Kwanini mgeni akiulizwa "unaondoka lini" inakuwa nongwa?

Huu mfumo wa maisha wa kimagharibi umeepunguza mnoo upendo baina yetu, ukikaa na wazee wakusimulie maisha yao ya zamani, utaona upendo naa umoja ulitawala japo hawakuwa na kitu kivile, ila siku hizi chamgamoto, hatutembeleani, hatukirimiani kabisa, kila mtu kakumbatia watoto wake, mwisho hawajuani, zamani shule zikifungwa hata km mzee wako yupo town, unapelekwa kwwa ndugu iwe kijijini au wapi, mnakutana watoto kibao, mtakula kilichopo, ila siku hizi ni killa mtu na wake.
 
Mkuu kwa nini unahusisha hilo swali na kukosa upendo?
 
Swali linajieleza kabisa. Hili lipo sana kwenye familia za Kiafrika.

Nimepokea mgeni, kutokana na mipangilio ya kifamilia na kibajeti nalazimika kumuuliza atakaa hapa ugenini kwa muda gani.

Mara mgeni anaanza kusambaza taarifa mimi ni mbinafsi, sitaki kutembelewa 😂😂😂😂😂
Kwa nini uniulize ulize habari za sijui klnaondoka lini?
Kwani nikiendelea kuwepo na wewe ukauchuna utakaukiwa damu?
 
Ni kweli hiyo ishara ya ubinafsi na uchoyo sio utamaduni was mwafrica hasa mtanzania
 
kwa mimi sisubiri niulizwe,nitasema kabla hata sijafika
Mahusiano yenu na ndugu hayako sawa mm nikienda kwa ndugu hawezi niuliza nitaondoka lini na nikisema naondoka lazima aone nimekaa mda kidogo na wao ni vivo hivo wakija kwangu najisikia fahari sana hata majirani zangu nao wanaona na ndugu sasa kukaa km mchawi ww na mke na watoto ya nn hii.
 
Mfano ww unaenda kusalimia sehem umefika unaulizwa lini unaondoka si utajisikia vibaya sana.Haya tuwaachie wazungu sisi tusiige kila kitu mkuu.
Wageni sio wa kuwachekea hata kidogo "

we na maisha haya unabebana na watoto watatu ,unaenda kwa mtu yupo na single room unakaa zaidi ya two weeks ama mwezi mmoja"

ukute na ye apo yupo na watoto tena , siongei kama mfano ila najionea mwenyewe ..

mambo mengine tusioneane aibu mi binafsi nakuchana vp unakaa siku ngap , Kama ntaweza kumudu fresh , kama siwezi ntakuambia ucheki ustaarabu mwingne kwishaaaa..
 
Huu mfumo wa maisha wa kimagharibi umeepunguza mnoo upendo baina yetu, ukikaa na wazee wakusimulie maisha yao ya zamani, utaona upendo naa umoja ulitawala japo hawakuwa na kitu kivile, ila siku hizi chamgamoto, hatutembeleani, hatukirimiani kabisa, kila mtu kakumbatia watoto wake, mwisho hawajuani, zamani shule zikifungwa hata km mzee wako yupo town, unapelekwa kwwa ndugu iwe kijijini au wapi, mnakutana watoto kibao, mtakula kilichopo, ila siku hizi ni killa mtu na wake.
Siku hizi tunaogopana..unaogopa ukienda kumtembelea ndugu atajiuliza kama mtoa mada..[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sababu kubwa maisha yamebadilika..na sio umagharibi. Mimi mgeni wangu siwezi abadan kumuuliza lini au saangapi anaondoka..ila nawaelewa pia watu wanaouliza.
 
Wageni sio wa kuwachekea hata kidogo "

we na maisha haya unabebana na watoto watatu ,unaenda kwa mtu yupo na single room unakaa zaidi ya two weeks ama mwezi mmoja"

ukute na ye apo yupo na watoto tena , siongei kama mfano ila najionea mwenyewe ..

mambo mengine tusioneane aibu mi binafsi nakuchana vp unakaa siku ngap , Kama ntaweza kumudu fresh , kama siwezi ntakuambia ucheki ustaarabu mwingne kwishaaaa..
Upendo wa ndugu umepungua ndo maana hata shida zetu tumeshindwa kushirikiana km ndugu kuwa na ndugu ni utajiri tosha maana ukiwa na shida unashangaa unaambiwa piga no hii kuna mchele nimekutumia ama mahindi ila ww ukijifanya kauzu na maisha huna utapigika mpaka utakoma.
 
Siku hizi tunaogopana..unaogopa ukienda kumtembelea ndugu atajiuliza kama mtoa mada..[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sababu kubwa maisha yamebadilika..na sio umagharibi. Mimi mgeni wangu siwezi abadan kumuuliza lini au saangapi anaondoka..ila nawaelewa pia watu wanaouliza.
Muache apumzike kidogo maisha yenyewe magumu mtu kaona kimvuli kwanini aende juani
 
Upendo wa ndugu umepungua ndo maana hata shida zetu tumeshindwa kushirikiana km ndugu kuwa na ndugu ni utajiri tosha maana ukiwa na shida unashangaa unaambiwa piga no hii kuna mchele nimekutumia ama mahindi ila ww ukijifanya kauzu na maisha huna utapigika mpaka utakoma.
naona unapelekea swali kwenye uelekeo tofauti kabisa. Swali langu lina mahusiano gani na kushirikiana kama ndugu?
 
Siku hizi tunaogopana..unaogopa ukienda kumtembelea ndugu atajiuliza kama mtoa mada..[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sababu kubwa maisha yamebadilika..na sio umagharibi. Mimi mgeni wangu siwezi abadan kumuuliza lini au saangapi anaondoka..ila nawaelewa pia watu wanaouliza.
Ni kweli maisha yamebadilika, ila umagharibi pia unachangia..

Maisha ni kwa wale wakina sisi vipato vya chini, umepanga chumba kimoja, una mke na watoto, hapa sawa ni sababu ya kimaisha.
Ila wengine ni umagharibi ana life zuri, class A ila anayofanya ndio hayo ninayoyazungumzia.
 
Kichwa Cha habari tu kimenichekesha sana[emoji16]

Nilikua na baba mkubwa Wang mmoja niliishi kwake huyu mwamba bana ye ilikua akija ndugu yeyote anamuuliza utakaa siku ngapi? Au baada ya siku mbili akimuona hana Raman na hakuna alichofata anamuuliza unaondoka lini?

Hizo kauli ukizizoea kuziskia hata ukimaliza shule hautaman kukaa nyumban we mwenyewe tu utajiongeza inasaidia sana kufanya watu wawe wapambanaji kuliko kurundikana kwa ndugu huku hakuna ulicho fata zaid ya kuangalia Tv na kumuongezea mtu budget ambazo hakua nazo. Jamaa ilikua anapenda sana mtu anae jituma na kuchukia Sana watu waliokaa kaa kizembe

Japo kwa jicho la uswahili inatafsiriwa ni roho mbaya.
 
Kama ni salamu basi nisalimie hata kwa simu.

mje mjini kwa mipango muhimu tu tena ya kiuzalishaji
 
Mie hua nauliza 'upo mpaka lini' ili nijue vile nitafix ratiba yangu niweze enjoy na mgeni wangu. Pia kama anakaa siku chache nianze kumlaumu
Nishawahi kugeuzia gia angani nikamkomesha mtu kama wewe!

kaniuliza mjomba unakaa siku ngapi, nikamwambia mbili tu! akasema ooh mjomba hutupendi, kaa kaa hata wiki... dadek zake nilikuwa namcheki tu.. nilizamia miezi mitatu kipindi cha corona kile mpaka akanihamishia nyumba ya pili😄😄😅🤣

anko asante sana kokote uliko ulinisaidia sana
 
Nishawahi kugeuzia gia angani nikamkomesha mtu kama wewe!

kaniuliza mjomba unakaa siku ngapi, nikamwambia mbili tu! akasema ooh mjomba hutupendi, kaa kaa hata wiki... dadek zake nilikuwa namcheki tu.. nilizamia miezi mitatu kipindi cha corona kile mpaka akanihamishia nyumba ya pili[emoji1][emoji1][emoji28][emoji1787]

anko asante sana kokote uliko ulinisaidia sana
Mie napenda wageni maana sina ndugu labda kusema hana issue aje tu kukaa kwangu. Kila mtu ana issues zake. Hata mimi nikienda nyumbani mama ataniuliza hilo swali ni kama kautaratibu hivi haina kukomeshana ni kuangalia jinsi gani utaspend time na mtu wako.
Kama atakaa siku mbili inabid uache na shughuli nyingine ufocus kwake kwa muda huo mchache
 
Back
Top Bottom