Mbeya hakuna mzunguko mzuri wa pesa pamoja na kuwa expenses za maisha zipo chini.
biashara nyingi zinategemea wanachuo so vyuo vikifungwa biashara nyingi hazitembei.. i can say 50% ya population ya mbeya mjini ni wanachuo.
Pia kuna kitu kinaitwa baridi, nais ndo sababu ya mkoa kuongoza kitaifa kwenye suala la maambukizi ya VVU. Mbeya kulala peke yako usiku ni mtiani
Kuna vumbi la hatari kuanzia mwezi wa 8 mpaka mwezi wa 11, utapachukia Mbeya hio miezi.
Faida
Gharama za kuishi Mbeya zipo chini
Usafiri uhakika.. bajaji za kutosha kuliko watu.
kwenda Mikoani unasafiri hata usiku bila shida yoyote, kuna magari pale Uyole na stendi ya nanenane.
Vyakula kule ndo vinalimwa..wanavuna kila siku
Nenda Mbalizi sokoni au Nzovwe ndipo wakulima wanauza bidhaa zao kwa bei sawa na bure
Usiende Soweto au Mwanjelwa bei zao zipo juu kidogo.
Starehe zipo sana tena pesa haziishi kama apa Dar
Kuna Bar kama Mwailubi, Mwamunyange, City Pub, Polos, Nasoma, Mbeya pazuri na baadhi ya hotels za gharama nafuu kama ni mtu wa kujichanganya kama Usungilo, Modern Highlands, Desderia, Peace of Mind, Beaco Resort n.k
Sehemu za kukaa ni Forest Mpya, Isyesye, Veta, Block T, Iwambi.. usikae maeneo ya wanachuo kuna wizi sana.
Kama ni Mfanyabiashara unaweza kwenda kuanzisha moja ya hizi Biashara maana ni chache sana af wafanyabiashara wengi wa Mbeya hawajui Biashara in terms of customer care and creativity
Biashara ya kuuza nyama [ Butchery ]
Mfano Soko zima la kabwe hakuna Bucha la Kitimoto mpaka mtu utembee hadi Juakali - Mwanjelwa
Pharmacy / duka la Dawa
Izo huduma zinapatikana Maeneo ya Hospitali tu kama Maranatha na Kabwe Sokoni [ in short maduka ya dawa yapo along Tanzam Road tena ni machache hayafiki matano]
Biashara ya urembo wa kucha maeneo ya vyuo.
Mpaka sasa kuna jamaa mmoja tu pale Soweto ndo anasifika kwenye hiyo fani sehemu zingine zote ndo biashara zinaanzishwa wengi bado ni amateurs.
Mwisho ni Biashara ya kuuza simu.
Simu ambazo ni tofauti na Tecno na Infinix ambazo zinauzwa pale kwa Kwa Mtawa - Ilomba zina bei karibia mara dufu ya bei za Dar.
Ukitaka kununua Samsung au iPhone iwe ni used au mpya kwa Mbeya mpaka uwe vizuri mfukoni.
The choice is yours
Kama kuna nilichokisahau kinachoitaji ufafanuzi please inform me ntakufafanulia