Kwanini Mashabiki wa Simba nguvu zao na mijadala wameielekeza yanga na kuisahau timu yao?

Kwanini Mashabiki wa Simba nguvu zao na mijadala wameielekeza yanga na kuisahau timu yao?

Majok majok

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2023
Posts
783
Reaction score
2,057
Nimeshangaa sana awa wafuasi wa mangungu kutoijadili timu yao iliyopigwa nje ndani na Aly ahly na badala yake wamekuwa makini kujadili mechi za Yanga dhidi ya Mamelod kuanzia mechi ya kwanza mpaka ya mwisho Pretoria?

Najiuliza timu yao walishaikatia tamaa siku nyingi na imepoteza mvuto mbele ya jamii?

Kwa maana ata body language ya wachezaji wa Simba ulikuwa unaona kabisa Kama vile wanakwenda Misri kukamilisha ratiba tu na sio kingine!

Mbumbumbu wameona isiwe tabu wajibanze kuisapoti Mamelod wapate angalau furaha ya muda lakini na penyewe wamepigwa za uso kwa maana walichokuwa wanategemea toka kwao kwamba wataiadhibu yanga ipasavyo kimeshindikana mpaka mbeleko ya mwamuzi kuwaokoa!

Mbumbumbu wanashindwa kujadili ni namna Gani wafanye usajili Bora na kupata viongozi Bora wamebaki kuipaisha yanga kwa kuiongea Kila baada ya sekunde moja!

Wanasahau wanaowajadili wameshawapita na kuwaacha kwenye mipango Bora na uwekezaji ndani ya uwanja kwa kuwa na quality ya wachezaji wanaoweza kucheza na timu yoyote Ile barani Africa na kupata matokeo!

Timu yao imekwenda Misri wakiwa wanajua imejaza wachezaji wengi wanaopatikana tandale kwa mujibu wa mwina kaduguda ndio maana macho na masikio yao yalikuwa Pretoria!

Kwa stahili hii mangungu ataendelea kuwaongoza mpaka kiama kwa maana juzi alifanya Tena kile alichokifanya kwa kumleta manzoki kwenye mkutano safari hii kabla ya mechi akawaletea mayele akahojiwa kabisa na muimba taarab Ahmed Aly ikiwa ni kuamisha tension ya mashabiki baada ya kichapo wasijadili kichapo Bali wajadili uwepo wa mayele kwenye kambi ya Simba na tetesi za usajili wake!

Kuiongoza Simba kwa sasa ni rahisi sana Kama kuendesha kikundi Cha saccos ama vikao vya kisiasa kwakuwa wanaoongozwa Awana tofauti na nyumbu!

Nawaambia Tena jadilini matatizo yenu vinginevyo ule mnara wa 5G utasimama Tena kwenye mechi ya watani!!!
 
Kwao hawajaumia sababu walisha shangilia baada ya kupangiwa na Al Ahly, so hata wakikaa kimya sasa sio mbaya kwani walisha shangilia. Wewe si unaliona vibe la msemaji na viongozi, kuna uwezekano walikuwa wanajua wanacho enda kukutana nacho,kwanzo kwao robo ni hatua kubwa kwao na ni kitu cha kawaida ndio maana hawa kushangaa kwani wanajua wao wanaishia robo.

View: https://m.youtube.com/watch?v=bwBTWSJNSjU&t=307s
 
Sasa kama jirani ameamua kuangua kilio kuanzia usiku mpk muda huu utaachaje kumpa kampani alie vzr?? Sisi mlitucheka mwakarobo ndo hivyo tuko kwny kawaida yetu..nyie pambaneni na kesi zenu..tupo kuwakampani kivyovyote vile...
 
Kalpana, kuna story imeanza juzi juzi hapa ya jamaa alienda beach akaanza kufatiliwa sijui, nimeipoteza kama unaikumbuka nitag embu.
Cc cocastic mshamba_hachekwi Nifah
 
Zm
Sasa kama jirani ameamua kuangua kilio kuanzia usiku mpk muda huu utaachaje kumpa kampani alie vzr?? Sisi mlitucheka mwakarobo ndo hivyo tuko kwny kawaida yetu..nyie pambaneni na kesi zenu..tupo kuwakampani kivyovyote vile...
 
Attachments

  • FB_IMG_1711632154119.jpg
    FB_IMG_1711632154119.jpg
    60.4 KB · Views: 4
Sasa simba kuna kipi interesting cha kuongelea🤷🤷🤷
 
Mashabiki wa simba wanatakiwa kumpa tuzo ya maono ya mbali; Mwenyekiti wao Rage kwa kuwaita hadharani mbumbumbu. Aisee yule mzee aliona mbali.
 
Sasa kama jirani ameamua kuangua kilio kuanzia usiku mpk muda huu utaachaje kumpa kampani alie vzr?? Sisi mlitucheka mwakarobo ndo hivyo tuko kwny kawaida yetu..nyie pambaneni na kesi zenu..tupo kuwakampani kivyovyote vile...
Hahahahaha
 
Back
Top Bottom