Mtu Fodontino
JF-Expert Member
- May 9, 2021
- 351
- 558
Ubepari haunaga hizi mambo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Leo familia yake itakuwa inakufa masikin na walio saidiwa hawarudishi fadhila kwa hiyo familia.Ila kweli nakumbuka mjomba wangu mwenyezi mungu amrehem ukifika kwake ilikuwa ndio sehemu yakujua ndugu maana nyumbani kwake kila mwenye shida na asiye na shida ilikuwa kimbilio, la wagonjwa, wanataka kusoma, kazi au mtaji na katika biashara zake walikuwa ndugu na jamaa wa karibu.
Sasa kabaki yule Shangai mnoko hatari, kweli kizuri akiishi daima.
Kiukweli ukikwama Maskini kwao ni furaha kubwa sana. Kwa hali ilivyo kila mtu abebe msalaba wake. Hakuna haja ya kufuatana fuatana. Cha muhimu wazazi wapambane kuhakikisha watoto wanapendana na wanakuja kujitegemea baadae. Sio kwenye familia inatokea watoto wanne maskini wa kutupwa mmoja ndo anajiweza. Wazazi hakikisheni watoto wanapata maadili na elimu nzuri. Inasaidia sana kupunguza matatizo.Ndugu masikini asilimia kubwa wanakuwa na roho mbaya na chuki waliowahi kuwa matajiri na baadae kufirisika tayari majibu wanayo ndugu ata umbebe kiasi gani siku ukikwama atafurahi
Siku hizi hakuna utumwa kama wa zamani, japo kuna utumwa wa hiari.Miaka ya nyuma, hata urudi katika vitabu vitakatifu, watu matajiri waliishi na watu wengi nyumbani na wote walinyooshwa na kutii sheria za nyumbani.
Mfano Nabii Ibrahim alikuwa Bilionea aliyeishi na mamia ya watu kwenye familia yake. Alikuwa hadi anajeshi la watu 300 ambao ni sehemu ya familia yake.
Wazee wetu matajiri wa zamani walikuwa na wake wengi pamoja na watoto kibao. mji ulikuwa na ndugu lukuki hadi wale walioomba jujiunga na undugu. Bado wote walinyooshwa kwa mkono wa chuma, unaweza usisikie hata mtoto anamimba bila kuolewa.
Siku hizi tatizo ni nini?
Unakuta mtu tajiri, hajiamini, anaishi na vitoto vyake viwili na housegirl/Boy na mkewe. Hataki kusikia shangazi, mjomba wala kuarika watu kwake.
Karibuni kwa maoni.
JE uwezo wa wanaume wenye pesa mingi kutiisha familia zao umeshuka?
Je, utajiri wa hofu?
Je, ndugu na marafiki wa zama hizi usnitch na umbea umezidi kiasi kwamba huwezi kuwanyoosha?
Unadhani kwanini
Mh Mwakilishi wa baba je wewe huwa unawajulia hali hao ndugu zako?.marehemu Baba aliwalea ndugu kibao, lakini hao aliowalea hakuna hata mmoja anaonyesha fadhila kiduchu tu ya hata kunijulia hali mimi mwakilishi wa Baba.
kwasababu hii ya waliolelewa kukosa fadhila, ndiyo maana matajiri wa siku hizi hawataki kukaa na ndugu.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Ukikutwa na watu wengi nymbn inakua kesi mfano bosslady zumaridi
Hayo matambuko yao wachaga ya mbuzi siyo ushirikinaSasa mtu mmoja akajiuliza mnataka watu muwe maskini wa kutupa Mungu asiinue wakuu?! [emoji848]
Wenzetu wachaga tu kwa wastani ndio hawanaga mambo ya uchawi na ushirikina.
Na ndio maana walau wanaendelea.
Lakini the rest ni shida.
We ng'ombe haitakuja kutokea siku ya mwishoLakini ujue jambo hili, kwamba katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari zilizo ngumu kushughulika nazo.2Kwa maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda pesa, wenye kujidai, wenye majivuno, wakufuru, wasiotii wazazi, wasio na shukrani, wasio washikamanifu,3wasio na upendo wa asili, wasiotaka makubaliano yoyote, wachongezi, wasiojizuia, wakali, wasiopenda wema,4wasaliti, wenye vichwa vigumu, waliojaa kiburi, wanaopenda raha badala ya kumpenda Mungu,5wakionekana kama watu wanaomwogopa Mungu lakini wakizikana nguvu zake; nawe jiepushe nao.
Hayo matambuko yao wachaga ya mbuzi siyo ushirikina
Siku hizi maharage tu kilo 4000 utakaa na wangapi sasaUmagharibi unatuumiza, tunafata maisha ya magharibi, tunageza kila Jambo.
Hatimae siku hizi hatuna mapenzi, mtu anaishi miaka dahari hajuk jirani yake anaishi vipi, ni kwenye gari, akirudi ndaani.
Nyumbani ni yeye na watoto zake wawili, mbwa na wafanyakazi.
Hilo moja, pili(nazungumzia mpaka masikini) Maisha yamebadilika, mahitaji siku hizi si nguvu ni pesa inahiitjika, zamani unaishi na mtoto wa mjomba, sijui nani na nani, ila una shamba kubwaa nguvu ya kulima((nguvu kazi ipo) una ng'ombe kadhaa.
Asubuhi mnakamua lita kadhaa ndani mipunga kibao na mahindi, nyuma kisamvu, matembele, maboga maisha yanasogea. Ila siku hizi kimbembe, ugali tabu, huna hela hujala, mjini una chumba na sebule tu.
Kabisa na ina migogoro sana mkuuLeo familia yake itakuwa inakufa masikin na walio saidiwa hawarudishi fadhila kwa hiyo familia.
Binafsi isingekuwa hayo mambo ya uchawi na ushirikina wala nisingejali sababu Mungu ni Pendo na ametuagiza kuwa wakarimu kwa wageni.
Ni Baraka sana kuwapenda ndugu Na kuwakarimu wageni maana kwa kufanya hivyo wengine huweza kuwakaribisha
Malaika wa Mungu ndani ya Nyumba na familia zao.
Na akiingia Malaika basi ni baraka kuzidi sana Na ustawi full package.
Na huwa ni fahari kuwatendea ndugu mema na watu wengine pasipo kutaka kujionesha.
Lakini linapokuja swala la uchawi na ushirikina ndipo huwa nachoka kabisa !
Hayo matambuko yao wachaga ya mbuzi siyo ushirikina