Kwanini mbwa hugongwa sana na magari barabarani?

Moja ya sababu ya kugongwa kwa mbwa ni la kibaiolojia zaidi tena wanaogongwa ni mbwa dume ipo hivi,mbwa jike anapokua katika heat period kwa binadamu wanawake tunasema wanapokua ovulation( yani siku tayari ya kupata mimba) mbwa majike uwa wanatoa harufu kama ishara yakuwa tayari kwa hilo tendo hivyo kutokana na uwezo wa mbwa kunusa mbwa dume anaweza akaisikia hiyo harufu toka mbali na inapelekea kuanza kutafuta mwelekeo wa hiyo harufu akitumia hisia zaidi na msukumo wa homoni bila kutumia akili katika matendo yake hivyo kutokujali uwepo wa barabara au magari ilimradi lengo lake litimie kwenye mwelekeo wa harufu kwenda kutimiza haja yake hapo ndipo huwa wanapogongwa!
 
Kuvuka barabara kunahitaji calculation zenye uhalisia za haraka sana na ambazo zinahitaji realtime respond.

Unapovuka barabara kwanza unakuwa umeshacalculate mwendokasi wako wa chini na wa juu unaoweza kukuvusha bila kugusana na object inayocross.
Pili calculation za haraka huwa zinafanyika kuhusu umbali wa gari inayopita na mwendokasi wake halisi kisha kuwianisha na mwendokasi wako wa juu na chini kisha kutoa jibu la haraka kwamba uvuke kwa mwendokasi gani ili usigongwe na gari.
Hesabu zote hizi zinafanyika ndani ya sekunde 1 na kukupa uamuzi wa kuvuka.

Sasa tatizo la mbwa kwanza hizo hesabu hapigi zote, anavuka tu kwa spidi.
Pili vyombo vinavyotembea kwa kuzunguka matairi, mbwa ana-detect kama kimesima, kikikaribia kumgonga ndio anashituka na anakwepa kwa kujiokoa.
Kuthibitisha hilo, mbwa anakuelewa vizuri ukiwa unamsogelea na baiskeli huku unazungusha pedeli kuliko ukiwa unamsogelea bila kuzungusha. Anakuona kama umesimama tu.

Nimejibiwa hapa na mtu mmoja.
 
mbwa wanagongwa sana kwa sababu moja tu
Kwa kawaida mbwa jike anapokua anajiskia kupandwa huwa anatoa harufu flani
Ambayo mbwa dume
Anapoiskia harufu hiyo anataka lazima afike kwa jike hilo akale mzigo

Sasa inapokea harufu hiyo inatokea upande wa pili wa barabara hapo ndio ajali inapomkuta
Maana ile harufu inakua imeshamvuruga kiasi ambacho anakosa umakini wa kuhahakisha usalama wake anachojali wakati huo ni kuwahi eneo la tukio tu.
 
Kigezo kimojawapo cha mnyama yeyote (akiwemo binadamu) kufundishika ni lazima awe na akili. Mnyama atashikaje mafunzo kama hana akili?
Ni kweli mbwa anafundishika hilo halijustify kwamba anaweza kuwa na akili maeneo yote, kuna wanafunzi wanaanza shule hawajawahi kushika nafasi ya tatu yeye ni MOJA hilo haliwapi guarantee kwamba wao ni bora kuliko yule wa tatu mwishoni
Tunayaona hata kwenye maisha halisi, halafu umejifunga kwenye factor za ubongo Ila kuna mtu amekuelekeza kuhusu vision hata mm KWA kiasi fulani nimemuelewa

Ungeruhusu mjadala uwe flexible KWA factor tofauti kama mfano wa mbwa koko kwahiyo wanatanga tanga hivyo risk yao ni kubwa pia


Umeweka mada KWA angle MOJA ilihali hata wewe hujui kama wale mbwa ni wazima au laah!! Maana uliwakuta chini wamekufa na ukushuhudia na huna historia ya mbwa hao
 
Mbwa labda umkanyage na tyre ndiyo unaweza kumuua lakini ukimbamiza tu anapona.
 
Nimeiguide hiyo topic kwa makusudi ili wataalamu watuchambulie jinsi mfumo wa ufahamu wa mbwa ulivyo. Hujawahi kukutana na mbwa anaona gari linakuja halafu yeye anacross barabara. Anafika katikati ya barabara, huku anaona gari imekaribia, anageuza kurudi alikotoka. Wakati anababaika hivyo ndipo gari humkuta na kumgonga. Hapo ndipo ninapohoji, tafsiri ya ubongo wake ikoje? Mbona wanyama wengine hawafanyi hivyo? Hiyo ndio sababu ililiyonifanya nilimit hili swali kwenye ubongo! Unaweza kuwauliza madereva juu ya hili ninalosema, au kama madereva mko humu, je, ninachosema ni uwongo?
 
Sawa mkuu mekuelewa
 
Macho yake yapo mbele hayapo pembeni mbuzi na ng'ombe si rahis kugongwa ndo maana hadi buguruni mbuzi wamavuka barababra kuzidi watu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Eti mwenyekiti wa vikao. Lol
 
Hii mpya mbna, khaaaah
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tatizo hapo ndugu yangu, ni dogo tu, umeshindwa kutofauti nyakati, Neno, Wakigongwa, na wamegongwa unaweza kuona kama neno moja, ila linatofautisha nyakati, nadhani umenielewa.
safi sana
 
Waafrika hatujali wanyama wengine unagongaje mnyama?
 
kuna mtu alijaribu kukutetea hapo kwenye bold akidhani hukumaanisha hvyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…