Kwanini Malipo ya kazi ya anuani za makazi Ilala yawe ni kidogo sana?

Kwanini Malipo ya kazi ya anuani za makazi Ilala yawe ni kidogo sana?

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2021
Posts
1,505
Reaction score
4,427
Habarini,

Niende moja kwa moja kwenye mada. Kiukweli nimefurahishwa na huu mpango wa anuani ya makazi na postikodi ambao kwa namna moja au nyingine litawezesha vijana kupata ajira hizo za muda mfupi.

Kilichonisukuma kuandika ni kuona vijana watakaofanikiwa kupata kazi hizo kulipwa ujira tofauti huku wakifanya kazi ile ile na majukumu Yale Yale.

Mfano katika halmashauri ya jiji la Dar es salaam kwa maana ya ilala wana kiwango cha chini sana cha malipo kwa kazi hiyo. Malipo yao kwa mwezi ni shilling 450,000 ambayo ni wastani wa shilling 15,000 huku halmashauri zote ndani ya dar es salaam malipo ni wastani wa Tsh. 30,000 kwa siku.

Je, ni nini kilichopelekea malipo kidogo kwa Jiji la Ilala?

Je, bajeti waliyopewa ni ndogo?

Kwa nini serikali isiweke kiwango elekezi cha malipo kuondoa sintofahamu hiyo?

NB: Nasikia harufu ya upigaji jiji la Ilala.
 
Bora huko 15000, kuna wilaya moja huku Mwanza wajumbe ndo wameingia wenyewe mzigoni[emoji119][emoji119]
 
Inawezekana kila halmashauri inajitegemea so wanalipa kilingana na pato lao
 
Back
Top Bottom