Kwanini Marais wa Kiafrika hawathaminiwi wakienda Nchi za Ulaya?

Pia mzungu hawezi kukuthamini wakati unapomfanya role model wako Kagame na nchi yake ndiye mfano wa kuigwa.
 
Tatizo lako ni kutokufuatilia na kuyajua mambo yalivyo duniani, marais waliokwenda huko ni wengi ingawaje wewe unajua ni Samia tu, kubwa zaidi huyo Samia unayemtetea wewe si mgeni wa serikali ya marekani na haihusiki kwakua yeye ni mgeni wa UN. Jukumu la kuwapokea marais si la Biden kama mlivyoaminishana kwenye ubishi wenu wa Simba na Yanga kwamba anafanya ziara ya marekani! Rais wa Burundi, wa Zambia na nchi nyingine wamekwenda huko pia, kama unaona rais Samia amebaguliwa ishauri serikali ifunge ubalozi UN, nikufahamishe tu balozi wetu UN hahusiani na ofisi ya balozi wetu Marekani, shughuri zao tofauti.
Ushauri, kabla ya kulalama jifunze historia na chanzo cha UN iliyotokana na LN iliyokuwa na makao Uswizi kisha UNO.
 
UN ni zaidi ya baraza kuu, UN inamashirika mengi sana ambayo yanatupa msaada tukiwa wanachama, inaekekea shule hamfundishwi umuhimu wa UN na hamuulizi kwanini Nyerere alikwenda huko kudai uhuru na si uingereza.
Wengi wanaochangia mada hii wanaonesha hawaijui UN wanadhani ni ya serikali ya marekani!
 
Yaani JF ya miaka hii!! Swali gani hili?
 
Shughuli za UN hazina uhusiano na serikali ya US, kama akiwa na mualiko wa WH hapo utaona mbwembwe kidogo, sio kama za huku kwetu though
 
Mwenyeji wqke ni UN .....hawezi kupokelewa na Govt of US sababu sio mwaliko wao...ingawa anaweza kuomba kuonana na Joe B...Ikulu kwake pia watakutana mkutano UN
 
Amepokelewa na mtukanaji wa Taifa Mange Kimambi
 
Ikitokea na wao wakaja kwetu wakapokelewe na kina mkandamizaji tu it's just ngoma droo
 
Mi ningependa kujua ameenda na ndege ipi? dreamliner? Naona this time wamefanya siri...
 
Tujithamini sis kwanza
 
Tofautisha Raisi kutoka nchi za Afrika(ukiacha Afrika kusini,Misri,)na Raisi kutoka India,Pakistan,Korea,Japan,
Sie hatuna kitu,wanatujua,wametuzoea kama OMBA OMBA,
Hakuna Cha upekee wanachosikia kutoka kwetu kwenye kila nyanja ya maswala,Uchumi,sayansi,diplomasia,nk,zaidi wanasikia vita,na kupiga nyungu,
Lakini haikuwa hivi siku zote,
Nyerere na Mandela walieshimiwa kwa misimamo yao na sera zao dhabiti.
Kwa Nyerere ishu kama sera ya kutofungamana na upnde wowote,kuvunja mahusiano ya kibalozi na Israel,UK,kuwatetea wapalestina,Vita ya Kagera,Ukombozi wa kusini mwa Afrika.
Sasa unategemea Wamuheshimu Samia kwa lipi kufanya Royal tour!?,
 
Ndiyo maana mwafrika wa ukweli haendi huko! Mfano JPM
 

Ndio maana hayati Rais Magufuli, akutaka kwenda kwao😄
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…