Uchaguzi 2020 Kwanini Marais wanaoangalia maslahi ya nchi zao hawatakiwi na Marekani?

Uchaguzi 2020 Kwanini Marais wanaoangalia maslahi ya nchi zao hawatakiwi na Marekani?

Tatizo siyo kuwakazia mataifa ya nje...

Tatizo linakuja pale unapokazia mpaka wananchi wake mwenyewe...

Cc: mahondaw

Kanuni za kuongoza nchi yeyeto duniani ni mbili
. usisomeshe namba watu wak
.usiwachokoze wakuu wa dunia
Hapo ni lzm uvune ulichopanda
 
Vipofu na viziwi tu ndiyo wanaweza wakasema Marekani kuna haki za binadamu, werevu tunaona ukiukwaji wa haki za binadamu mara kibao na raia wanauawa wazi wazi, wanakuja kupora mali zetu kwa jina la demokrasia, haki za binadamu na brabra nyingi, halafu watu wanaojiita wasomi kumbe ni wavivu waliozoea kuiba na kufisadi ndio wanaunga mkono, kosa vyote kuliko kukosa jicho na akili ya kung' mua yaliyojificha nyuma ya pazia. Kamwe Tanzania haiwezi kuwa chini ya wasaliti, mapandikizi na waliojaa roho mbaya kama Lisu na orodha yao kwa ujumla.
Madikteta uchwara wa Afrika hupenda sana kutumia kisingizio cha kuangalia maslahi ya nchi na uzalendo kuwatendea udhalimu wananchi wao. Nchi ambazo zimeendelea ikiwa ni pamoja na Marekani ni watetezi wakubwa wa haki za binadamu, demokrasia na utawala unaozingatia haki na sheria. Sasa wewe dikteta ukifikiri bado tunaishi enzi za old stone age (na madikteta wengi hufikiri hivyo) utakuta dunia nzima inakusuta.

Kuna ubaya gani wa kulinda maslahi ya nchi yako (yaani ukawa mzalendo kweli kweli) na wakati huo huo ukawatendea haki (haki za msingi za kibinadamu) wananchi wako na ukazingatia utawala wa sheria ambao ni silaha muhimu kulinda maslahi hayo ya nchi? Ukiona mtu hafanyi haya, huyo ni dikiteta na ni halali yake kupingwa kadri iwezekanavyo ndani na nje ya nchi.
 
Baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani na kuamua Tanzania iwe nchi inayojitegemea katika masuala yake za kiuchumi pamoja na kuleta mageuzi makubwa katika mikataba ya madini na uwindaji wanyama imekuwa kero kubwa kwa hawa wa Marekani.

Namkumbuka baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani kundi la maseneta waliwasili na kujaribu kuonana na Rais Magufuli lakini hawakufanikiwa.

Tumeona huko Venazuela na Bolivia jinsi serikali za nchi hizo zillizopata misukosuko baada ya kuvunja mikataba na makampuni za kinyonyaji za Marekani.

Watanzania tuache ushabiki wa kisiasa ni Rais Magufuli pekee ambaye atatuvusha watanzania kuelekea taifa lenye uchumi imara. Hawa wa Marekani wanapenda kukumbatia viongozi mafisadi.
Daaaaaaah Kwenye mfano hapo ndo ulipoaribu uhalisia wa mada, Magufuli hangalii maslahi ya nchi, ila angalia maslahi ya tumbo lake
 
Mtakumbuka CCM na Rais Magufuli kwani hata Kenya walimwita hayati Rais Moi Dictator. Walimwondoa kwa mbwembwe na kupata katiba mpya lakini leo wakenya wamekuwa masikini kuliko enzi ya utawala wa Rais Moi na Ufisadi umezidi kuwa mbaya sana. Tundu Lissu katika kampeni zake ameipa somo zuri sana CCM na nategemea CCM itafanyia kazi. President Magufuli still is the best for this country
Umetumwa wewe
 
Uko sahihi kwa asilimia 100! Naweka mkazo pale unaposema Watanzania tuache ushabiki wa kisiasa kwani Marekani wanapenda kukumbatia viongozi mafisadi. Tumeona barua aliyoandika mwanasheria wa Lissu akimuonya JPM kwa maneno makali kama vile anamuonya mtoto wake.

Umetoa mifano ya Venezuela na Bolivia ambazo zilikuwa zikijitutumua kulinda uchumi wao. Vivyo hivyo hata kwa Iraq na Libya. Tukaambiwa viongozi wao ni madikteta. Tunajionea wenyewe 'demokrasia' iliyofuatia kuuawa kwa Saddam Hussein na Moamar Gaddafi. Watanzania tujifunze kutokana na historia hiyo.
Tatizo uyu ni mshamba.anaendesha nchi kawa wote wasukuma
 
Hivi kweli watanzania leo tuone Tanzania ikiongozwa na mawaziri ya aina ya Hallima Mdee, Lema ama Heche. Dunia itatushangaa sana
Sasa ivi wanashanga kweli kuongozwa na uyu eti phd holder.mara maendeleo hayana vyama,Mara kwenye upinzani sileti maendeleo,wanatushangaa kweeeli kweli
 
Upo sahihi japo pia si wazungu wote.
Tatizo ni sisi viongozi weusi tukipata madaraka akili zetu huehuka na kujiona miungu.
Mtu anapost kibonzo cha happy birthday - anaswekwa ndani.
Mtu akikosoa jambo- jela
Mkosoaji anawindwa kuliko jambazi. Watu wanaishi kwa hofu nchini mwao.

Kweli tulinde mali zetu lakini tusinyanyasane.
Tuheshimu katiba na sheria zetu.

(Hapo ukute hata majibu haya tu tayari naanza kuwindwa)
Asante mkuu.eti nchi huru yangu 1961 halafu kuna watu wasiojulikana??upuuzi tu huo.waje tu wazungu
 
hakuna mtu au Mtanzania aliemchukia Magufuli,wananchi wanaichukia CCM ,msimbakizie matatizo Magu,hili linawahusu CCM wote kwa ujumla wao,matatizo kuanzia serikali kuu mpaka serikali za mitaa ni shida tu.

CCM walifunga mikutano kwa vyama vingine,Mauaji mengi yasio na maelezo ya uhakika yametokea kiasi sasa wananchi wanaishi kwa hofu,kubambikiziwa kesi kumekuwa jambo la kawaida chini ya utawala wa CCM ,yaani ni shida tu,

sasani zamu ya wananchi kuamua na mnatakiwa muheshimu,tume ikivuruga na wao watavurugwa.
 
#ZEC mnaulizwa hawa Wapiga Kura yenu ya Mapema hapo tarehe 27/10/2020 mmewatoa wapi katika mitaa na vijiji vya #Zanzibar? Maana Raha ya #Zanzibar tunajuana kila mtaa na kijiji. Mliwaandikisha lini? Kama mmeamua kuuharibu huu Uchaguzi nyiye ndiyo mtakaowajibika kwa matokeo ya matendo yenu.

View attachment 1610078
Inasemekana hio ni fomu kutoka sehemu za Tunduru wameletewa,angalia hayo majina utajua imenyofolewa sehemu gani hapa Tanzania bara.
 
Usidanganyike mkuu Marekani anapenda sana kuona nchi inakuwa failed state ili waibe mali asili mfano halisi ni huko Syria kwasasa Wamarekani wanaiba mafuta nchini humo baada ya kuanzisha vita kwa jina la demokrasia

..unadhani kati ya Syria na Saudi Arabia Marekani anaipenda nchi gani?

..anaipenda zaidi Saudia. kwasababu, kwanza wana amani, na pili wana viongozi mafisadi.

..huko Syria mpaka watoe hayo mafuta ni lazima warushiane marisasi, mabomu, drones, it is just too costly and risky.

..Wamarekani na mabeberu do not want failed states. Failed states zinaongeza gharama za wao kuiba rasilimali za nchi changa.

..Habari ya kusema kwamba mabeberu wanataka kutuletea vita ni uongo na tunapaswa kuukataa.

..Vita huwa zinatokea ktk nchi ambazo kuna uminywaji wa haki. Na vita ikitokea mabeberu watakuja kuuza silaha, lakini silaha wanazouza inategemea na ukubwa na sophistication ya wanaopigana vita.

..Again, mabeberu wanapenda nchi yenye amani, yenye rasilimali, na yenye kiongozi fisadi. Hawapendi nchi yenye vita.

NB:

..mimi sipendi vita hata kidogo.
 
Mbona Rais wa Misri Sisi ni dikteta na muuaji mkubwa lakini mpaka leo anapewa misaada na heshima zote na Marekani.
Hawa Marekani ni wahuni wakubwa
Unatuambia sisi kinakuhusu nini??? Hujui siasa za mashariki ya kati kwa iyo kaa kimya. Kwa Mashariki ya kati Marekani anataka mtu wa kuhakikisha Israel inakuwa salama tu!
 
Madikteta wote yafaa wayashughulikie ndio yanaingiza dunia gharama za kuhudumia wakimbizi sababu ya malezi mabovu utotoni
 
Baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani na kuamua Tanzania iwe nchi inayojitegemea katika masuala yake za kiuchumi pamoja na kuleta mageuzi makubwa katika mikataba ya madini na uwindaji wanyama imekuwa kero kubwa kwa hawa wa Marekani.

Namkumbuka baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani kundi la maseneta waliwasili na kujaribu kuonana na Rais Magufuli lakini hawakufanikiwa.

Tumeona huko Venazuela na Bolivia jinsi serikali za nchi hizo zillizopata misukosuko baada ya kuvunja mikataba na makampuni za kinyonyaji za Marekani.

Watanzania tuache ushabiki wa kisiasa ni Rais Magufuli pekee ambaye atatuvusha watanzania kuelekea taifa lenye uchumi imara. Hawa wa Marekani wanapenda kukumbatia viongozi mafisadi.
Maslahi ya nchi au wananchi?
Tumia akili kidogo ulizibaki nazo
Tunataka tuishi vizuri,chakula kipatikane kwa uhakika kwa kuanzisha skim za umwagiliaji,mazao tuuze kwa maslahi,elimu iwe bora kwa kulipa vizuri walimu.

Huduma za afya ya uhakika na kwa bima.
Siyo midege na sgr
 
Chama Cha kikominist cha China kimetawala miaka 70 na leo China ndio nchi yenye uchumi mkubwa duniani. Rais Magufuli ametawala miaka 5 na ameonyesha uwezo mkubwa kwanini asipewe miaka 5 mingine akamilishe kazi zote alizozianzisha.
We unadhani ni kwa sababu gani uchumi wetu haufiki angalau asilimia 50% ya ule wa china ikiwa tumepishana miaka 11 pekee kiungozi?
 
Haiwezekani uminye uhuru na demokrasia watu wakuangalie tu.

Unafosi tulia na gambo wawe wabunge, ndo wananchi wanavyotaka? Nec na polisi wanavuruga uchaguzi halafu wananchi wakae kimya kisa nini

Sauti za wananchi zimefika ulaya ila kwa sasa bado sana 2025 ujinga huu ukiendelea tutalambishwa vikwazo hapo kipindupindu kitarudi na dawa hakuna
Mkuu unaongelea vikwazo 2025? Amini usiamini ngoja jiwe atangazwe na tume alafu baada ya muda utaniambia,l. Tena yawezekana ikawa vikwazo na baadhi ya watu kuburuzwa The Hague, mark my word
 
Baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani na kuamua Tanzania iwe nchi inayojitegemea katika masuala yake za kiuchumi pamoja na kuleta mageuzi makubwa katika mikataba ya madini na uwindaji wanyama imekuwa kero kubwa kwa hawa wa Marekani.

Namkumbuka baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani kundi la maseneta waliwasili na kujaribu kuonana na Rais Magufuli lakini hawakufanikiwa.

Tumeona huko Venazuela na Bolivia jinsi serikali za nchi hizo zillizopata misukosuko baada ya kuvunja mikataba na makampuni za kinyonyaji za Marekani.

Watanzania tuache ushabiki wa kisiasa ni Rais Magufuli pekee ambaye atatuvusha watanzania kuelekea taifa lenye uchumi imara. Hawa wa Marekani wanapenda kukumbatia viongozi mafisadi.
Namibia wana UCHUMI mzuri sana, tatizo la Magufuli hana utu
 
Mkuu unaongelea vikwazo 2025? Amini usiamini ngoja jiwe atangazwe na tume alafu baada ya muda utaniambia,l. Tena yawezekana ikawa vikwazo na baadhi ya watu kuburuzwa The Hague, mark my word
Kwani ni serious kiasi hicho?
 
..Mabeberu wanapenda nchi zenye amani na viongozi walarushwa ili wazinyonye vizuri.

..Tanzania na Magufuli wanavyo vigezo nilivyovitaja hapo juu.

..Amani ikikosekana hapa Tanzania, makampuni ya madini kama Barrick hayataweza kuchimba madini.

..Pia kukiwa hakuna kiongozi fisadi kama Jiwe, Tanzania haitanunua midege tusiyoihitaji toka kwa mabeberu.

..Kwa hiyo Mabeberu kama Marekani wanapenda Tanzania iwe na amani, na zaidi iwe na kiongozi fisadi anayewapelekea mapesa ya bure kama Jiwe na miradi yake ya ununuzi wa midege[dreamliners] tusiyoihitaji.

cc Chige
Hii pumba uliyoandika hapa haiendani kabisa na umri wako. Daah
 
Back
Top Bottom