TheForgotten Genious
JF-Expert Member
- Jan 18, 2014
- 2,087
- 3,156
kidato cha nne na sita kuna topic inaitwa Genetics kuna kipengele kinaitwa colour blindness wamedadavua kwa kina sana na kidato cha tatu na tano kuna topic inaitwa coordination and sensitivity wameelezea sana.Hili ni Somo jipya kwangu.
Hoja iliopo mezani, ni mbwa kugongwa sana, ukilinganisha na wanyama wengine, wafugwao, hata wanyama pori na binadamu hugongwa, ila leo amejiuliza juu ya mbwa.Hoja dhaifu sana hii mleta uzi mbona hata binadsmu hugongwa sana na magari Kila siku?
Hajashuhudia wakigongwa, kasome vizuri alichoandika.Hao mbwa 6 uliowashuhudia wakigongwa na magari wote walipona kweli ?!?
Aise nimeshudia pale mataa ya chang'ombe polisi, mbuzi wanavuka kwa kutumia zebra.Macho yake yapo mbele hayapo pembeni mbuzi na ng'ombe si rahis kugongwa ndo maana hadi buguruni mbuzi wamavuka barababra kuzidi watu
Juzi nimesafiri kutoka mkoa wa Dar es Salaam kwenda mkoa wa Shinyanga. Kijiografia, ni umbali mrefu, ambapo magari ya abiria hutumia si chini ya masaa 16 kufika mwisho wa safari.
Sasa kuna jambo moja nimeliona katika safari hii ndilo nataka wajuvi wa mambo ya wanyama watueleze, kwani ni jambo la kufikirisha kidogo!
Mnyama mbwa, ni miongoni mwa wanyama wanaotumiwa na binadamu katika shughuli mbalimbali za kijamii, kama ulinzi, kunusa, nk. Lakini pia, mnyama huyu anaweza kufundishwa michezo mbalimbali na akamudu kuicheza sawia.
Kwa muktadha huo, inaonyesha kuwa, mbwa ana akili pengine kuliko wanyama wengine, na ndiyo maana ni rahisi kwake kufundishika, tofauti na wanyama wengineo (most).
Sasa juzi katika safari yangu hiyo, nimeshuhudia si chini ya mbwa 6, mahala tofauti tofauti, wamegongwa na magari. Hapo ndio najiuliza, inakuwaje mnyama mwenye akili kuliko wengine; kama mbuzi, punda, paka, kuku, nguruwe, kondoo, ng'ombe, nk, anagongwa na magari wakati hawa wenye akili kidogo hawagongwi?!
Wakati tunajibu swali hili, majibu yetu tuhusianishe na ubongo wa mbwa, na sio factor nyingine kama uwingi wao, kukosa matunzo, kichaa cha mbwa, nk; kwani hizi ni hoja nyepesi. Mbwa wanaoongelewa hapa ni wakamilifu kwa mitazamo yote.
Mtu anaweza kuona nimeuliza jambo la kijinga, lakini wataalamu wa wanyama najuwa watakuja na sababu za msingi kuhusiana na jambo hili! Au wenzangu hamjawahi kijiuliza kwanini mbwa anagongwa kirahisi sana na magari kuliko wanyama wengine?
Hajashuhudia wakigongwa, kasome vizuri alichoandika.
nimeshuhudia si chini ya mbwa 6, mahala tofauti tofauti, wamegongwa na magari.
Naona gari ilikuwa inasukumwa [emoji1]Wanakuwaga na wenge sana wakati wa kuvuka barabara
View attachment 2630305NB: Huyo mbwa aliyegongwa pichani, alipona bila jeraha lolote.
kidato cha nne na sita kuna topic inaitwa Genetics kuna kipengele kinaitwa colour blindness wamedadavua kwa kina sana na kidato cha tatu na tano kuna topic inaitwa coordination and sensitivity wameelezea sana.
Tatizo hapo ndugu yangu, ni dogo tu, umeshindwa kutofauti nyakati, Neno, Wakigongwa, na wamegongwa unaweza kuona kama neno moja, ila linatofautisha nyakati, nadhani umenielewa.Je haya hapa chini sio maneno yake??![emoji1313]
Hivi hizi tafsiri za wanyama huwa mnazitoa wapi,Mimi niseme hivi; binadamu tu ambaye anazo fikra naye anaweza kugongwa na gari sembuse mbwa?!--- mbwa mara nyingi huwa muoga kama utamtishia kumpiga fimbo au jiwe, yeye anajua hatari kutoka kwa binadamu ni jiwe na fimbo tu lakini hajui hatari ya kugongwa na gari linaloendeshwa na binadamu, yeye anajua gari ni kama kitu tu cha kawaida alichozoea kukiona kila siku katika mazingira yake mfano nyumba, mti, mawe nk hivyo haoni kama ni tishio kwa uhai wake ukiweka kutokuwa na uelewa juu ya neno "hatari".--- the same applies to the cat.
Tatizo hapo ndugu yangu, ni dogo tu, umeshindwa kutofauti nyakati, Neno, Wakigongwa, na wamegongwa unaweza kuona kama neno moja, ila linatofautisha nyakati, nadhani umenielewa.
Ni kwasababu mbwa hawaoni usiku. Siwezi kuelezea zaidi mm siyo mwana biologiaJuzi nimesafiri kutoka mkoa wa Dar es Salaam kwenda mkoa wa Shinyanga. Kijiografia, ni umbali mrefu, ambapo magari ya abiria hutumia si chini ya masaa 16 kufika mwisho wa safari.
Sasa kuna jambo moja nimeliona katika safari hii ndilo nataka wajuvi wa mambo ya wanyama watueleze, kwani ni jambo la kufikirisha kidogo!
Mnyama mbwa, ni miongoni mwa wanyama wanaotumiwa na binadamu katika shughuli mbalimbali za kijamii, kama ulinzi, kunusa, nk. Lakini pia, mnyama huyu anaweza kufundishwa michezo mbalimbali na akamudu kuicheza sawia.
Kwa muktadha huo, inaonyesha kuwa, mbwa ana akili pengine kuliko wanyama wengine, na ndiyo maana ni rahisi kwake kufundishika, tofauti na wanyama wengineo (most).
Sasa juzi katika safari yangu hiyo, nimeshuhudia si chini ya mbwa 6, mahala tofauti tofauti, wamegongwa na magari. Hapo ndio najiuliza, inakuwaje mnyama mwenye akili kuliko wengine; kama mbuzi, punda, paka, kuku, nguruwe, kondoo, ng'ombe, nk, anagongwa na magari wakati hawa wenye akili kidogo hawagongwi?!
Wakati tunajibu swali hili, majibu yetu tuhusianishe na ubongo wa mbwa, na sio factor nyingine kama uwingi wao, kukosa matunzo, kichaa cha mbwa, nk; kwani hizi ni hoja nyepesi. Mbwa wanaoongelewa hapa ni wakamilifu kwa mitazamo yote.
Mtu anaweza kuona nimeuliza jambo la kijinga, lakini wataalamu wa wanyama najuwa watakuja na sababu za msingi kuhusiana na jambo hili! Au wenzangu hamjawahi kijiuliza kwanini mbwa anagongwa kirahisi sana na magari kuliko wanyama wengine?
Ni kwasababu mbwa hawaoni usiku. Siwezi kuelezea zaidi mm siyo mwana biologia
Hapana, interest hapa ni kujuwa tatizo la ubongo wa mbwa; kwanini aweze mambo makubwa halafu ashindwe jambo dogo tu la kuepuka ajali. Mbona wanyama wenye akili ndogo kuliko yeye (mbwa) wanaepuka ajali? Na wakati mwingine unaweza kukuta mbwa anaiona gari inakuja na yeye ndio anaingia barabarani. Hapo ndio inashangaza, na ndio nahoji ubongo wa mbwa unafanya kazi vipi?je tunaruhusiwa kuhusisha Imani?ushirikina na uchawi?
Nimekuambia hivi, juzi nimesafiri kutoka Dar es Salaam mpaka Shinyanga, nimeshuhudia mbwa 6:wamegongwa, lakini sijashuhudia mtu hata mmoja amegongwa (simaanishi kuwa nataka mtu agongwe), hivyo unaweza kuona uwiano huo. Kama utataka kutafuta uhalisia wake, basi unaweza kukuta akigongwa mtu mmoja, basi watagongwa mbwa 1000 (uwiano). Hivyo, kugongwa watu hakuondoi ukweli kuwa mbwa wanagongwa kwa kiwango kikubwa sana, pengine kuliko wanyama wengine wote. Kwahiyo hoja yangu ina mashikoHoja dhaifu sana hii mleta uzi mbona hata binadsmu hugongwa sana na magari Kila siku?