Kwanini Mapadri na Masister hawaruhusiwi kuoa au kuolewa lakini wanasisitiza wenzao waoe na kuolewa?

Kwanini Mapadri na Masister hawaruhusiwi kuoa au kuolewa lakini wanasisitiza wenzao waoe na kuolewa?

HAKI KWA WOTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2022
Posts
2,783
Reaction score
2,396
Habarini,

Hili jambo linanitatiza sana,sana iwapo wafuasi wa yesu wanaoa na kuolewa kupitia kwa mapadri na masister inakuwaje wenyewe mapadri na masister wasioe ma wasiolewe?

Kila kiungo cha mwili kiliumbwa na Mungu kwa makusudi ma kazi yake sasa hawa mapadri ma masisyer siga ya kwanza ni wawe marijali je hivyo viungo vyao wanavitumiaje na mwili wao ukiwa timamu??

Unafiki huu kwa Waafrika unapaswa kupuuzwa kwani padri anawezaje kufungisha ndoa au kusuluhisha wanandoa wakati yeye hana mke na wala hana uzoefu na ndoa?

Yaani hata hili wafia dini wameshindwa kutambua kuwa ni swala la kiuchumi kwa wakoloni kulileta ktk hali hii wakiamini padri au sister akioa au kuolewa ataanzisha familia ambayo itategemea mapato ya sadaka na kusababisha hasara kanisani itakayopelekea wakoloni kutopata faida?

Waafrika situkeni!!
 
Mapadre wamekula kiapo cha USEJA

1 Wakorintho 7:1 "Na sasa kuhusu mambo mliyoniandikia. Ni vizuri mtu asioe"

Je, Mtume Paulo, Petro na hata Yesu walioa? HAPANA

Ni vigumu kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja. Ni vigumu kujitoa 100% Kuchunga kondoo wa Bwana na huku una jukumu la Mke na Familia. Ndiyo maana kuna wito wa familia na wito wa useja. Mapadre na Masista wote wameitwa katika useja.

1Wakorintho 7:1.8
“Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika,ni heri mwanaume asimguse mwanamke,8.Lakini nawaambia wale wasiooa bado na wajane heri wakae kama mimi nilivyo”
Na Paulo Mtume anasema “Ni bora kuoa au kuolewa” lakini hakusema “Ni LAZIMA kuoa au kuolewa”
Suala la kutooa kwa mapadre kadiri ya historia lilianza tangu zamani kabisa mwanzoni mwa milenia ya pili katika mtagusi wa pili wa Laterani mwaka wa 1139 ili waweze kumtumikia Mungu kwa uhuru na bila mawaa wala pasipo vikwazo(1wakorintho 7:32-35)
1wakorintho 7:32-35
“32Lakini nataka msiwe na masumbufu.Yeye asiyeoa hujishughulisha zaidi na mambo ya Bwana ampendezeje Bwana;33.bali yeye aliyeoa hujishughulisha zaidi na mambo ya dunia hii,jinsi atakavyompendeza mkewe.34-Tena iko tofauti kati ya mke na mwanamwali.Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana ili apate kuwa mtakatifu mwili na Roho.Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii,jinsi atakavyompendezesha mumewe.,35.Nasema hayo niwafaidie ninyi,si kwamba niwategee tanzi,bali kwaajili ya vile vipendezavyo,tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine”
Maandiko hayo hapo juu yanajieleza wala sidhani kama yanahitaji kufafanuliwa zaidi ya yanavyojifafanua yenyewe.
Watu wengine wanafikiri kwamba kutooa ni dhambi,kama ni hivyo basi hata Yesu mwenyewe alikosa maana hata yeye mwenyewe hakuoa.
Yesu mwenyewe anafundisha kuhusu ubikira(Mathayo 19:10-12)

Mathayo 19:10-12,
“Wanafunzi wake wakamwambia,kama mambo ya mme na mke yakiwa hivyo ni afadhali kutuooa kabisa.Lakini Yeye akawaambia ‘SI WOTE WAWEZAO KULIPOKEA NENO HILO,ILA TU WALE WALIOJALIWA,maana wako MATOWASHI waliozaliwa katika hali hiyo toka matumboni mwa mama zao;tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi,tena wako Matowashi WALIOJIFANYA WENYEWE KUWA MATOWASHI KWAAJILI YA UFALME WA MBINGUNI’,awezaye kulipokea neno hili na alipokee”
Yesu mwenyewe analifafanua jambo hili kwa mapana,katika orodha ya matowashi Yesu aliowataja,Mapadre ni Matowashi waliojifanya hivyo kwaajili ya huduma ya kanisa na ufalme wa Mungu.
Tena Yesu anatuambia waziwazi kwamba”sio wote wawezao kulipokea neno hilo”yaani sasa sio wote wawezao kuwa Matowashi(Mapadre)bali ni wale tu waliojaliwa na Mungu neema hiyo.wale wasioweza kuishi upadre huoa na kuwa na familia.Tena Yesu anamalizia kwa kusema “Awezaye kulipokea fundisho hili na alipokee”,kwa maana nyingine ni kusema “Fundisho au Utowashi huu sio wa lazima”anayeweza kuishi maisha hayo basi na ayapokee na yule asiyeweza basi aache!
Vilevile Mitume ili kumfuata Yesu kikamilifu waliyaacha yote waliokuwa nayo ikiwepo familia zao ili wamtumikie Bwana(Mathayo 19:27.29)
Mathayo 19:27.29:
“Ndipo Petro akajibu akamwambia ‘Tazama sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe,tutapata nini basi?29.Amini nawaambia,kila mtu aliyeacha nyumba au ndugu wa kiume au wakike,au baba au mama au watoto au mashamba KWAAJILI YA JINA LANGU,atapokea mara mia zaidi na kuurithi uzima wa milele”
katika injili hiyo,Yesu anadhihirisha kwamba aliyeacha hayo yaliotajwa si kwasababu hawezi kuyapata la hasha,bali ameyaacha hayo yote KWAAJILI YA JINA LA YESU atapokea mengi hapa duniani halafu tena ataurithi ufalme wa mbinguni.

Mapadre wameyaacha hayo yote,wameacha nyumba,familia zao na kila kitu SIO KWASABABU HAWANA UWEZO AU HAWAWEZI KUPATA MAMBO HAYO bali WAMEACHA KWASABABU YA KUMTUMIKIA MUNGU KWA KADIRI YA MAANDIKO MATAKATIFU na kwakutaka kwao kuyaishi kimamilifu MASHAURI YA INJILI ikiwepo USEJA.
Maneno ya Paulo na yale ya Yesu mwenyewe kuhusu kumtumikia Mungu bila kuoa sio ya bahati mbaya bali ndiyo njia bora na inayofaa sana na kukubalika mbele ya Mungu.
Kwahiyo unapowaona mapadre hawaoi ujue sababu yake ni hiyo kwamba “Wamejitoa kwaajili ya kulihudumia kanisa”
(Na pia huwa nawashangaa mno watu wanaowapiga vita Mapadre kwamba kwanini hawaoi,najiuliza je,hao Mapadre wamewakataza wao kwamba wasioe?.)..na kama jibu ni hapana,sasa Je,”Pilipili ya shamba usiyoila inakuwashia nini?”
TUMSIFU YESU KRISTO!
 
Habarini,

Hili jambo linanitatiza sana,sana iwapo wafuasi wa yesu wanaoa na kuolewa kupitia kwa mapadri na masister inakuwaje wenyewe mapadri na masister wasioe ma wasiolewe?

Kila kiungo cha mwili kiliumbwa na Mungu kwa makusudi ma kazi yake sasa hawa mapadri ma masisyer siga ya kwanza ni wawe marijali je hivyo viungo vyao wanavitumiaje na mwili wao ukiwa timamu??

Unafiki huu kwa Waafrika unapaswa kupuuzwa kwani padri anawezaje kufungisha ndoa au kusuluhisha wanandoa wakati yeye hana mke na wala hana uzoefu na ndoa?

Yaani hata hili wafia dini wameshindwa kutambua kuwa ni swala la kiuchumi kwa wakoloni kulileta ktk hali hii wakiamini padri au sister akioa au kuolewa ataanzisha familia ambayo itategemea mapato ya sadaka na kusababisha hasara kanisani itakayopelekea wakoloni kutopata faida?

Waafrika situkeni!!
Kama hutaki kuoa basi uwe shoga. Chagua moja, usiyumbishe jamii humu.
 
Nafikiri acha aje askifu aliweke bayana hili jambo
 
Hiyo ni life dedication yao kwa kumtumia Mungu , wapo wale Shaolin pia hawana mambo ya ndoa.
 
Patia picha Baba Askofu mtoto wake ni Shoga, Jambazi, au Malaya au ana Kesi ya Mauaji alafu Mke wake anadai Talaka au Mke wake anaenda kwa waganga na mama mkwe anadai mwanaye apewe talaka na aachiwe urithi wa Baba Askofu 😀 Alafu huyo askofu anatakiwa achunge kondoo wa Bwana labda anatakiwa akasalishe Misa mahali, Unadhani atakuwa sawa? Ni sahihi kabisa na tuwaheshimu Mapadre na masista kwa kuchagua maisha ya useja.Kama una wito wa kuwa baba/mama nenda kaoe/kaolewe. Kama una wito wa kuwa Padre/Sista/Shemasi nenda kwenye wito wako kama wale Monks/Friars wa Tai chi 😀 au Shaolin Monks ambao wanaishi milimani tu na wanaamini katika upweke. Hata Catholic kuna Wanaoitwa Mapadre wa Shirika la St. Francis (Franciscans) ambao zamani walikuwa hawavai viatu na wanaishi maisha ya upweke. Kuna shirika lingine wanafuga ndevu na wanaishi kwenye monastery na hawaongei tofauti na kusali, kufanya meditation tu, nk. Kwa hiyo kumtumikia Mungu kuna namna nyingi.
 
Je, Mtume Paulo, Petro na hata Yesu walioa? HAPANA

Petro atoke kwenye list maana alikuwa na mke.

Luka 4:38
[38]Akatoka katika sinagogi, akaingia katika nyumba ya Simoni. Naye mkwewe Simoni, mamaye mkewe, alikuwa ameshikwa na homa kali, wakamwomba kwa ajili yake.
And he arose out of the synagogue, and entered into Simon's house. And Simon's wife's mother was taken with a great fever; and they besought him for her.
 
Haijalishi, Yesu mwenyewe alisema ni vigumu kutumikia mabwana wawili. Hauwezi kusumbuliwa na mahangaiko ya Ndoa, Familia, Ndugu na hapohapo ukajitoa kwa ajili ya kuchunga kondoo wa Bwana.
 
Back
Top Bottom