Kwanini miaka chini ya 2000 matikiti maji yalikua adimu?

Kwanini miaka chini ya 2000 matikiti maji yalikua adimu?

Mhandisi Mzalendo

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2010
Posts
6,682
Reaction score
11,461
Tokea nianze kupata ufahamu mwishoni mwa miaka ya 80 mpaka mwanzoni mwa miaka ya 2000, sikuwahi kuona mtu anakula tikiti maji wala mimi kula... Je Tunda hili limepata umaarufu kwa ajili ya nini ? Maana zamani kilikua chakula cha nguruwe na ng'ombe kama ilivyo malapu lapu ya mbwa siku hizi mnaita michemsho...
Tikiti maji kwa nini zamani hatukula?
 
MATIKITI MAJI YALIKUWEPO ILA YALE YA ASILI YANAPANDWA MASIKA HADI MASIKA NA HAYAKUWA MENGI,
Umenena kweli mkuu na hili ndiyo jibu matikiti ya sasa hivi ni yale ya laboratory siyo ya asili ndiyo maana kila siku yapo tu hayana msimu zamani matunda yalikuwa yana msimu na unajulikana kipindi hiki ni msimu wa embe baadaye nanasi, machungwa nk siku hizi mambo ya mabadilika mwaka mzima matunda yapo maana ni matokeo ya laboratory tutaachaje kuumwa?

Ndiyo maana yale magonjwa waliokuwa wanaumwa watu wazima nayo siku hizi hadi watoto wanayo chanzo.....
 
tusubiri korosho bandia
 
First of all let me declear interest mimi ni afisa kilimo hivyo ngoja nikujibu kitaalam kidogo!
Pana mambo kama mawili au matatu hivi yaliyokua yanasababisha hiyo hali unayoiona lakini kubwa kabisa ni kilimo kutokua cha KIBIASHARA.
Utakubaliana na mimi kua kwa miaka ya hivi karibuni atleast watanzania tumeanza kukiona kilimo kwa mtazamo tofauti, na kuanza kulima kibiashara sasa hii imepelekea wakulima kuanza kulima si tu kwa kutegemea msimu wa mvua bali kwa kumwagilia kwa njia mbali mbali kuanzia visima, kumwagilia kwa kutegea maji mtoni mpaka kwa njia ya matone ikiwa ni mapinduzi ya kisayansi mpaka sasa katika sekta yetu ya kilimo.

Sababu nyingne kubwa zaidi ni uwepo wa mbegu za kisasa za mazao mbali mbali ikiwemo na hizo za matikiti kwani haya ya kisasa yamekuja na sifa ambazo zile mbegu zetu za asili hayakua na uwezo wa kua nazo ndo mana yakafanya zao hili kutokua maarufu!.
Mbegu za kisasa zmekuja na sifa za kukomaa mapema ndani ya siku 60 - 75 tayari linakua limekomaa tayari kwa kupelekwa sokoni pia matikiti yake yanakua makubwa (baadhi ya varieties zinaenda mpaka kilo 7 - 10 Kwa tunda moja) kitu ambacho matikiti yetu ya asili hayakua na uwezo huo wa kua makubwa kwa kiasi hiko pia varieties za kisasa matikiti yake ni matamu sana (sina haja ya kulielezea hili sote tunafahamu) na per one acre unaweza kuvuna zaidi ya tani 20
Kwa sababu hizi nadhani utakua umenipata!
 
Back
Top Bottom