Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,892
- 16,476
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.
Ndugu zangu watanzania eti;
Kwanini mafunzo ya mgambo yasiwe "compulsory" kwa wanafunzi wote waliohitimu kidato cha sita ambao hawakuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya J.K.T?
www.jamiiforums.com
Nimeamua kuuliza hivi kwa maana kwamba, inafahamika vema na watanzania wengi ya kuwa lengo la kuwapeleka hawa wadogo wetu JKT ni kuwajengea uzalendo, ukakamavu pamoja na mentality ya kujitegemea.
Ninafahamu fika ya kuwa serikali haiwezi kupeleka graduates wote wa kidato cha sita kwenda mafunzo ya JKT kutokana na ufinyu wa budget, lakini inapaswa kukumbuka pia kwa kutokufanya hivyo inakuwa imetengeneza kundi lingine kuwa la vijana waliokosa fursa adhimu ya kupata mafunzo ya ukakamavu na uzalendo huko vyuoni na mtaani.
Kuna mtoto mmoja wa mama yangu mdogo yeye hakubahatika kupata nafasi ya kuchaguliwa kwenda huko sasa kwa namna anavyogombana na baba yake kila siku ilikuwa mpaka kero.
Kijana mdogo wa kiume yeye akilala usiku kuja kuamka kesho yake basi ni saa nne au tano asubuhi. Mtoto hajui kufagia uwanja wala kufuta madirisha ya nyumbani kwao mpaka huwa ninajiuliza sasa watoto kama hao ambao ndio tunategemea watakuja kuwa taifa la kesho ndio wanakuwa lelemama kiasi hiki sijui Tanzania ya mwaka 2050 itakuwa na watu wazima wa aina gani?
ANGALIZO: Mimi Infantry Soldier sio askari jeshi wala mtumishi wa ofisi yoyote ya serikali bali ni raia mwema ninayeipenda sana Tanzania. Hili jina nilijpa tu kutokana na changamoto kadhaa nzito nilizowahi kuzipitia katika maisha yangu. Hakika umasikini ni m-baya.
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Maoni ya mdau
=====
Ndugu zangu watanzania eti;
Kwanini mafunzo ya mgambo yasiwe "compulsory" kwa wanafunzi wote waliohitimu kidato cha sita ambao hawakuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya J.K.T?
JKT yatangaza majina ya vijana waliohitimu Kidato cha Sita 2020 wanaotakiwa kujiunga na JKT kwa Mujibu wa Sheria
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2020, kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria. Sanjari na uchaguzi huo, JKT limewapangia makambi watakayo kwenda kupatiwa mafunzo na wanatakiwa...
Nimeamua kuuliza hivi kwa maana kwamba, inafahamika vema na watanzania wengi ya kuwa lengo la kuwapeleka hawa wadogo wetu JKT ni kuwajengea uzalendo, ukakamavu pamoja na mentality ya kujitegemea.
Ninafahamu fika ya kuwa serikali haiwezi kupeleka graduates wote wa kidato cha sita kwenda mafunzo ya JKT kutokana na ufinyu wa budget, lakini inapaswa kukumbuka pia kwa kutokufanya hivyo inakuwa imetengeneza kundi lingine kuwa la vijana waliokosa fursa adhimu ya kupata mafunzo ya ukakamavu na uzalendo huko vyuoni na mtaani.
Kuna mtoto mmoja wa mama yangu mdogo yeye hakubahatika kupata nafasi ya kuchaguliwa kwenda huko sasa kwa namna anavyogombana na baba yake kila siku ilikuwa mpaka kero.
Kijana mdogo wa kiume yeye akilala usiku kuja kuamka kesho yake basi ni saa nne au tano asubuhi. Mtoto hajui kufagia uwanja wala kufuta madirisha ya nyumbani kwao mpaka huwa ninajiuliza sasa watoto kama hao ambao ndio tunategemea watakuja kuwa taifa la kesho ndio wanakuwa lelemama kiasi hiki sijui Tanzania ya mwaka 2050 itakuwa na watu wazima wa aina gani?
ANGALIZO: Mimi Infantry Soldier sio askari jeshi wala mtumishi wa ofisi yoyote ya serikali bali ni raia mwema ninayeipenda sana Tanzania. Hili jina nilijpa tu kutokana na changamoto kadhaa nzito nilizowahi kuzipitia katika maisha yangu. Hakika umasikini ni m-baya.
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Maoni ya mdau
=====
Kwa msisitizo tu ni kwamba kijana yoyote ambae ni raia wa kuzaliwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ambae amemaliza kidato cha sita anapaswa kujiunga JKT kwa mujibu wa sheria.
Hiyo haijalishi umemaliza Mzizima, Al Haramain au Feza boys au Girls.
Iwe ni kwa mujibu kwa sheria ya JMT.
Na hata iwe kwa sababu mbalimbali kijana huyo hakuweza kujiunga huo basi iwe ni deni na atumukie kwa muda utakaofaa.
Nchi kama Israeli, Korea Kusini, Kazakhstan na zingine wanafanya hivyo.
Hii yaondoa matatizo kama kutokuwa mzalendo, uzembe wa kufikiri na ushawishi wa kujiunga na makundi kama yale ya kule Kibiti.
Enzi zetu sisi kaka na dada zenu tulikuwa tukikutana pamoja JKT na bila kujali tajiri au maskini au mtoto wa mkulima wote tulinyoa nywele na kuwa na madenge sawa.
JKT ndipo ndipo misingi ya umoja, amani na upendo baina ya wana wa nchi inapojengwa.
Wengine wanaobadilika kama tunaowaona leo hii na wamepitia JKT ni kwa kudanganywa na vijienti vya hapa na pale.