Kwanini mbwa hugongwa sana na magari barabarani?

Kwanini mbwa hugongwa sana na magari barabarani?

Hata binadamu anagongwa
Na hoja ya kuwa mbwa ana akili kuliko wanyama wengine sio kweli ni hoja dhaifu kabisa

Mbwa hao wanaogongwa ni koko na mara nyingi kama kawaida ya waafrika kuwapiga mbwa pasipokuwa na sababu zozote hiyo ndio inachangia zaidi

Ukifanya utafiti mzuri utakuta asilimia kubwa walikuwa wanafukuzwa kwa mawe

Unakuta mpaka jitu Zima na akili zake likiona mbwa tu linaanza kutafuta mawe

Sijui dhana ya kuwachukia mbwa au wanyama kwa ujumla tumeitoa wapi.
Kila kitu tunamsingizia mwarabu na mzungu
Sasa mbona wazungu wanawapenda sana wanyama?

Hata India utakuta binadamu wanaamini kabisa wanyama walitutangulia na wengine wanaabudiwa kabisa kama miungu yao

Watoto wafundishwe kutokuwapiga wanyama nao wataishi vizuri tu
Hao wamekurupuliwa sehemu na sio kuwa walikatisha wakagongwa na magari
 
Hoja dhaifu sana hii mleta uzi mbona hata binadsmu hugongwa sana na magari Kila siku?
Hoja iliopo mezani, ni mbwa kugongwa sana, ukilinganisha na wanyama wengine, wafugwao, hata wanyama pori na binadamu hugongwa, ila leo amejiuliza juu ya mbwa.
 
Wanakuwaga na wenge sana wakati wa kuvuka barabara
273821B500000578-0-image-a-9_1427974117921.jpg
NB: Huyo mbwa aliyegongwa pichani, alipona bila jeraha lolote.
 
Juzi nimesafiri kutoka mkoa wa Dar es Salaam kwenda mkoa wa Shinyanga. Kijiografia, ni umbali mrefu, ambapo magari ya abiria hutumia si chini ya masaa 16 kufika mwisho wa safari.

Sasa kuna jambo moja nimeliona katika safari hii ndilo nataka wajuvi wa mambo ya wanyama watueleze, kwani ni jambo la kufikirisha kidogo!

Mnyama mbwa, ni miongoni mwa wanyama wanaotumiwa na binadamu katika shughuli mbalimbali za kijamii, kama ulinzi, kunusa, nk. Lakini pia, mnyama huyu anaweza kufundishwa michezo mbalimbali na akamudu kuicheza sawia.

Kwa muktadha huo, inaonyesha kuwa, mbwa ana akili pengine kuliko wanyama wengine, na ndiyo maana ni rahisi kwake kufundishika, tofauti na wanyama wengineo (most).

Sasa juzi katika safari yangu hiyo, nimeshuhudia si chini ya mbwa 6, mahala tofauti tofauti, wamegongwa na magari. Hapo ndio najiuliza, inakuwaje mnyama mwenye akili kuliko wengine; kama mbuzi, punda, paka, kuku, nguruwe, kondoo, ng'ombe, nk, anagongwa na magari wakati hawa wenye akili kidogo hawagongwi?!

Wakati tunajibu swali hili, majibu yetu tuhusianishe na ubongo wa mbwa, na sio factor nyingine kama uwingi wao, kukosa matunzo, kichaa cha mbwa, nk; kwani hizi ni hoja nyepesi. Mbwa wanaoongelewa hapa ni wakamilifu kwa mitazamo yote.

Mtu anaweza kuona nimeuliza jambo la kijinga, lakini wataalamu wa wanyama najuwa watakuja na sababu za msingi kuhusiana na jambo hili! Au wenzangu hamjawahi kijiuliza kwanini mbwa anagongwa kirahisi sana na magari kuliko wanyama wengine?

Mimi niseme hivi; binadamu tu ambaye anazo fikra naye anaweza kugongwa na gari sembuse mbwa?!--- mbwa mara nyingi huwa muoga kama utamtishia kumpiga fimbo au jiwe, yeye anajua hatari kutoka kwa binadamu ni jiwe na fimbo tu lakini hajui hatari ya kugongwa na gari linaloendeshwa na binadamu, yeye anajua gari ni kama kitu tu cha kawaida alichozoea kukiona kila siku katika mazingira yake mfano nyumba, mti, mawe nk hivyo haoni gari kama ni tishio kwa uhai wake ukiweka kutokuwa na uelewa juu ya neno "hatari".--- the same applies to the cat.
 
kidato cha nne na sita kuna topic inaitwa Genetics kuna kipengele kinaitwa colour blindness wamedadavua kwa kina sana na kidato cha tatu na tano kuna topic inaitwa coordination and sensitivity wameelezea sana.

You adress it to one who never went to school, lad.🤣
 
Je haya hapa chini sio maneno yake??![emoji1313]
Tatizo hapo ndugu yangu, ni dogo tu, umeshindwa kutofauti nyakati, Neno, Wakigongwa, na wamegongwa unaweza kuona kama neno moja, ila linatofautisha nyakati, nadhani umenielewa.
 
Mimi niseme hivi; binadamu tu ambaye anazo fikra naye anaweza kugongwa na gari sembuse mbwa?!--- mbwa mara nyingi huwa muoga kama utamtishia kumpiga fimbo au jiwe, yeye anajua hatari kutoka kwa binadamu ni jiwe na fimbo tu lakini hajui hatari ya kugongwa na gari linaloendeshwa na binadamu, yeye anajua gari ni kama kitu tu cha kawaida alichozoea kukiona kila siku katika mazingira yake mfano nyumba, mti, mawe nk hivyo haoni kama ni tishio kwa uhai wake ukiweka kutokuwa na uelewa juu ya neno "hatari".--- the same applies to the cat.
Hivi hizi tafsiri za wanyama huwa mnazitoa wapi,
 
Tatizo hapo ndugu yangu, ni dogo tu, umeshindwa kutofauti nyakati, Neno, Wakigongwa, na wamegongwa unaweza kuona kama neno moja, ila linatofautisha nyakati, nadhani umenielewa.

Vyovyote iwavyo, wakigongwa au wamegongwa, swali ni je walipofikwa na kitendo cha kugongwa wote hao walikuwa wamekufa au walikuwa wazima ??
 
Juzi nimesafiri kutoka mkoa wa Dar es Salaam kwenda mkoa wa Shinyanga. Kijiografia, ni umbali mrefu, ambapo magari ya abiria hutumia si chini ya masaa 16 kufika mwisho wa safari.

Sasa kuna jambo moja nimeliona katika safari hii ndilo nataka wajuvi wa mambo ya wanyama watueleze, kwani ni jambo la kufikirisha kidogo!

Mnyama mbwa, ni miongoni mwa wanyama wanaotumiwa na binadamu katika shughuli mbalimbali za kijamii, kama ulinzi, kunusa, nk. Lakini pia, mnyama huyu anaweza kufundishwa michezo mbalimbali na akamudu kuicheza sawia.

Kwa muktadha huo, inaonyesha kuwa, mbwa ana akili pengine kuliko wanyama wengine, na ndiyo maana ni rahisi kwake kufundishika, tofauti na wanyama wengineo (most).

Sasa juzi katika safari yangu hiyo, nimeshuhudia si chini ya mbwa 6, mahala tofauti tofauti, wamegongwa na magari. Hapo ndio najiuliza, inakuwaje mnyama mwenye akili kuliko wengine; kama mbuzi, punda, paka, kuku, nguruwe, kondoo, ng'ombe, nk, anagongwa na magari wakati hawa wenye akili kidogo hawagongwi?!

Wakati tunajibu swali hili, majibu yetu tuhusianishe na ubongo wa mbwa, na sio factor nyingine kama uwingi wao, kukosa matunzo, kichaa cha mbwa, nk; kwani hizi ni hoja nyepesi. Mbwa wanaoongelewa hapa ni wakamilifu kwa mitazamo yote.

Mtu anaweza kuona nimeuliza jambo la kijinga, lakini wataalamu wa wanyama najuwa watakuja na sababu za msingi kuhusiana na jambo hili! Au wenzangu hamjawahi kijiuliza kwanini mbwa anagongwa kirahisi sana na magari kuliko wanyama wengine?
Ni kwasababu mbwa hawaoni usiku. Siwezi kuelezea zaidi mm siyo mwana biologia
 
Interesting topic! Kwa mtazamo wangu, ni mchanganyiko wa sababu zinazofanya mbwa wengi kuwa wahanga wa ajali za gari. Kikubwa nadhani ni upekepeke wa hao wanyama, mbwa huwa wakati mwingine ni wajuaji sana.

Kuna mbwa wa jirani, Mama Kadada ambae jina lake alikuwa anaitwa Tom. Dog Tom ilikuwa lazima aende sambasamba na kila gari inayopita karibia na nyumbani. Anga za usiku, Tom ndio alikuwa mwenyekiti wa vikao. Pale jirani walikuwa wanakuja Mbwa kama hamsini kumfuata huyu mbwa wa Mama Kadada.

Niliporudi kutoka masomoni, nikaambiwa Tom alifariki kwa kugongwa na gari. Tabia za mbwa ni tofauti na paka. Paka ni kama vile wanajua kuepuka ajali kuliko mbwa.
 
Mbwa mara nyingi ugongwa nyakati za usiku. Hii ni kwasababu;

Wakati wa usiku barabara zenye rami utunza joto,, ambalo mnyama Mbwa upendelea zaidi kulala barabarani kwa lengo la kulifaidi joto hilo.

Usingizi na joto hilo umlaghai na kuhisi yupo sehemu salama hivyo kujisahau mpaka kufikiwa na ajali.
 
je tunaruhusiwa kuhusisha Imani?ushirikina na uchawi?
Hapana, interest hapa ni kujuwa tatizo la ubongo wa mbwa; kwanini aweze mambo makubwa halafu ashindwe jambo dogo tu la kuepuka ajali. Mbona wanyama wenye akili ndogo kuliko yeye (mbwa) wanaepuka ajali? Na wakati mwingine unaweza kukuta mbwa anaiona gari inakuja na yeye ndio anaingia barabarani. Hapo ndio inashangaza, na ndio nahoji ubongo wa mbwa unafanya kazi vipi?
 
Hoja dhaifu sana hii mleta uzi mbona hata binadsmu hugongwa sana na magari Kila siku?
Nimekuambia hivi, juzi nimesafiri kutoka Dar es Salaam mpaka Shinyanga, nimeshuhudia mbwa 6:wamegongwa, lakini sijashuhudia mtu hata mmoja amegongwa (simaanishi kuwa nataka mtu agongwe), hivyo unaweza kuona uwiano huo. Kama utataka kutafuta uhalisia wake, basi unaweza kukuta akigongwa mtu mmoja, basi watagongwa mbwa 1000 (uwiano). Hivyo, kugongwa watu hakuondoi ukweli kuwa mbwa wanagongwa kwa kiwango kikubwa sana, pengine kuliko wanyama wengine wote. Kwahiyo hoja yangu ina mashiko
 
Tabia za mbwa kutembea halafu kusimama katikati ya ROAD kinawapaonza sana
 
Back
Top Bottom