Kwanini mgogoro wa Loliondo haukuibuka wakati Magufuli yupo hai? Hawa OBC ni akina nani? Kwanini Loliondo Gate? Mbona wanasiasa wa Oman?

Kwanini mgogoro wa Loliondo haukuibuka wakati Magufuli yupo hai? Hawa OBC ni akina nani? Kwanini Loliondo Gate? Mbona wanasiasa wa Oman?

Aiseee kwa hapa hapana, tumuache mzee wa watu aendelee kucheza vizuri na vitukuu vyake, kuanza kumuuliza kuhusu haya mambo kunaweza changia kumkosa sio muda.

Hii ngoma imevuma wakati huu wa utawala awamu ya 6, ichezwe makidamakida mukidemukide na aliyeko madarakani
Mambo ya uongozi kama kweli tuko makini hakuna cha tumwache! Aliuza nchi full stop, anastahili adhabu au hata kuulizwa, Mwarabu anafaida gani zaidi ya wananchi?
 
Mzee wa watu huenda alifariki tu Kwa maradhi yake, lakini Kwa hizi sarakasi zinazoendelea, unawezakujikuta unaamini tetesi kwamba kifo chale kina namna.
Ile betri (pacemaker) aliyowekewa kwa michango ya wanafunzi wenzake UDSM ilikuwa kwa unachokiita "sarakasi zinazoenedelea sasa"?
Ignorence is bliss
 
Magufuli ni mjinga tuu alikuwa muoga wa ku face reality kwa sababu hajiamini na analazimisha kupendwa..

Hilo la Ngorongoro alilifumbia macho kama tuu ambavyo alifumbia macho kuzagaa hovyo kwa machinga..

Magufuli aliruhusu hadi Polisi kuchukua rushwa akisema ni vihela vidogo vidogo...

Zaidi ya propaganda hakuna kitu chochote cha maana alifanya..

Namkubali Rais Samia Kwa sababu hana mda wa kufanya cheap politics,kulazimisha kupendwa kwa maigizo na yuko straight kama ni nyeusi ni nyeusi tuu..

Masai lazima wapishe,haiingii akikini wanaharibu hifadhi Kisa nini?

Wewe utakuwa unaishi kongo hata sami 100 anapenda kusifiwa na kila siku tunawasikia viongozi na machawa kama kina mwijaku...hakuna Rais asiyependa sifa na cheap politics.......kila keo tunaona mabango na matisheti ya Mama anaupiga mwingi unafikiri yanatoka wapi kama sio kitengo cha kusifu na kuabudu?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Oterlo business Corporation ni akina nani? Na kwa nini wanalitaka hili eneo la Loliondo tokea miaka ya utawala wa Mwinyi?

Loliondo gate kuna nini? Kwa nini wakati wa hayati JPM haya masuala hayakuibuka?

Hawa OBC wana siri kubwa na nzito hawa sio watu wema.

Mkuu wa nchi anashiriki kutwanga vitu vizito raia maskini wasio na mbele wala nyuma.
Mbaya zaidi kwanini waarabu hawalalamiki?
 
Kuwahamishia wamasai kwenye makazi ya 'mjini'ni kuwadhulumu haki yao! Wao wanahitaji uhuru wa kufanya mila na desturi zao. Wanahitaji kukimbia na kuruka hukohuko maporini. Kuwajengea nyumba na kuwalazimisha kuishi maisha ya kisasa ni uonevu.
Umeshusha point tupu mkuu
 
Back
Top Bottom