Kwanini Micky Jnr anachochea sana moto Tanzania wapokonywe nafasi yao AFCON apewe guinea?

Kwanini Micky Jnr anachochea sana moto Tanzania wapokonywe nafasi yao AFCON apewe guinea?

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
15,966
Reaction score
26,404
I salute you kinsmen.

Huyu jamaa kwa sasa amezidi kututibua nyongo watanzania kwa kiasi kikubwa sana

Inasemekana kuwa Tanzania wanaweza kupokonywa nafasi yao kushiriki Afcon na akapewa Guinea sababu hasa ni kuwa jamaa wameandika barua CAF kuwa.

Tanzania kumchezesha mchezaji ambaye namba anayovaa na iliyoandikwa kwenye ubao ni tofauti yaani 24 na 26 ambaye alikuwa ni Ame.

kupangiwa match officers ambao walikuwa wanatoka Kenya yaani CECAFA zone hivyo ni upendeleo.

Kubadilisha muda wa match kutoka saa 1 kwenda 10 jioni.

Haya yote ni nonsense kabisa Guinea wanatapa tapa tu hawana la maana sababu
Yote hayo hayana mashiko.

mchezaji aliyeingia alikuwa ni Ame ni si mwengine hivyo hakuna ubadhilifu hapo.

kuhusu kubadilishwa match muda Shirikisho liliomba CAF mapema match ichezwe mapema.

kuhusu match officers kutoka Kenya ni CAF ndiyo wamepanga sio sisi .

Sasa huyu limwandishi tapeli kutoka Ghana limeshikilia bango sana kuhusu hili swala mpaka unajiuliza kama amelipwa na Guinea?

Ni kama post ya 10 hii anazungumzia jambo moja hilo hilo yaani anamwaga petrol kwenye moto!

Mambo mengine huwa hakazii sana hasa mabwana zake waarabu wanaomlipa hela huwa anaongelea mazuri tu sana sana ahly ahly na wydad pia team takataka Simba.

Je, amelipwa au namna gani au sababu taifa lake halijafuzu anataka tukose wote?

Kinachokera matanzania mapumbavu na majinga yamejaa kwenye page yake yanamsapoti na kumpetipeti kila jambo yanasifia na kujipendekeza yaani huu utahira watanzania tutaacha lini?

Kwanini tunakosa uzalendo kabisa?
Unadhanj ingekuwa nchi yake ya GHANA ndiyo ina scenario kama ya Tanzania je angeshikilia bango hivi?

Acheni upumbavu
 
Pointi ya kwanza ina mashiko ningekuwa mtoa maamuzi wa CAF ningewadisqualify Tanzani
Tupe sheria zao CAF zinasemaje kwanza?

Sababu mchezaji aliyeingia ni AME halafu namba waliyotaja kwenye bango sidhani kama inavaliwa hapa national team
 
Mimi siyo mwanasheria! Ila sioni kama kuna kesi hapo. Halafu huyo jamaa hata simfahamu eti!! Labda nimuulize Kalpana anaweza kunipa darasa la kutosha kumhusu huyo jamaa.
 
Sio sheria baki kanuni,kila mchezaji atakayeshiriki mchezo,jina lake lipelekwe CAF sanjali na namba yake ya jezi,sasa namba ya Ame sio iliyowasilishwa CAF
Sawa. Nimekupata. Hata kama mimi sio mwanasheria, Je, kama mchezaji jina lake lilipekwa CAF, hivi tofauti ya namba ya jezi inaweza kuwa issue kubwa sana?
 
Sawa. Nimekupata. Hata kama mimi sio mwanasheria, Je, kama mchezaji jina lake lilipekwa CAF, hivi tofauti ya namba ya jezi inaweza kuwa issue kubwa sana?
Sijajua hapo kuna wakat kanuni haziko wazi sana maana ni kitu hakitarajiwi kutokea,nimepekua sijaona adhabu kwa hilo kosa,ila wakiamua kukuadhibu wanaweza
 
Sijajua hapo kuna wakat kanuni haziko wazi sana maana ni kitu hakitarajiwi kutokea,nimepekua sijaona adhabu kwa hilo kosa,ila wakiamua kukuadhibu wanaweza
Wanawezaje kukuadhibu na huna kosa?
 
Yaani ni mashabiki wa hiyo team nawajua vizuri sana wanajipendekeza sana kwake hata kama anawatukana yaani mashabiki wa Simba ni hasara kwa nchi hii inabidi waende Ghana huko wakamfuate si wanampenda sana?
sawa basi tunaomba utupe nauli tuende ghana
 
"
Kwanini tunakosa uzalendo kabisa?
Unadhanj ingekuwa nchi yake ya GHANA ndiyo ina scenario kama ya Tanzania je angeshikilia bango hivi?"

Mzalendo nchi hii alikuwa Nyerere TU. Na wengine wengi ambao hawajulikani yaani unakuta wazalendo lakini pia sababu Wana njaa.....
 
Yeye ni mwandishi tu kama alivo shafih dauda hayuko kwenye kamati za caf na hana ushawishi wa kuingilia maamuzi ya caf labda utwambie kama yeye kama mwandishi wa habari za michezo ameripoti tofauti na shirikisho la genea lilivotuma hio case caf ni sawa. Hata hivo nimeona leo channel ten pia wqmeongelea hio kitu na tanzania tumefanya kosa.
 
kilichonipa faraja ni kwamba, mchezeji bishaniwa alikuwa kwenye list, alikaguliwa na timu pinzani na kamisaa. shida ni jezi tu sio mchezaji. na kwamba kosa kama hilo likitokea huwa kuna adhabu, na adhabu mojawapo ni faini, kufutiwa kama itakuwa serious. sasa ya kwetu haiwezi kusemekana kuwa ni serious fraud wakati alikuwa kwenye list na alikaguliwa na wapinzani. itadondokea kwenye faini tu.
 
Back
Top Bottom