Kwanini Matajiri wa siku hizi hawawezi kuishi na watu wengi majumbani mwao kuliko wale wa enzi za zamani?

Kwanini Matajiri wa siku hizi hawawezi kuishi na watu wengi majumbani mwao kuliko wale wa enzi za zamani?

Lakini ujue jambo hili, kwamba katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari zilizo ngumu kushughulika nazo.2Kwa maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda pesa, wenye kujidai, wenye majivuno, wakufuru, wasiotii wazazi, wasio na shukrani, wasio washikamanifu,3wasio na upendo wa asili, wasiotaka makubaliano yoyote, wachongezi, wasiojizuia, wakali, wasiopenda wema,4wasaliti, wenye vichwa vigumu, waliojaa kiburi, wanaopenda raha badala ya kumpenda Mungu,5wakionekana kama watu wanaomwogopa Mungu lakini wakizikana nguvu zake; nawe jiepushe nao.
Tafuta hela uondokane na hayo makasiriko
 
Miaka ya nyuma, hata urudi katika vitabu vitakatifu, watu matajiri waliishi na watu wengi nyumbani na wote walinyooshwa na kutii sheria za nyumbani.
Mfano Nabii Ibrahim alukuwa Bilionea aliyeishi na mamia ya watu kwenye familia yake. Alikuwa hadi anajeshi la watu 300 ambao ni sehemu ya familia yake.

Wazee wetu matajiri wa zamani walikuwa na wake wengi pamoja na watoto kibao. mji ulikuwa na ndugu lukuki hadi wale walioomba jujiunga na undugu. Bado wote walinyooshwa kwa mkono wa chuma, unaweza usisikie hata mtoto anamimba bila kuolewa.

Siku hizi tatizo ni nini?
Unakuta mtu tajiri, hajiamini, anaishi na vitoto vyake viwili na housegirl/Boy na mkewe. Hataki kusikia shangazi, mjomba wala kuarika watu kwake.

karibuni kwa maoni.
JE uwezo wa wanaume wenye pesa mingi kutiisha familia zao umeshuka?

Je utajiri wa hofu?

Je ndugu na marafiki wa zama hizi usnitch na umbea umezidi kiasi kwamba huwezi kuwanyoosha?

unadhani kwa nini
Ndumba mzee hao bandugu wanaharibu sana.
 
Dunia imebadilika sana na inaenda kwa kasi
Kukiwa na ndugu wengi hata wachache ni yaleyale tu wote wamekuwa hawana maadili na heshima kama zamani
Mtoto anakuja kukaa kwa mda mfupi au mrefu lakini vituko unaona mara arudi manane ya usiku na ukimkaripia anakunja uso na kumwambia mama yake ooh uncle ananinyanyasa

Watoto na Mali ni Fitna hili tumefundisha kwenye vitabu

Kaa mbali nao kama kuwasaidia wasaidie walipo ila usiwalee zaidi ya yatima

Siku hizi hata uliemzaa anakulia time kama una mali anataka utangulie kuzimu
 
Marehemu Baba aliwalea ndugu kibao, lakini hao aliowalea hakuna hata mmoja anaonyesha fadhila kiduchu tu ya hata kunijulia hali mimi mwakilishi wa Baba.

Kwasababu hii ya waliolelewa kukosa fadhila, ndiyo maana matajiri wa siku hizi hawataki kukaa na ndugu.
 
Sababu wamegundua uadui huanziaga kwa ndugu wa nyumbani mwa mtu.

Ukianza kupata neema ya kipato basi ujue unaingia kwenye short list ya target ya kurogwa na ndugu.

Yaani hawana maana hata kidogo.

Yaani watakuroga pande zote za Dunia kila mtu anakupiga kivyake.

Baba Mungu Jehova na awalipe maana visasi na hukumu kasema viko mikononi mwake yeye mwenyewe.
 
Kweli nimeaamini ya kuwa Dunia haina haki wakati mwingine.

Unaweza kuwa na moyo wa kupenda sana ndugu lakini ukawa mtu wa kupigwa vita na uadui mkubwa bila wewe mwenyewe kujua mpaka Mungu aamue kukufunulia kwa kadiri ya rehema zake!
 
IMG_7051.png
 
Miaka ya nyuma, hata urudi katika vitabu vitakatifu, watu matajiri waliishi na watu wengi nyumbani na wote walinyooshwa na kutii sheria za nyumbani.
Mfano Nabii Ibrahim alukuwa Bilionea aliyeishi na mamia ya watu kwenye familia yake. Alikuwa hadi anajeshi la watu 300 ambao ni sehemu ya familia yake.

Wazee wetu matajiri wa zamani walikuwa na wake wengi pamoja na watoto kibao. mji ulikuwa na ndugu lukuki hadi wale walioomba jujiunga na undugu. Bado wote walinyooshwa kwa mkono wa chuma, unaweza usisikie hata mtoto anamimba bila kuolewa.

Siku hizi tatizo ni nini?
Unakuta mtu tajiri, hajiamini, anaishi na vitoto vyake viwili na housegirl/Boy na mkewe. Hataki kusikia shangazi, mjomba wala kuarika watu kwake.

karibuni kwa maoni.
JE uwezo wa wanaume wenye pesa mingi kutiisha familia zao umeshuka?

Je utajiri wa hofu?

Je ndugu na marafiki wa zama hizi usnitch na umbea umezidi kiasi kwamba huwezi kuwanyoosha?

unadhani kwa nini
Matajiri wa sa hii ni wachoyo kheeeeee
 
Back
Top Bottom