Kwanini Magufuli aliwaogopa sana Nape na January Makamba?

Kwanini Magufuli aliwaogopa sana Nape na January Makamba?

MAGUFULI NI UTITIRI ALIYEMBEBA TEMBO KWA SPIDI YA CHEETAH.

Kama NECTA wangepewa kusahihisha posts za JF na kutoa matokeo ya wanaostahili kubaki JF nadhani wangebaki watano tu (mimi nikiwemo) na Mello angelazimika kufunga JF maana hasingeweza kutumia rasilimali fedha kuendesha jamvi la watu watano tu.

Watanzania tutafute kuijuwa vizuri historia ya nchi ili tubalance story zetu tunapoandika. Huo ndiyo uandishi unavyotakiwa kuwa.

Kila kukicha propaganda zinashamiri juu ya Ben Saanane, Tundu, Roma Mkatoliki.

Kimsingi, ifahamike kwamba sipingani na yaliyowatokea maana ni dhahir shahir yamewatokea, ila kwa nia gani na kwa mikono ya nani siyo hoja yangu.

Kinachonishangaza ni kuwa hatutendi haki kwa Magufuli kumuhusisha na hao watu.

Ifahamike kwamba Tz haikuanza enzi ya Magufuli 2015, Tz ilikuwepo tangu Tanganyika na matukio yalikuwepo tena mengi kuliko enzi ya Magufuli maana enzi zile dunia ilikuwa kwy vita ya itikadi (nipige nikupige).
Diplomasia ilipoteza uwezo wa kusimamia amani ya dunia, na silaha za maangamizi ya umma ndiyo zikachukuwa nafasi ya diplomasia. Zikaundwa kambi za kujihami za Unipolar na Bipolar.

Ili kutenda haki inabidi unayepost u balance story. Tujuwe binadamu ana hulka kwamba akisikiliza habari moja tuu 24/7/30/365... inamkifu na habari hiyo inapungua thamani, uzito na umuhimu kwenye masikio, ubongo na mtima wa mlaji wa habari hiyo.

Kila kukicha ni Ben Saanane, Tundu, Roma Mkatoliki kama vile hawa pekee ndiyo wamefikwa na madhila hayo kwenye nchi.

Mbona hamumtaji Chacha Wangwe? Mbona hamumtaji Akwilina Akwilini?

Kila siku ni Ben Saanane, Tundu, Roma Mkatoliki.

Ina maana hao wana nguvu za kikatiba na kiitifaki kuliko wafuatao?

1. Rais Sheikh Abeid Karume?

2. Rais Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi?

3. Sheikh Thabit Kombo Katibu Mkuu wa ASP?

4. Abdulla Sadala Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi?

Namba 3 na 4 walijeruhiwa kwy mauaji (uhaini) ya Rais Karume Kisiwandui 7 Apr 1972.

Ina maana Roma ana nguvu kuliko hao marais?

Hayo mambo Magufuli amezaliwa ameyakuta, ameingia kwenye urais ameyakuta, hajaondoka nayo ameyaacha pia.

Kama hujui kudurusu historia utaandika zombie tu. Binadamu akichoshwa na habari moja tuu hutamani kusikia ya kale ili ajuwe alikotoka, alipo na aendako (anatamani kurejelea ya kale ambayo ni dhahabu).

Hivi kwanini hamshikii bango kwa kuandika juu ya wafuatao au hamjui historia ambayo ina kawaida ya kuweka kumbukumbu?

1. Bibi Titi Mohammed alifia Afrika Kusini.

2. Abdullah Kassim Hanga Waziri Mkuu wa Znz aliyedumu kwa miezi 3 na nusu tu 12 Jan 1964 hadi 27 Apr 1964.

3. Abdulaziz Twaha Znz.

4. Fr. Joseph Anselmo Mwagambwa Znz. Alishambuliwa kwa tindikali.

5. Prof. Abdulrahman Babu. Mkimbizi.

6. Oscar Kambona. Mkimbizi.

7. Kassanga Tumbo. Mkimbizi.

8. Hussein Shekilango Waziri wa Maliasili. Ndege ndogo aliyopanda ilianguka Monduli milimani. Habari za kuvumishwa zinadai ndege ilishambuliwa na majangili. Shekilango aliacha rekodi ya ushupavu kwy wizara hiyo ngumu duniani.

9. Edward Sokoine Waziri Mkuu wa JMT. Msafara wake uliingiliwa na kugharimu uhai wake. Operesheni yake dhidi ya wahujumu uchumi ilimjengea kutopendwa na waovu kama Magufuli alivyokuwa hapendwi na waovu. Nilishuhudia wafanyabiashara wakimwaga ela kwa tipa (binua mchanga) mtoni kwenda ziwani na wavuvi wakaacha kuvua samaki wakawa wanavua ela tu, vijiji vikatapakaa ela. Nyerere ikambidi akabili anguko la uchumi kwa ela kuzagaa kwa kubadili noti kuleta mpya na walioenda na mifuko ya ela kuzibadili benki waliswekwa ndani. Mbona Magufuli tuu ndiyo nongwa eti kanyang'anya watu ela! Kwanza Sokoine hana legacy ya kuonekana kwa macho ukimlinganisha na Magufuli.

10. Lt. Gen. Imran Kombe.

12. Stan Katabalo.

13. Saed Kubenea.

14. Adam Mwaibabile (aliwekwa kizuizini bila kupelekwa Kortini na kupigwa marufuku mkoa wa Ruvuma kwa ripoti zake za uchunguzi dhidi ya wakubwa hadi hapo nguvu za kalamu za umma wa wanahabari zilipomtoa kizuizini na kufikishwa Kortini na kuhukumiwa kihalali kwa kosa la kuhujumu usalama wa taifa kufuatia kujipatia nyaraka za siri zilizoandikwa kumzuia kupewa vibali vya kazi zake. Alikufa 1 Feb 2007 kwa matatizo ya figo).

15. Daudi Mwangosi.

16. Dr. Stephen Ulimboka.

Ijulikane kwamba Saanane, Tundu na Roma siyo mashujaa wa nchi hii hadi wasujudiwe kihivyo.

Mtu kuwa shujaa wa taifa kuna vigezo vinavyozingatia maisha yake chanya na hasi. Umma haujui upande hasi wa Saanane, Tundu na Roma ili uone kama wanatosha kuwa mashujaa.

Tundu mwenyewe hilo analijuwa vizuri ndiyo maana alipambana Bungeni kuondoa jina la Dr. Lawrence Gama kwy orodha ya mashujaa kwy Makumbusho ya taifa Songea.

Abdallah Said Fundikira alikuwa mpinzani lakini kwa nguvu ya katiba, sheria, mila na desturi alitambuliwa kama shujaa wa taifa kwa wadhifa wake wa Chifu wa Unyanyembe. Mfumo huo huo alioishi kuupinga ndiyo huo haukuwa na choyo ya kumtambua kama shujaa wa taifa.

Tundu hili analijuwa, sasa kama alimpinga Dr. Gama kutambuliwa kama shujaa mbona hampiganii Roma Mkatoliki et al watambuliwe kama mashujaa?

Magufuli mwenyewe hakuwa mpigania uhuru, ameingia kwenye orodha ya mashujaa wa taifa kwa nguvu ya katiba iliyompa wadhifa wa kiongozi wa nchi (rais). Sasa Tundu, Saanane na Roma walipigania uhuru?

Kumsemasema Magufuli kila siku ili achukiwe na umma wote ni kumpa umaarufu bila kujuwa. Hiyo ni kumsujudia ambako ni sawa na kumuabudu na ghadhabu ya MUNGU haitawaepuka maana MUNGU ni mwenye wivu.

Hatuwezi kufungua ukurasa mpya tukamwacha Magufuli akapumzika? Hatuna habari zingine za kuandika? Kweli nimeamini Magufuli hafutiki kwa kemikali yoyote duniani. Kama mmenasa kwa Magufuli anayewakera mjuwe watu wenye vinasaba kama vyake wataendelea kuzaliwa hivyo mjiandae kukereka milele yote.

Maswali ya msingi tunayopaswa kujiuliza ni haya:-

1. Mauti ya Magufuli kama yanapaswa kufurahiwa YAMELETA MABADILIKO GANI NAFUU KWENYE NCHI? Watz wote 100% wanafaidika na kifo chake?

2. Uhai wa Magufuli kama unapaswa kufurahiwa ULILETA MABADILIKO GANI NAFUU KWENYE NCHI?

Tusipokuwa makini na kumsemasema Magufuli ipo hatari inatunyemelea ya kumfanya Idol (kama ambavyo Nyerere amefanywa Mtakatifu na Wakatoliki) na watazuka watu watatumia uhuru wa katiba wa kuabudu utakacho kujenga sanamu kubwa ya Magufuli na kwenda kuiabudu kwa kuiomba iwape majibu ya matatizo ambayo serikali imeshindwa kuwapa. Ni hapa ndipo Idol itakuwa na nguvu kuliko kiongozi aliye hai.

Kama Wakatoliki wamempa Nyerere kuwa Mtakatifu iko siku zitazuka dhehebu au dini nyingine nazo zitamsimika Magufuli kuwa Mtakatifu wao (na hapa pia ndipo tutakapopima kauli ile ya Makamba ya wema na wabaya)

Caucasians wenyewe wanatamani wangepata kinasaba chake wangeenda kuchunguza kama kweli alikuwa mwafrika 100%.

Msiba wake kwa kauli ya PM ulifuatiliwa na watu 3.5 bl kati ya watu 7.5 bl wa dunia.

Marais 14 duniani walisitisha kazi kwa muda kufuatilia maziko Kijijini Mlimani Chato kwa njia ya TV.

Viongozi wa nchi na serikali zaidi ya 20 hawakujali Uviko-19 na wakahudhuria maziko. What if kama Uviko-19 isingekuwepo? Tz pangetosha? Siingekuwa kama nyomi la Kombe la Dunia!.

Kwa mara ya kwanza nilishuhudia wapiganaji (maaskari) wakitokwa machozi hadharani Kijijini Mlimani.

Kiongozi wa nchi ni nembo ya nchi, ukimdhihaki umeidhihaki nchi yako na ukiidhihaki nchi yako umejidhihaki mwenyewe (wewe ni mtumwa)

Watz tunatia aibu. Hata kwenye forums za ughaibuni Watz wanatia aibu. Watz wanashindwa kujenga hoja. Hawawezi kutengeneza mahusiano ya maudhui/content, muktadha/context na mantiki/logic. Hawana maarifa ya Critical Thinking/Kufikiri kwa makini na Critical Reasoning/Kujenga hoja kwa umakini. Watz wakipewa changamoto wanaishia kutukana (wanajibu hoja kwa matusi na dhihaka badala ya kujibu kwa point)

View attachment 2457745View attachment 2457746
Umenena !!
 
Wote waliohusika kumsema Magufuli kwenye zile sauti zilizovuja, wote walipotezwa kisiasa kasoro Nape na Makamba.

Ngeleja japo hakuwa mshiriki mkubwa na kuwa wa kwanza kuomba msamaha lakini alipotezwa kwenye ubunge baada ya Magufuli kumfadhili mshindani wake.

Membe alifukuzwa, Kinana nae akawa suspended kwenye chama(hata hivyo baadae Magufuli alimrudisha licha ya Kinana kutoomba msamaha rasmi).

Lakini Nape na Makamba japo ndio walikuwa viongozi wakuu wa uasi ule, Magufuli aliwaacha wakapita kwenye kura za maoni ndani CCM na majina yao hakuyakata na wakarudi bungeni na sasa ni mawaziri wenye nguvu kwenye Serikali ya Samia.

Sasa nauliza kwa nini Magufuli alikuwa anaogopa kuwaadhibu hawa watu?

Leo hii wafuasi wa Magufuli wanateseka sana wakiona Nape na Makamba wanavyotesa na kuvimba huku wakiwatupia vijembe.
Aliwaogopa kiaje
 
Wote waliohusika kumsema Magufuli kwenye zile sauti zilizovuja, wote walipotezwa kisiasa kasoro Nape na Makamba.

Ngeleja japo hakuwa mshiriki mkubwa na kuwa wa kwanza kuomba msamaha lakini alipotezwa kwenye ubunge baada ya Magufuli kumfadhili mshindani wake.

Membe alifukuzwa, Kinana nae akawa suspended kwenye chama(hata hivyo baadae Magufuli alimrudisha licha ya Kinana kutoomba msamaha rasmi).

Lakini Nape na Makamba japo ndio walikuwa viongozi wakuu wa uasi ule, Magufuli aliwaacha wakapita kwenye kura za maoni ndani CCM na majina yao hakuyakata na wakarudi bungeni na sasa ni mawaziri wenye nguvu kwenye Serikali ya Samia.

Sasa nauliza kwa nini Magufuli alikuwa anaogopa kuwaadhibu hawa watu?

Leo hii wafuasi wa Magufuli wanateseka sana wakiona Nape na Makamba wanavyotesa na kuvimba huku wakiwatupia vijembe.
Mwamba Magu awezi kuwaogopa vikaragosi hao.
Najua wana tumia fedha kwenya mass media kusafisha majina yao. Waulize kwa nini waliomba msamaha na kunywea kwa Magu?
 
Mwamba Magu awezi kuwaogopa vikaragosi hao.
Najua wana tumia fedha kwenya mass media kusafisha majina yao. Waulize kwa nini waliomba msamaha na kunywea kwa Magu?
Ile ilikuwa ni kumpiga chenga ya mwili
 
Wewe uko shimoni naona, ndio maana hukuona zile habari za viongozi wa Chadema wakikatwa mapanga na kuuawa
Viongozi wawapi waliouwawa kwa mapanga?ukisema Mawazo Magufuli alikuwa bado hajawa Rais ndio alikuwa anagombea hivyo alikuwa hajawa na mamlaka,Mtikila kafariki kabla ya Magufuli kuwa Rais,nitajie Wapinzani wapi waliouwawa na Magufuli kama sio maneno ya vijiweni tu.
 
Mwamba Magu awezi kuwaogopa vikaragosi hao.
Najua wana tumia fedha kwenya mass media kusafisha majina yao. Waulize kwa nini waliomba msamaha na kunywea kwa Magu?
Vikaragosi? Huyo mwamba yupo wapi na hivyo vikaragosi vipo wapi? Unamjua ROSTAM WEWE? alimpeleka low asali ikulu kama nani? Kilichafuatia baada aya pale? Unachezea system wewe???
 
Mlishindwa mwelewa JPM, ni hili ndo kosa kubwa alilolifanya .

Kikawaida Adui, mtafune na ummalize jumla jumla.

Ila Kwakuwa JPM, mkristo wa watu, mahiri asiyekuwa na makuu.

Yeye baada ya kuwashughuli awali kama funzo, na akawaona kama Vijana wake ambao walihitaji tu kuelekezwa, aliamua kuwasamehe.

Na aliwasamehe Kwa Moyo mweupe kabisaaa , akiombwa na kubembelezwa na wazee !!.

Mzee wa watu akawasamehee, na wao wakamuaminisha hawana kinyongo.!!.


Leo tunaambiwa "Watu wazuri hawafi"....



Ukristo hautoi maelekezo ya kumsamehe mtu hadharani mbele ya makamera baada ya kumtembeza mwendo mrefu huku unamchoresha kwenye kamera labda kama ni ukristo wa Chato ila kimaandiko kusameheana ni baina ya waliokoseana tu bila kuhusisha wengine (Siri)
 
Dkt Magufuli alikuwa mzalendo sana, aliamini ktk vijana ndiyo maana akawaacha. Ila kwa sasa laana inawatesa sana Nape na January.
Ungesema Nduli Magufuli alikuwa Dictator na aliamini yeye ni zaidi ya nguvu za Mungu na akajiimarisha kiusukuma, dhulma, ubinafsi roho mbaya na ukatili ila kwa nguvu za Mungu yote hayo Mungu kayatokomeza milele na aliwashindwa Nape na Makamba ,na kwa sasa Neema ya Mungu inawameremeta, na machawa ya lake zone wangali hawaamini waking'ata midomo yao
 
Back
Top Bottom