Kwanini mikoa hii minne (4) hutajwa sana katika matangazo mbalimbali ya biashara kwenye redio na runinga?

Kwanini mikoa hii minne (4) hutajwa sana katika matangazo mbalimbali ya biashara kwenye redio na runinga?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
1. Dar es Salaam

2. Arusha

3. Mwanza

4. Mbeya

Kama Tanzania nzima ina jumla ya Mikoa 31 kama sijakosea baada ya mingine kuongezeka ikiwemo yangu ya asili ya Mara (Musoma) na Mtwara (Masasi) ni kwani nii hii Minne (4) tu tajwa hapa ndiyo hutajwa mara kwa mara?

Ila ninachofurahi hata mikoa ya watani zangu wakubwa Wahaya, Wanyiramba, Waha, Wanyaturu, Warangi, Wakara na Wanyamwezi nayo pia haimo na ningeshangaa sana kusikia kama na yenyewe ingetajwa (ingekuwepo) kwani ni mikoa ya watu masikini na washamba tupu, ila wakija mkoani Mara ndiyo huja kutajirika na kujanjaruka.

Watani mpo?
 
Sababu hiyo Mikoa ndio Tanzania
Kwahiyo Kagera, Singida, Kigoma, Dodoma na Tabora wanakotoka Watani zangu siyo Tanzania?

Mkuu Mimi ni Mtani wao mkubwa hapa JamiiForums na Nawamudu je, nawe una Utani nao ili wasije Kukupararua kwa Kutoithamini hiyo Mikoa yao?
 
Hayo ni majiji yenye uwekezaji mkubwa na yapo kikanda zaidi. Dar kanda ya pwani, Arusha kaskazin, Mwanza kanda ya ziwa, Mbeya Nyanda za juu kusini.
Kwahiyo hii Mikoa ya Masikini na Washamba ya Kagera, Singida, Kigoma, Dodoma na Tabora yenyewe siyo ya Kikanda?
 
Uuzi zako mkuu unazilewa mwenyewe naona kama umeishiwa mada mpya, basi uwe unasoma za wengine sio lazima

Sasa kasema uongo? Kibiashara mikoa hiyo minne hutajwa sana mwisho kachomekea utani kwa sisi watani zake huyo mnywa uji wa mtama mwekundu usio na sukari hadi aombe kwa babu zake, kila siku aandike maada za akina kibu denis ndio furaha yenu?
 
Asante Mkuu na tupo pamoja japo kuna Mtu Mmoja Covax anadhani GENTAMYCINE anayenichukia Nimekurupuka tu Kuuanzisha huu Uzi.
Wenye chuki waache na chuki zao mkuu wewe tuletee mada km hizi tuenjoy, kwenye watu 10 huwezi kukosa wawili wasiokufurahia Ila wapo 8 wanaokukubari
 
Ututolee vurugu ndio maana samaki waliwakimbia wakahamia bukoba, mtama mwekundu mbegu watu waliiba kwa sasa unapandwa na kustawi singida, hamna jipya mtulie tu mmebaki mnamiliki sauti za kufoka na besi, kama mbegu za mtama mliibiwa mna nini tena
 
Nimesoma nimerudia na kurudia na rudia sijaelewa.

1 .Anyway nijibu kwa Utafiti Gani ulio ufanya ukajua ni mikoa ijayo tajwa tajwa????

Huo Utafiti utapelekea wewe kupata majibu kujua ni kwanini Huwa inatakwa tajwa.

2. Hivi kweli mtu Mwenye akili timamu usijue Jiji la Dar es salamu kwa nini always linatakwa!!!!!!

Dar es salaam- kitovu Cha Biashara , Siasa, Vyombo vya habari, Mji mkongwe, Bandari, Ikulu nk.
Lango la nchi

Arusha.
Ina vivutio vingi vya utalii.
Mji wa kitalii.

Mwanza.
Mji wa kibiashara
Madini , samaki, ziwa Victoria kilimo pamba nk.

Mbeya.
Inapakana karibu na nchi Tatu
Kilimo ndio kwao. Mbeya ndio inailisha Tanzania.
Biashara za kutosha.
Magari kutoka south, Malawi,Zambia,
 
Ila nilikwambia Usome kitabu Cha Mwalimu Nyerere.

KINAITWA TUJISAHIHISHE.

Isitujazie seva za Jf.
 
Dodoma haisahauliki siku hizi maana purchasing power imehamia huku.
Yaani Watani zangu Warangi wawe na Purchasing Power kuliko Sisi Wazanaki, Wakurya, Wajita na Wajaluo kutoka Kwetu Mkoani Mara? Mkuu are you Serious?
 
Yaani Watani zangu Warangi wawe na Purchasing Power kuliko Sisi Wazanaki, Wakurya, Wajita na Wajaluo kutoka Kwetu Mkoani Mara? Mkuu are you Serious?
Hapa saivi kila kabila lipo hapa hao wagogo na warangi wamekimbilia porini huko
 
Back
Top Bottom