shule za msingi mpaka form six na kuendelea juu...
 
Huko JKT wangewasaidia vijana wanaokwenda kujitolea kwa kuwapa mafunzo ya ufundi stadi Kwa kuwatawanya kwenye miradi mikubwa kama ya reli, bwawa la umeme, madaraja na barabara wajifunze ufundi umeme, bomba, rangi, magari na ujenzi kisha wakimaliza inabidi hao wakandarasi wawatengenezee Certificate of service ili hata wakimaliza mikataba yao wanaporudi nyumbani wawe na ujuzi wa ziada ambao unaenda na wakati na anaweza jiajiri.

Ukiangalia miaka ya karibuni vijana wengi waliorudishwa baada ya mikataba kuisha wamerudi mtaani na wengi hawana fani wanapambana kusaka ajira kwenye kampuni za ulinzi na kazi ndogo ndogo.

Mkuu wa JKT anaweza akawabana hata wale wachina au wajerumani ambao hushirikiana na jeshi letu wangefundisha vijana technology ya mitambo ya barabara, kilimo, madini na magari wakirudi mtaani wajue wapi wanaanzia.
 
Sasa tupo kwenye zama za science na technology serikali inabidi ikubali vijana wanaohitimu au walio mitaani wapate technical skills ili waweze kukitegemea na kujiajiri.
Mbona serikali inafanya hivi kupitia VETA pamoja na technical schools zingine. Mkuu, jaribu kutembelea shule pamoja na vyuo vya ufundi vya serikali uone jinsi wanavyojitahidi kutoa elimu na ujuzi kwa vijana wetu.

Ingawa kuna mapungufu kadha wa kadha lazima wanajitahidi sana kwa kweli...
 
Hii ni idea nzuri sana ya kufanywa na wakuu wa Wilaya pamoja na viongozi wengine kwa ngazi zao lakini sio mbadala wa kupeleka vijana wetu JKT pamoja na mgambo.

Sasa kama mtu hana ukakamavu atawezaje kufanya kazi za ufundi wa mikono kama vile rangi, welding pamoja na automobile mechanics?
 
Hili waxo bovu sana mkuu, litaleta makundi miongoni mwa vijana mara hawa mgambo mara hawa jkt bora waache kama hawawezi kuliko kuunda makundi
Kwanini sasa hakuna makundi kuwa hawa ni JKT na wale hawajaenda mafunzo yoyote ya ukakamavu?
 
Nakuunga mkono asilimia mia mbili. Zama zimebadilika,skills ulizotaja ni perfect kabisa kuwasaidia vijana wa zama hizi na sio magwaride na ukakamavu
 
Kumpeleka mtoto JKT ni kumwandaa kuwa fukara maisha yake yote ,kwasababu

1.Hatakuwa na akili za ubunifu tena zaidi ya kusubiri command tu
2.Unaanda watu ambao hawana mawazo mbadala zaidi ya kutumia nguvu tuu
3.Litakuwa liCcm la kudumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…