Kwanini Marais wote tuliwaita 'Surname' yao wakati wa sasa tunamwita "Rais Samia"?

Kwanini Marais wote tuliwaita 'Surname' yao wakati wa sasa tunamwita "Rais Samia"?

MdogoWenu

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2009
Posts
553
Reaction score
917
Niliwahi kutukanwa kwamba sina adabu nilipoandika mahala jina "Rais Julius".

Nikaelekezwa kwamba wanaomwita jina Julius ni ndugu zake tu. Sisi wengine tunalazimika kumwandika au kumwita "Rais Nyerere".

Imekuwa hivyo tangu uhuru hadi juzi tu.

Hatukutumia majina kama Rais Ali, Rais Benjamin, Rais Jakaya, Raus John.

Hata kule Zanzibar tuliwaita kwa jina moja la surname, hatukuwaita Rais Abeid, Rais Aboud, Rais Idrisa, Rais Amour, Rais Amani, Rais Mohamed, Rais Hussein.

Wengine hata majina yai ya mwanzi hatujuyajua.

Sasa tumejikita kumuita huyu Raus Samia, sijajua jwa nini na kwa utaratibu upi.

Hebu nisaidieni kupata mantiki wnyi great thinkers.
 
Rais Samia ina Heshima kuliko hata Jakaya ..
 
Kama surname yake ingekuwa Suluhu , nategemea ingekuwa maarufu ila mama umuite Hassan kila muda haiji .Mama Samia inatosha
 
Mmmh! Labda kwenu huko lakini kwetu hatuna utamaduni huo
 
wanaomwita jina Julius ni ndugu zake tu. Sisi wengine tunalazimika kumwandika au kumwita "Rais Nyerere".
🤣🤣Umenikumbusha Moshi hii tabia.

Ukiwa na hela au cheo kikubwa ni haramu kuitwa jina lako halisi. Lazma utumie la ukoo,cheo au heshima au maarufu/a.k.a (Mushi,Massawe)

Ukimwita mkubwa wako jina "John" ni kukosa nidhamu na fimbo utachezea, wanaomwita ni wale tu rika lake au wakubwa zake tu
 
Mi naona ni inconvenience kwa Mwanamke kumwita surname yake.
Refer makazini na mavyuoni wengi wanatumia system ya kuita watu kwa surname, lakini wanawake hawaitwagi hivyo labda surname yake iwe na accent ya kuvutia.
 
Ni swala la Gender issue,ukimwita kwa jina lake la kwanza ina sound more
 
Mi naona ni inconvenience kwa Mwanamke kumwita sir name yake.
Refer makazini na mavyuoni wengi wanatumia system ya kuita watu kwa sir name, lakini wanawake hawaitwagi hivyo labda sir name yake iwe na accent ya kuvutia.

Surname
 
Hatuna utamaduni wa kuita mrs kama wenzetu
Ila tuna utamaduni wa kuita mama fulani ambapo kwa Rais haliwezekani na kumuita jina la Ukoo kwa mama haiwezekani

Nafikiri Rais Samia linatosha
 
Back
Top Bottom