Umagharibi unatuumiza, tunafata maisha ya magharibi, tunageza kila Jambo.
Hatimae siku hizi hatuna mapenzi, mtu anaishi miaka dahari hajuk jirani yake anaishi vipi, ni kwenye gari, akirudi ndaani.
Nyumbani ni yeye na watoto zake wawili, mbwa na wafanyakazi.
Hilo moja, pili(nazungumzia mpaka masikini) Maisha yamebadilika, mahitaji siku hizi si nguvu ni pesa inahiitjika, zamani unaishi na mtoto wa mjomba, sijui nani na nani, ila una shamba kubwaa nguvu ya kulima((nguvu kazi ipo) una ng'ombe kadhaa. Asubuhi mnakamua lita kadhaa ndani mipunga kibao na mahindi, nyuma kisamvu, matembele, maboga maisha yanasogea. Ila siku hizi kimbembe, ugali tabu, huna hela hujala, mjini una chumba na sebule tu.