Kwa nijuavyo hata wakati wa JK, upinzani hawakukubalina na mambo mengi tu.
Tofauti ya wakati uliopita na wakati wa JPM, wakati wa JPM mitandao ya kijamii ilikuwa na nguvu zaidi na wafuasi wengi.
Waliofuatilia siasa za wakati wa awamu ya nne, rais JK, alisemwa sana kwa ubaya. Na alitukanwa hadi hadharani; mkwere wa watu alichukulia sawa tu. Na wakati mwingine aliwajibu kwa mafumbo.
Ila msukuma hakuweza kukubaliana na ukosoaji wa hadharani au popote pale. Hii ndio tofauti hata kwa awamu hii ya sasa.
Kwenye siasa, viongozi wengi hawako tayari kukosolewa hata kama wanakosea!
Tena binafsi naona bora hata JPM, alijidhihirisha wazi kuliko hao wengine wanafanya kwa siri.
Ama sivyo, 'mama' asingehangaika na suala la job ikiwa hakukuwa na ukweli wowote! Na inawezakana hata sasa anachukiwa sana tu, ila muda haujafika.
Ni maoni tu!