Kwanini Marais wa Kiafrika hawathaminiwi wakienda Nchi za Ulaya?

Mama kaenda kuhudhuria UN sio ziara ya kiserikali kila nchi balozi zake zinawajibika na viongozi wao. Raha ya USA Mama akitoka peke yake pale bila wapambe hakuna hata wa kumuuliza amani tu mitaani shida yule dada mpambe kuvaa magwanda kaharibu show. NY hawana habari na mtu ni sehemu pekee duniani viongozi wote wa dunia wanakutana sehemu moja.
 
Mleta hoja naomba nikukumbushe kitu kimoja, Marekani siyo Ulaya!
 
Sisi Tupo Brainwashed kuhusu Viongozi wetu. Tunajinyenyekeza Kwao wakati wao Ndio wanatakiwa Wajinyenyekeze Kwetu maana Tumewapa Dhamana.

Sisi Bado tuna Tamaduni za Kiuchifu chifu na Kifalme falme za Kuogopwa ndio maana Wenzetu waliostaarabika Mnawaona Kama Hawashtuki kumbe sisi Ndio tunatakiwa Tujiulize
 
Kwani kaenda kwenye ziara rasmi ya kiserikali hadi apokelewe na Rais wa Marekani?
 
Sisi ndiyo wenye kimbelembele, tunadiriki mpaka kuwafukuza machinga wasionekane jijini ati wanaliaibisha taifa, USA wao kule wamerahisisha sana maisha, nyekundu ni nyekundu blue ni blue
 
Kuna mtu amesema "mama naomba nipige picha na wewe" mama bila noma akasimama, ingekuwa huku angepigwa mtama na kuchukuliwa mzobemzobe mpaka Segerea
Yaani Watanzania Wanaoishi Marekani Ndio walio Jitokeza Kumpokea Rais Wa JMT.
 
Wenzetu walishaachana na ujinga.
 
Sisi ni Watumwa bado. Wazungu wanatuona kama Watumwa tu.
 
Ndiyo maana hakukuwa na ulazima wa kuchukua delegtation kubwa ya kwenda kuhudhuria mkutano ambao hakuna atakeyesikiliza hotuba yako. Angalia mifanoi hii:


Mnangangwa anahutubia ukumbi mtupu.



 
Bro hao wamarekani watapokea wangapo? Ukienda suala la UN unapokelewa Na ubalosi wako. Ukienda umeutwa Na marekani mapokeI ni washngton sio New York. Hapo kaenda kwa business zake na sio za USA
 
Bosi wako unaka akuthamini anayekupa kula yako?

Hadi siku mtakapoacha kwenda kuwapigia magoti kuwaomba misaada.

Nyie kazi yenu kujisifu kwasasa Tanzania tunskopesheka badala ya kuwa na mikakati ya nyinyi kuwakopesha wengine nyinyi akili yenu mnawaza kukopesheka na misaada yao.

Tulia sindano iwaingie.,,
 
Yaani Biden aache kupanga mipango na NASA, FBI apoteze muda kumpokea Rais wetu anayesumbuliwa na Mbowe.

Hayo mapokezi tuyaote ndotoni tu
 
Bro ni vizuri ujifunze mambo vizuri,kabla hujaandika kitu,nchi za ulaya na marekani hawana utamaduni wa kumpokea rais wa nchi yoyote kama tunavyofanya sisi,marais wa nchi hizo huwa hawaendi uwanja wa ndege kupokea marais,hata anapokuja rais wa nchi kubwa.Huo ndio utamaduni wao

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…